Maalim Seif awaponza viongozi wa Jeshi la Polisi Pemba, yaamriwa wavuliwe vyeo

Tumeichoka amani,tumevimbiwa,wanaichezea Zanzibar bila.kujua vita ya nchi yetu itaanzia Zanzibar na kisha itasambaa Tanzania Bara yote.

Huu ulevi wa madaraka wa ccm utatuingiza kwenye machafuko very soon.

Bashiru Ally anakwenda kufanya siasa Zanzibar na huyo masauni na makamanda wote wanahudhuria mikutano yake .

Halafu Maalim Seif na Makamu wa kwanza wa Rais anaambiwa asifanye mikutano?

Sasa wasimamisheni au mkamateni maalim Seif mumuweke jela mpate mnachomitaka.

Acheni ujinga msituiletee machafuko,Wazanzibar wanahasira sana na wamefikia hatua ya kuona hawana cha kupoteza.

Wachezeeni Watanganyika ambao wamejawa na woga,lkn kanuni ya machafuko huwa yanaanza eneo dogo kisha yanasambaa.

Case study iwe machafuko ya Mtwara.polisi walishindwa kuwadhibiti,mahakama zilichomwa,vituo vya polisi vikachomwa,halmashauri zikachomwa magari yake pamoja na magereza kuvunjwa.polisi wa Dar,Lindi na Mtwara walishindwa mpaka jeshi lilipoingilia kati.

Sasa nawakbusha tu kuwa muache ulevi,nchi yetu tunaipenda,katiba inawaruhusu kufanya siasa ,msituharibie nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo siku hizi maamuzi yanatolewa kwenye vyombo vya habari , official protocals tupa kule.
 
Naibu Waziri wa mambo ya ndani Hamad Masauni amemwagiza IGP Sirro kuwavua vyeo RPC wa Kusini pemba Hassan Nasir Ally na RPC wa Kaskazini Pemba Shekhan Mohamed kwa kosa la kumwacha Jabali Maalim Seif kuhutubia wananchi wa Pemba , huku siasa za majukwaani zikiwa zimekatazwa


Zanzibar si wana serikali yao kamili, iweje waziri wa Bara akawanyifoe askari Zanzibar waliko na bendera yao, wimbo wao wa taifa na rais wao
 
Kangi Lugola yuko wapi akanushe habari hii?
ALIWAHI KUSEMA JESHI LA POLISI HALIFANYI KAZI KWA MAAGIZO YA CHAMA CHOCHOTE.
 
ndammu,
Mwaka 2001 ulikuwa na umri gani mkuu? Kawaulize waliokimbilia shimoni
Mkuu sikiliza ya 2001 sio ya leo hata wewe ulipokuwa 2001 kimaisha sio ulipoleo.

Ikiwa akili zenu haziendi na kufanya kazi bila ya policcm msijidanganye.

Katika watu waliokuwa wanajiamimi kwa kuwaikia migomo baadhi ya waajinga WA kiccm ni Pemba kwanza hawajali. Waulize waunguja 2005 na jeshi lenu lakini lilikuwa halina uwezo WA kutulazimisha migomo. Na tutaendeleza kuweka migomo Ikiwa hamjali haki za binadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiondoa pale bungeni ambapo kazi ya Naibu waziri ni kujibu maswali ya wabunge kwa niaba ya waziri husika......huku mtaani majukumu yao ni kama yanafanana.

Kama Naibu waziri anaweza" kumuagiza " IGP sidhani kama kuna tofauti kubwa ya majukumu yake na yale ya waziri, huu ni mfano tu.

Niishie hapo

Maendeleo hayana vyama!
 
Ukiambiwa kuwa RC wa Dar anauwezo wa kumuamuru waziri au IGP si ndiyo utachanganyikiwa zaidi
 
Kweli kabisa. Ila kule nadhani walifanya vile strategically kwa kumtumia mtu wa kulekule ili isije kuonekana kua wabara wanaleta fujo visiwani. Lile biti lingetolewa na mzee wa mwibara inge sound kivingine pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naibu Waziri wa mambo ya ndani Hamad Masauni amemwagiza IGP Sirro kuwavua vyeo RPC wa Kusini pemba Hassan Nasir Ally na RPC wa Kaskazini Pemba Shekhan Mohamed kwa kosa la kumwacha Jabali Maalim Seif kuhutubia wananchi wa Pemba , huku siasa za majukwaani zikiwa zimekatazwa
---
mm.png

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Hamad Masauni amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro kuwaondoa makamanda wawili wa polisi kisiwani Pemba kwa kushindwa kuzuia mikutano ya Mshauri wa chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad.

Masauni ametoa agizo hilo leo Alhamisi Desemba 12, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Unguja.

Amesema kwa muda mrefu kisiwa cha Pemba kimekuwa na matukio yasioridhisha jambo linaloashiria kuwa wameshindwa kazi.

Makamanda hao ni Hassan Nassir Ally wa Mkoa wa Kusini Pemba na Sheikhan Mohamed Sheikhan wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Akitoa mfano wa matukio hayo, Masauni amesema Maalim Seif anafanya mikutano kila kona huku ikijulikana kuwa imezuiwa.

Amesema sababu nyingine ni kutojengwa nyumba za polisi kisiwani humo licha ya Serikali kutoa maagizo.
View attachment 1289883
Ni juzi tu Katibu mkuu wa CCM alikuwa Pemba akifanya mkutano.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom