Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 674
Maalim Seif amsifu Rais Karume kwa mafanikio
Habari Zinazoshabihiana
Na Ali Suleiman, Zanzibar
KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, amesema suluhisho la matatizo ya Zanzibar ni wananchi kumaliza tofauti zao na kuweka pembeni chuki na uhasama.
Maalim Seif alisema hayo juzi katika ukumbi wa Baraza la Idd katika Jamat-Khan mjini hapa, alipozungumza na wananchi na wafuasi wa chama hicho.
"Wazanzibari kama kweli tunahitaji umoja na utulivu, basi kwanza tunatakiwa kuondosha tofauti za kisiasa...chuki na uhasama, zisipewe nafasi kutawala nyoyo zetu," alisema Maalim Seif.
Alisema yamekuwapo mafanikio makubwa katika kipindi cha Serikali ya Rais Amani Abeid Karume, ambapo wafadhili wamerudisha misaada yao na hiyo yote ni matokeo ya kuwapo mshikamano.
Alisema wapo watu hawataki kubadilika na wanaamini, kwamba chuki na fitina ndiyo njia pekee ya kufanikiwa na kutekeleza matakwa yao.
Maalim, Seif alieleza kufurahishwa kwake na kuwapo chakula katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, hali ambayo inaonekana wazi wakulima kujitahidi katika kilimo.
Alisifu wakulima wa kisiwa cha Pemba kwa kuzalisha chakula kwa wingi na ziada yake kutumika Unguja na mikoa mengine ya Tanzania Bara.
"Wakulima katika kisiwa cha Unguja, wanatakiwa kuimarisha shughuli za kilimo ili kufikia malengo ya kujitosheleza kwa chakula, kama ilivyo kwa upande wa Pemba," alisema Maalim Seif.
Katika Mwezi wa Ramadhan, chakula zikiwamo ndizi na muhogo, kilifurika kwa wingi Unguja kutoka Pemba.
source majira