Maalim Seif atembelewa na Dr. Shein: Tafsiri hizi picha

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,307
4,585
Concentrate na eye contact, pamoja na mikono

WEDNESDAY, MARCH 09, 2016




Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiambatana na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Ikulu na Utawalabora Mheshimiwa Dkt. Mwinyihaji Makame, amemtembelea kumjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanibar Maalim Seif Shariff Hamad ambaye yuko hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko baada ya kutolewa hospitali. Amesema afya yake inazidi kuimarika siku hadi siku. Dkt. Shein alifika hotelini hapo mnamo majira ya saa mbili usiku. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akimjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanibar Maalim Seif Shariff Hamad hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akimjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanibar Maalim Seif Shariff Hamad hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Picha na OMKR



CHANZO: MICHUZI BLOG WEDNESDAY, MARCH 09, 2016
 
SHEIN NA SEIF SHARIF HAMAD wala hawana ugomvi wowote.Kwanza wote wanatoka sehemu moja ambayo ni Pemba,pili wamesoma wote shule moja ni ma-school mate na tatu wote wamepewa uraisi na umakamu pamoja ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya zanzibar toka ipate uhuru kwa wapemba kushika uraisi na umakamu wa kwanza wa raisi Zanzibar.

Hawagombani hao na hawajawahi gombana maisha yao yote.

Usilolijua ni kama usiku wa giza.Washabiki kazi mnayo.Mtajijua.
 
Shein ni kama hajiamini. Hakuna direct eye contact. Hata alipomshika Seif kwa mikono miwili bado hakufanya direct eye contact. Ni ajabu. Sijui kuna nini.

Hiyo direct eye contact, wewe inakusaidia nini? Unawatafsiri watu kwa matukio ya picha! Unajua ni mambo mangapi wameongea? Hiyo direct eye contact una uhakika kwamba haikutokea?
 
Shein ni kama hajiamini. Hakuna direct eye contact. Hata alipomshika Seif kwa mikono miwili bado hakufanya direct eye contact. Ni ajabu. Sijui kuna nini.
Siku zote mtu mbaya kwako huwa anajishuku, mwoga hivi, anaona kama unamuona ndani ya moyo wako hivi.
 
Shein ni kama hajiamini. Hakuna direct eye contact. Hata alipomshika Seif kwa mikono miwili bado hakufanya direct eye contact. Ni ajabu. Sijui kuna nini.
mkuu hata Jana ilikuwa hivyohivyo sikuona direct eye contact bila Shaka wataalamu wa saikolojia wanajua maana yake
 
12801415_10204530587865037_2019982198199698893_n-jpg.328417





Wauza mitumba mnaotembeza nguo fursa hiyo !! Naomba mwende hoteli ya SERENA mkamuuzie Seif Shariff HAMAD shati na suruali kaishiwa.

Shati na suruali alizovaa jana ndio hizo hizo kavaa leo.ANGALIA PICHA ZA JANA NA LEO.
 
why kawekwa hotelini badala ya nyumbani kwake? siyo matumizi sahihi ya fedha za umma
Huyu angewekwa nyumbani asinge pumzika maana ndio rais wa anaependwa na alie chaguliwa...ingekua msururu wa watu....na Tunamlipia apumzike . Sawa sawa ?
 
Back
Top Bottom