Maalim Seif aomba kuzungumza na Rais Magufuli

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899



Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Zanzibar Maalim Seif, amemuomba Rais Dk. John Magufuli wakutane na wazungumze kwa lengo la kumaliza mgogoro wa Zanzibar na kudumisha Muungano.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Kipindi cha TUJADILIANE cha Union Tanzania Press Club (UTPC) jijini Mwanza, ambapo ameeleza utendaji kazi wa Mahakama za Zanzibar zinafuata amri ya viongozi wa serikali.

"Kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini ZEC kutangaza kurudia Uchaguzi wakati mshindi anajulikana ni kinyume cha taratibu na sheria hata katiba ya nchi yetu hairuhusu, mimi na wenzangu tulipata kazi ngumu kuhamasisha vijana waliokuwa wanataka kuingia barabarani waachane na vitendo hivyo," alifafanua.

Aidha amesema kuwa chama cha CUF Zanzibar wanashiriki uchaguzi kwa ajili ya mapambano kwani ndio chama kikuu cha upinzani Zanzibar, kwani waungwana na waombapo mazungumzo wapewe nafasi ili kujenga muungano wenye maendeleo kwa Taifa la Tanzania.
 
tuliwashauri sana msimamishe wagombea uchaguz wa marudio..leo hii kwishaa..seif amgekuwa makamu wa pili lipumbafu lisingemsumbua
Seif alipokea ushauri wa kinafiki kutoka chama fulani cha upinzani TZ Bara kuwa asishiriki uchaguzi wa marudio. Kumbe waliomshauri waliona kuwa hata akishindwa kwenye marudio angekuwa serikalini na hivyo kuwa na nguvu kuliko wao. Seif asisahau kuwa CUF ndio walioshinikiza kuweka kwenye katiba ya Zanzibar kuwa maamuzi ya tume yao ya Uchaguzi ni finality hayataingiliwa na mtu wala chombo wala taasisi yoyote nje au ndani ya Zanzibar. Cha ajabu wakamtaka Magufuli aingilie bila kutaja kifungu cha katiba wala sheria kinachomruhusu kuingilia. Seif kaingizwa town asubiri 2020 agombee tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akina Mtatiro walimtukana sana Prof Lipumba Kwa kuitikia wito wa Rais kwenda Ikulu , Leo Bosi wake hajaalikwa lakin tayari anaomba mualiko!

Unakataa kumpa Mkono Mpemba Na Mzanzibar Mwenzako mnaeweza kukutana Kama ndugu Na kuzungumza kindugu unakuja kuomba mualiko Kwa Msukuma mliejuana ukubwani
 
Kuwa Rais wa Z'bar kwa Seif haiwezekani tena, labda Magu akimuhurumia ampe ukuu wa mkoa huku bara au ubalozi... Mazungumzo ni kitu kizuri. Kama mh Rais ana muda amkubalie wakutane...
 
Kuwa Rais wa Z'bar kwa Seif haiwezekani tena, labda Magu akimuhurumia ampe ukuu wa mkoa huku bara au ubalozi... Mazungumzo ni kitu kizuri. Kama mh Rais ana muda amkubalie wakutane...


Tangu Magu alivyomshauri Shein 'amfungie' vioo hata Safar za kuja kulala Serena Hotel ziliisha wala check up za Ulaya hazifanyiki Tena , akiumwa tunakutana nae Hindumandal

Adui yako muombee njaa inamtosha Sio maradhi
 
Toka lini CuF Na chadema Wanataka muungano? To hell with them.Chadema puppets wa wakoloni wajerumani CuF puppets wa waarabu masultani wa Zanzibar CCM hatuwezi ongea Na local puppets wa waarabu wa Oman waliobeba waswahili watanganyika biashara ya utumwa Na wajerumani waliotukoloni ambalo Chadema ndio local mawakala wao
 
Kama hadithi ya aliyemuomba nyani wakazungumze kuhusu ugomvi wake na ngedere..... hahaha.
 
Toka lini CuF Na chadema Wanataka muungano? To hell with them.Chadema puppets wa wakoloni wajerumani CuF puppets wa waarabu masultani wa Zanzibar CCM hatuwezi ongea Na local puppets wa waarabu wa Oman waliobeba waswahili watanganyika biashara ya utumwa Na wajerumani waliotukoloni ambalo Chadema ndio local mawakala wao
Babu zako watumwa wapo marekani,akina ben carson
 
Back
Top Bottom