Zanzibar 2020 Maalim Seif atangaza kugombea urais Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
1,973
2,000
Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Hamad ametangaza kugombea Urais Visiwani Zanzibar kupitia chama chake cha ACT-Wazalendo. Atachukua fomu ya kugombea urais Tarehe 4 mwezi Julai.

Amewaomba Wazanzibari kumkubali kama walivyofanya kwa chaguzi zilizopita kwa kuongeza idadi ya wanaompigia kura kila uchaguzi mpya tangu mwaka 1995.

Amesema walifanya tafiti kuona kama wazanzibar kama bado wanamkubali na tafiti hiyo ilionyesha kuwa bado anakubalika ndani ya Zanzibar

Amedai tafiti waliyofanya ilionyesha kuwa, kuna wazanzibari waliahidi kutopiga kura kama asipopewa turufu ya chama kugombea Urais Zanzibar

 

Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,571
2,000
Maalim kwa muda wa miaka yote kweli umeshindwa kumuandaa mtu mwingine kuchukua nafasi yako.

Miaka yote ni wewe tu,ina maana wazanzibar hawana mtu mwingine wa kumkubali hadi wakukubali wewe tu kuwa mgombea wao kwa miaka nenda rudi,jua siasa ni kama jeshi.

Kamanda mmoja akifeli mbinu anarudi nyuma na kuacha mwingine aje na mbinu mpya za kushinda vita,wewe umeshafeli achia wengine.
Hii ni ishara hata siku ukiipta hii nafasi hautoiacha

Toka enzi za Mkapa mgombea ni wewe tu,badilika sasa,waachie wengine.
 

mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
21,865
2,000
Mbona miaka yote maalim anashinda.

Tatizo jechalism
Maalim kwa muda wa miaka yote kweli umeshindwa kumuandaa mtu mwingine kuchukua nafasi yako,miaka yote ni wewe tu,ina maana wazanzibar hawana mtu mwingine wa kumkubali hadi wakukubali wewe tu kuwa mgombea wao kwa miaka nenda rudi,jua siasa ni kama jeshi, kamanda mmoja akifeli mbinu anarudi nyuma na kuacha mwingine aje na mbinu mpya za kushinda vita,wewe umeshafeli achia wengine.

Hii ni ishara hata siku ukiipta hii nafasi hautoiacha, toka enzi za Mkapa mgombea ni wewe tu,badilika sasa,waachie wengine.
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
5,817
2,000
Hahaha CCM eti hawamtaki mgombea kupitia ACT wazalendo , tena Zanzibar anawahusu nini nyie?!

CCM Zanzibar mnawatia nia 30, kwanini msijikite kwenye kumtafuta mgombea wenu, badala ya kuanza kulalamikia maamuzi ya Maalim Seif?!

Hajapitishwa kugombea na chama chake, naye kaweka nia kwa kuchukua form kuomba ridhaa ya kugombea nafasi hiyo.
Mlitaka vijana wa UVCC ndio wakachukue form ACT Wazalendo?!

Sijaona UVCC aliyechukua Form kuomba ridhaa iwe Tanganyika au Zanzibar, lakini mnasema eti maalim Seif ni kikongwe, kwani waliogchukua form Zanzibar kwa ticket ya ccm hamuwaoni kina JECHA?!

Hajawa mgombea yeye anatia nia kugombea.

Hii siyo ccm inayozuia watu kuchukua form jamani.
 

vposterior

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
635
1,000
Naona hofu imewatanda wana CCM, nyinyi tatizo lenu nini hasa? Si chama chenu kinakubalika mbona povu jingi. Maalim Seif ni mwiba kwa siasa za Zanzibar na mara hii sijui mutatumia mbinu gani kupora Uraisi kule Zanzibar. Vijana wamejipanga vizuri ENOUGH IS ENOUGH.
 

Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
7,365
2,000
Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Hamad ametangaza kugombea Urais Visiwani Zanzibar kupitia chama chake cha ACT-Wazalendo. Atachukua fomu ya kugombea urais Tarehe 4 mwezi Julai

Amewaomba wazanzibari kumkubali kama walivyofanya kwa chaguzi zilizopita kwa kuongeza idadi ya wanaompigia kura kila uchaguzi mpya tangu mwaka 1995

Amesema walifanya tafiti kuona kama wazanzibar kama bado wanamkubali na tafiti hiyo ilionyesha kuwa bado anakubalika ndani ya Zanzibar

Amedai tafiti waliyofanya ilionyesha kuwa, kuna wazanzibari waliahidi kutopiga kura kama asipopewa turufu ya chama kugombea urais Zanzibar

Mh. Seif asipoteze muda, kamwe hatokuja kuwa rais wa Zanzibar ktk maisha yake! Awaachie wengine wagombee, yaani yeye kagombea sasa ni zaidi ya miongo kazaa, aache tamaa, anapoteza muda kabisa.
 

Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
7,365
2,000
Kama anashinda na hatangazwi, kilichobadilika ni kitu gani?
Muuza nchi na msaliti, muongo muongo na mchonganishi wa muungano nani amtangaze kuwa rais?? Hizo kura za kumtangaza kuwa mshindi zitatoka wapi???? Mtu ambaye amekuwa brainwashed na kazi yake ni kubrain wash wazanzibar apewe nchi??? Kwa ufupi Mh. Seif hawezi na haitakuja kutokea kura kutosha maana wazanzibar hawamtaki kabisa kabisa, tena safari hii atapata kura kiduchu zaidi ya za last time. Awaachie vijana wagombee
 

aloycious

JF-Expert Member
Dec 17, 2012
5,722
2,000
Watakuza ruzuku ACT na ulaji utatoka CUF kuja ACT kwa kina Zitto. Siasa ni ulaji.
Fikiria mnapata 200M kila mwezi mnakula hazina kodi ni kuzingia tuu shughuli za uongo na kweli.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom