Maalim Seif arejea Zanzibar

1974hrs

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
741
536


Siku chache baada ya Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein kuapishwa baada ya kushinda uchaguzi wa marudio uliosusiwa na baadhi ya vyama vya upinzani, Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amerejea Zanzibar.


Maalim Seif ambaye alikuwa mapumzikoni katika hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es Salaam kwa takribani siku 17, jana alirejea Zanzibar kuendelea na mapumziko yake, Maalim Seif alilazwa katika Hospitali ya Hindu Mandal ya jijini Dar es Salaam,mara baada ya kuruhusiwa March 8 mwaka huu alishauriwa na Daktari wake kupata mapumziko ya muda mrefu.

Kurejea kwa Maalim Seif visiwani humo kunazidisha shauku na kiu ya baadhi ya Wazanzibar kutaka kusikia atakachokisema kiongozi huyo wa upinzani mwenye ushawishi mkubwa kwenye jamii.


Maalim Seif aliugua wakati Wazanzibar wakiwa katika maandalizi ya kurudia uchaguzi mkuu uliofanyika March 20, mwaka huu baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar( ZEC), Jecha Salim Jecha kwa madai kuwa uligubikwa na dosari nyingi.


Gharama za Hotelini

Taarifa zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari siku chache zilizopita zilidai kuwa kila siku aliyokaa kwenye hoteli hiyo, Maalim Seif alikuwa akitumia wastani wa Sh. 6,162,500, Kutokana na takwimu hizo, hadi kufikia jana, Maalim Seif atakuwa ametumia kiasi kisichopungua sh. Milioni 92.4
 
Bado hatujakata tamaa,tunajipanga kwa 2020.
Kama Mandela aliweza kuingia madarakani akiwa Mzee Lowassa na Maalim Seif watashindwa vipi?
Just a matter of time.
 
kama anashindwa kuandaa strategies za kudai ushindi wake anajifungia tuu hotelini nae hafai, anatakiwa ahamasishe wazanzibar wapambane kudai haki yao!

Ameiga style ya kina Mbowe baada ya Mkwala wa kwenye Conference kudai wameibiwa kura huendelea na shughuli zao za uzalishaji Mali.
 
Amerudi na Jussa..... Kuna jambo nililisikia kati ya Seif na Jusa kuwa wana uhusiano wa kiCameroon.
 
MLIWACHAGUA LAKINI KWA BAHATI MBAYA HAMKUWA WENGI...MIKWARA YA STILL PICTURES NA VIDEO ZA GUINEA BISSAU HAZICHAGUI RAIS
Ukawa hatukupambana na maccm ila tulipambana na dola, Na ukweli utabaki kuwa ukweli kwamba seif na Lowasa ndo warais tuliyowachagua watanzania zaid ya 62% kwa bara,
 
Walitegemea angekuwa mkimbizi kama DR. Slaa kurudi kwake lazima wapate kihoro, mwenye nchi karudi sijui wata jificha wapi.
 
Back
Top Bottom