Uchaguzi 2020 Maalim Seif: CCM imeweka mikakati yake ya kumtafutia ushindi Dkt. John Magufuli, Tundu Lissu aje nimpe mikakati ya kushinda kwenye Uchaguzi

Tatizo hujui kilichopo. Watu wa deep state wanaelewa kila kitu. Kwanza fungua fumbo LA mzimu wa 2015 Kule Zanzibar na kilichojiri. Hivi unaamini Maalim ashiriki tens uchaguzi kwa mazingira Yale Yale? Jiulize kunani? Think big. Kichwa unaambiwa kinatoka ACT.

Lissu nenda kwa Maalim ukachukue mbinu, nenda.
Maalim kaanza 2015 kulalamika kuporwa ushindi?

2016 alitwambia atakabidhiwa nchi yake baada ya miezi 3,vipi alikabidhiwa?
 
Maalimu seif safari hii, anashindwa kwa tofauti kubwa kuwahi kutokea katika historia ya uchaguzi zanzibar. Kijana mchapakazi Hussein Ally Hassan Mwinyi ndiye chaguo la kizazi kipya
Sief anafikiri bado yuko 60s ambako kiazazi chake ni kile cha kupinga muungano!

Sasa hivi kuna kizazi kipya kabisa kilichozaliwa ndani ya muungano! Ambao wako huru kuja bara kununua ardhi na kuwekeza kwenye biashara watakavyo sasa wakimtafakari Seif hawamwelewi kabisa.
 
Tundu Lissu kura tunakupigia.. na tutazilinda. Mikakati hiyo ya hawa jamaa ya wizi please ujiandae namna ya kukabiliana nayo. Kama kuna ambacho wananchi tunatakiwa kufanya cha ziada tujulishe. Sasa hivi enough is enough. Hatutaki tena kuongozwa kwa masimango na dhulma. Tunakutaka wewe.
Hivi Lisi anakura za kuibiwa kweli?

Mtu anaepata si zaidi ya 20% unamuibia kitu gani hapo?
 
Mgombea aliyewahi kushindwa na CCM hiyohiyo mara tano, Leo amekuwa fundi wa kuwapa Mbinu wengine kushughurika na CCM hiyohiyo.

Hivi, mpaka muda huu, bado kunamjinga anaamini CCM itashindwa mwaka huu, Walishindwa kuing'oa 2015 wakiwa na ukawa wenye Vyama zaidi ya vinne na wanasiasa wakongwe na maarufu na wenye uzoefu wa kisiasa mara tatu zaidi yao, waje kuweza leo?

Ujinga kwelikweli!!
Hata Goliathi alipigwa na mtoto.
 
Sief anafikiri bado yuko 60s ambako kiazazi chake ni kile cha kupinga muungano!

Sasa hivi kuna kizazi kipya kabisa kilichozaliwa ndani ya muungano! Ambao wako huru kuja bara kununua ardhi na kuwekeza kwenye biashara watakavyo sasa wakimtafakari Seif hawamwelewi kabisa.
Maalim si wa kubezwa 2015 alikaba kila kona hadi CCM wakasema uchaguzi haukuwa huru na haki wakati tume yao, jeshi lao, usalama wa taifa wao, vyombo vya habari vyao halafu bado walilia mchana kweupe uchaguzi haukuwa huru. Wakalazimisha kuufuta kitu ambacho hakijawahi kutokea tangia dunia iumbwe.
Sasa wewe mdharau tu ila Zanzibar CCM hawana amani kabisa.
 
Mgombea aliyewahi kushindwa na CCM hiyohiyo mara tano, Leo amekuwa fundi wa kuwapa Mbinu wengine kushughurika na CCM hiyohiyo.

Hivi, mpaka muda huu, bado kunamjinga anaamini CCM itashindwa mwaka huu, Walishindwa kuing'oa 2015 wakiwa na ukawa wenye Vyama zaidi ya vinne na wanasiasa wakongwe na maarufu na wenye uzoefu wa kisiasa mara tatu zaidi yao, waje kuweza leo?

Ujinga kwelikweli!!
Wajua balbu ya umeme ilijaribiwa mara ngapi mpaka ikawaka? Mataga mnashida gani?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Mgombea aliyewahi kushindwa na CCM hiyohiyo mara tano, Leo amekuwa fundi wa kuwapa Mbinu wengine kushughurika na CCM hiyohiyo.

Hivi, mpaka muda huu, bado kunamjinga anaamini CCM itashindwa mwaka huu, Walishindwa kuing'oa 2015 wakiwa na ukawa wenye Vyama zaidi ya vinne na wanasiasa wakongwe na maarufu na wenye uzoefu wa kisiasa mara tatu zaidi yao, waje kuweza leo?

Ujinga kwelikweli!!
Seif hajawahi kushindwa uchaguzi wowote Zanzibar na hata wewe ni shahidi.

Hata huku Tanganyika ni vigumu sana kujua ukweli kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ushindi wa ccm kwa kuangalia hii tume yao inavyosimamia hizi chaguzi. Inatia shaka sana.
 
Maalim si wa kubezwa 2015 alikaba kila kona hadi CCM wakasema uchaguzi haukuwa huru na haki wakati tume yao, jeshi lao, usalama wa taifa wao, vyombo vya habari vyao halafu bado walilia mchana kweupe uchaguzi haukuwa huru. Wakalazimisha kuufuta kitu ambacho hakijawahi kutokea tangia dunia iumbwe.
Sasa wewe mdharau tu ila Zanzibar CCM hawana amani kabisa.
Ni enzi hizo si wakati huu! Seif kachoka na kizazi chake pia kimechoka..

Kizazi kinachopiga kura zanzibar wakati huu ni kile kilichozaliwa ndani ya Muungano
 
MAALIM Seif Sharif Hamad, Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo anataka kukutana na Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema ili ampe mikakati ya ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

Maalim Seif ambaye ni Mwenyekiti chama hicho ametoa kauli hiyo jana Jumanne tarehe 22 Septemba 2020 katika mkutano wake na timu za ushindi za mikoa na majimbo ACT-Wazaendo za Unguja.

“Kule bara kuna mikakati yao yote nimeshaambiwa na mimi nataka nikutane na Lissu nimpe mikakati hiyo na nimwambie akiweza kuzuia mikakati hiyo wamekwisha hawa,” alisema Maalim Seif.

Kuhusu uchaguzi huo, Maalim Seif aliswma mpinzani wake wa karibu Dk. Hussein Ali Mwinyi, Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM anapaswa kujiandaa kushindwa huku akimtaka Dk. Magufuli kukusanya virago vyake kwa maelezo kwamba hawatashinda katika Uchaguzi Mkuu huo.

“Mara hii rafiki yangu Magufuli ajiandae kufunga Virago vyake na Hussein Mwinyi akikubali ajiandae kua Makamu wangu wa Kwanza wa Rais. Mara hii kichwa lazima kitoke ACT-Wazalendo,” alisema Maalim Seif.

Hivi karibuni, Lissu akiwa Zanzibar alitangaza kumuunga mkono Maalim Seif kwenye mbio za urais huku Maalim Seif naye ameweka wazi kumuunga mkono Lissu. Chadema imesimamisha mgombea urais wa Zanzibar, Said Issan Mohamed ambaye Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemteua kugombea urais.

Pia, ACT-Wazalendo imemsimamisha Bernard Membe, kugombea urais wa Tanzania na tayari amekwisha zindua kampeni zake za urais mkoani Lindi ingawa kwa sasa haendelei na kampeni.

Jana Jumanne, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe akihutubia mkutano wa kampeni wa mgombea Ubunge wa Tabora Mjini kupitia chama hicho, Msafiri Mtemelwa alisema, mazungumzo ya kushirikiana yamekamilika.

Zitto alisema, mazungumzo ya kusimamisha mgombea mmoja wa nafasi ya urais, kuachiana majimbo na kata nayo yamenalizika na tarehe 3 Oktoba 2020 katika mkutano wa kampeni
Hiyo mikakati ya ushindi kwa nini Maalim Seif asimpe mgombea wake Membe? Kwani ni kulikoni ACT si kuna mgombea Urasi wao?
 
Kachero mbobezi ndo Kwisha vile..
Mlitegemea mteremko sasa wapinzani wameamua kufanya mambo kiakili kwelikweli mnasota wachoma nyavu nyie lisu kasema anatulipa bomoabomoa vyeti feki hawa wamefundisha watu wakada mbalimbali madactor waalimu mahakimu watendaji leounawafukuza kwa aibu
 
Ccm hawana kipigo cha kumpiga mtu akalia, bali wanawizi tu ndio wanaotumia, sasa safari hii mtajamba cheche na mtakunya moto.
 
maalim seif ni sayari nyengine acha mazoea mara hii hali yenu ni ngumu zaidi pande zote, jiulize swali 1 tu moyoni mwako, kwanini maalim seif ameijua mikakati ya jiwe kupewa ushindi mapema hivi? ni wazi huko juu kumeoza wachawi wanaomtafuna jiwe ni wengi ambao utawaona bega kwa bega pamoja naye lakini nje ya hapo ni nyoka.
Ajiulize pia kwanini Jiwe kaenda mapimzikoni mara tu chopa ilipozinduliwa na chama chake?? Ukweli ulio wazi hivi sasa Uongozi wa juu wa ccm unahaha kwa kila namna kumpatia Mgombea wao wa Urais ahueni.
 
Yeye mwenyewe ameshindwa kutumia hizo mbinu halafu anataka kumpa mwenzake.
 
Back
Top Bottom