Maalim Seif anakagua miradi ya maendeleo Tz bara kama nani?

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Je halali kwa kiongozi ambaye hatukumchagua kwa kura zetu, wala hana mamlaka yeyote ya kutuongoza kikatiba, kuja kufungua na kukagua miradi ya serikali huku Tz bara? Kwa mujibu wa chanel ten leo, seif ameonekana akifungua madarasa, kukagua mirad na kuhutubia wananchi!

Mkuu hilo swali kwa kweli linahitaji mjadala wa kitaifa,na hapa ndipo unapona katiba yetu na muungano wa picha za wazee wetu unamapungufu makubwa sana.Sijui msafara wake unahudumia na fedha za upande upi wa nchi,kama ni bara ni chini ya wizara gani?na bajeti hiyo ilipitishwa na bunge lipi?je yupo kiserikali au kichama?maswali ni mengi mno.

Je halali kwa kiongozi ambaye hatukumchagua kwa kura zetu, wala hana mamlaka yeyote ya kutuongoza kikatiba, kuja kufungua na kukagua miradi ya serikali huku Tz bara? Kwa mujibu wa chanel ten leo, seif ameonekana akifungua madarasa, kukagua mirad na kuhutubia wananchi!

Hapa kuna maswali mengi na labda wataalamu wa katiba watatusaidia.

Hivi mkuu wa mkoa wa Tanga, Meja mstaafu Said Kalembo anaweza kufanya ziara ya kiserikali huko Unguja au Pemba???

wewe mjipya elewa kuwa kiongozi wa nje kufungua mradi ni ile ambayo wamegharamia. Kwa hiyo huyo seif hana haki kufungua miradi bara, waishie huko huko zenj na serikali zao za mseto. Huku bara hakuna mseto ingawa serikali ya bara iko likizo.

seif anaweza kuja bara na kufungua miradi ya maendeleo kwa kuwa hii ni serikali ya muungano ambapo zanzibar ni sehemu ya muungano, acha Jazba na ubaguzi, cdm mmelikoroga mtalinywa.

wana ndoa wenzao CCM wameamua kuwapa shavu na kuwajenga kisiasa zaidi huku bara ambako wameanza kupoteza umaarufu

rais wa china alipokuja kufungua uwanja wa taifa alifungua kama nani?
Hilary clinton alipotembelea kukagua symbon power na kule kibaha alitembea kukagua kama nani?
Usiwe unaleta mada mfu wewe au ulitaka nawewe uonekane umeanzisha thread?

seif anaweza kuja bara na kufungua miradi ya maendeleo kwa kuwa hii ni serikali ya muungano ambapo zanzibar ni sehemu ya muungano, acha Jazba na ubaguzi, cdm mmelikoroga mtalinywa.

Katika serikali ya Muungano Seif ana madaraka gani kikatiba????

more to come
CUF wana nafasi kubwa ya kuwa ccm A very soon na CUF kufa

..kwa kuwa hii ni serikali ya muungano ambapo zanzibar ni sehemu ya muungano, acha Jazba na ubaguzi
"Hii ni serikali ya Muungano,"

Hii ipi ? Seif Hamad yupo serikali ipi?

Unaongelea ubaguzi? Ubaguzi ni pale Mtanzania bara anapokataliwa na sheria kumiliki real estate ndani ya Zanzibar.

rais wa china alipokuja kufungua uwanja wa taifa alifungua kama nani?

Hilary clinton alipotembelea kukagua symbon power na kule kibaha alitembea kukagua kama nani?
uyo rais wa china na hilary clinton walikuja kuzindua miradi waliyofathili apa nchini kwa mfano uwanja wa Taifa weye siuliona wachina walivyojitolea pale,usiwe km jk anaye ongwa suti london.
Usiwe unaleta mada mfu wewe au ulitaka nawewe uonekane umeanzisha thread?

rais wa china alipokuja kufungua uwanja wa taifa alifungua kama nani?

Hilary clinton alipotembelea kukagua symbon power na kule kibaha alitembea kukagua kama nani?

Usiwe unaleta mada mfu wewe au ulitaka nawewe uonekane umeanzisha thread?

Mkuu! Kwa upeo wangu wa Kiendabure nakumbuka uwanja wa taifa umejengwa na wachina ni sawa kwa Rais wa China kuja kufungua. Bi Clinton alitembelea Symbion ni ya USA. Pia huko Kibaha alitembelea miradi inayofadhiliwa na USA. Maalim Seif bado anapwaya ktk hili la kufungua miradi ya Bara.

Back
Top Bottom