Maalim Seif atoa masharti ya kurejea CCM

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Nilishawahi kusema Muheshimiwa huyu anatafuta kuwa Rais wa ZNZ kwa nguvu zote!!!

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Bw. Seif Sharif Hamad amesema atarejea kwenye chama tawala cha CCM kama atapewa nafasi ya kuwa Makamu wa Rais na kuitishwa kwa uchaguzi ndani ya miezi mitatu na kuwa Rais wa Muungano.

Alisema kama CCM itakuwa tayari kufanya mambo hayo, yuko tayari wakati wowote kuanzia sasa kurejea kwenye chama hicho kwa vile atatekeleza ahadi aliyoitoa kwa wananchi ya kuwaletea maendeleo.

Bw. Hamad alikuwa akiongea na Nipashe katika mahojiano maalum, Makao Makuu ya CUF, Mtendeni Zanzibar, juu ya kumbukumbu ya Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Katibu Mkuu huyo wa CUF alisema hadi sasa hajui ni lini atajiuzulu siasa kwa vile bado hajawatekelezea ahadi wananchi ya kuwaletea mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi.

`Nitakuwa msaliti nikijiuzulu kabla ya kutekeleza ahadi niliyowapa wananchi. Ndio maana nasema sifahamu siku ya kujiuzulu siasa katika maisha yangu,` alisema.

Alisema kwamba katika maisha yake tukio atakalolikumbuka sana ni kufukuzwa uanachama ndani ya CCM baada ya kushutumiwa kuanzisha upinzani ndani ya chama na tukio la Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, kuvunja ushirikiano na Ujerumani Magharibi.

Alisema mgogoro na Ujerumani Magharibi ulisabishwa na Zanzibar baada ya kuanza ushirikiano wake na Ujerumani Mashariki, kitendo ambacho kiliwapa kinyogo Ujerumani Magharibi na kusitisha misaada ya kijeshi.

Akimzungumzia marehemu Baba wa Taifa, Bw. Hamad alitoa siri ya mazungumzo aliyoyafanya na marehemu Baba wa Taifa, kabla ya kifo chake.

Alisema aliwahi kuitwa na Baba wa Taifa kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, ambapo mazungumzo hayo aliweka siri kubwa.

Bw. Hamad alisema alipokea wito kutoka kwa Baba wa Taifa uliomtaka afike nyumbani kwake Msasani na kufanya mazungumzo naye siku chache kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa kwanza.

`Wito ule ulinishitua kadiri safari yangu ilivyokuwa ikiendelea kutoka Zanzibar hadi Dar es Salaam na baada ya kukutana naye nilipokea maneno mazito kutoka kwake,` alisema Bw. Hamad.

Alisema katika kikao hicho Mwalimu Nyerere alimueleza (Seif) kwamba ameanzisha chama katika mfumo wa vyama vingi, lakini akumbuke suala la kulinda umoja wa kitaifa na vyama vya siasa isiwe chanzo cha ugomvi miongoni mwa wananchi.

`Baba wa Taifa alinikumbusha umuhimu wa kufahamu rasilimali kubwa katika nchi yetu imegawika katika umoja wetu, tusijetukachukua hatua za kuathiri umoja`, alikariri maneno ya Mwalimu Nyerere katika mazungumzo hayo.

Alisema kwamba mazungumzo kati yake na Mwalimu Nyerere yalimpa wakati mgumu kwa vile watu mbali mbali walitaka kuyafahamu wakiwemo viongozi wa kimataifa, lakini aliheshimu umuhimu wa kuendelea kubakia mazungumzo hayo kuwa siri.

`Hapakuwa na ajenda yoyote ya kuhujumu viongozi, isipokuwa alisisitiza umuhimu wa kuzingatia umoja katika safari ya mageuzi,` alisema Bw. Hamad.


(Soma mahojiano kamili na Maalim Seif Nipashe ya Jumapili ambayo itakuwa na makala kemkem kuhusu maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa).

SOURCE: Nipashe
 
Haya kayazungumza wapi?

TCRA kaeni chonjo kuna mtu anataka kuingia mtegoni
 
Kamwe asiondoke CUF, sisi CHADEMA tutapata hasara, maana ndiye kiongozi pekee ndani ya CUF anayetuunga mkono CHADEMA.
 
Back
Top Bottom