mbinguni
JF-Expert Member
- Jan 2, 2013
- 2,746
- 1,051
Mzee wa uliberali anadhani Elerai ni Zenji?Asubiri June 16, 2013 ataisikilizia kwenye bomba chadema itakavyowaunguza cuf na wenza wao,ccm.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hammad amekirushia kombora Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kile alichodai kinapoteza mwelekeo kutokana na fujo nyingi zinazotokea wakati wa vikao vya Bunge. Alisema fujo hizo, ni wazi zinaonekana kusababishwa na uroho wa madaraka.
Maalim Seif alitoa kauli hiyo juzi jijini hapa, wakati wa kampeni za kumnadi mgombea nafasi ya udiwani wa Kata ya Eralai, John Bayo.
Alisema wakati CUF, ilipofanikiwa kuongoza Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni chini ya uongozi wa Hammad Rashid Mohamed, kulikuwa na busara za hali ya juu katika uendeshaji wa vikao vyao.
Alisema kutokana na umoja na uaminifu ambao CUF ilikuwa nao, ndiyo ilimteua Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilbroad Slaa kuwa Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni.
Wakati CUF inaongoza Kambi ya Upinzani Bungeni, tulikuwa na umoja mno, tulishirikiana na vyama vyote vya upinzani na naibu wetu, alikuwa Dk. Slaa.
Ila wao Chadema, walipopata wakaanza kusema wao ni wao, ndugu zangu ndio maana leo hii mnaona Bunge limekuwa la fujo utadhani soko, watu wanamwaga matusi kama cherehani, maadili ya Bunge yameachwa, alisema Hammad.
Alisema CUF ni chama chenye dira na kinachoona mbali, kwa sababu kimeundwa kwa lengo la kutetea maslahi ya wananchi wote na dira yao.
Kwa upande wake, Bayo akiomba kura alijikuta akiangua kilio mbele ya wananchi waliokuwa wakimsikiliza.
Bayo, ni moja ya madiwani waliotimuliwa CHADEMA kwa madai ya kupokea rushwa na kukisaliti chama hicho.
Sijagusa hata senti kwa ajili ya kuwasaliti watu wangu, najua kitendo hicho kinakiuka maadili na kuwasaliti nyinyi mlionichagua.
Kwa hisani ya Mtanzania.