Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 129
Maalim Seif amkejeli Yusuf Makamba
Na Salma Said, Zanzibar
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amesema anajisifia nafasi yake ya ukatibu mkuu katika chama chake kutokana na kuheshimiwa maamuzi yake tofauti na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba, ambaye hana maamuzi katika chama chake.
Seif aliitoa kauli hiyo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Demokrasia Mkoa wa Mjini Magharibi alipokuwa akiwahutubia wanachama na wapenzi wa CUF baada ya maandamano makubwa ya kupinga maamuzi yaliotolewa na CCM kuhusiana na mazungumzo ya muafaka Visiwani Zanzibar baina ya vyama vyao.
"Mimi najisifu kuwa kweli ni katibu mkuu, ninaposema ninasikilizwa na maamuzi yangu yanaheshimiwa na viongozi wote lakini wewe Makamba kwa nini unakubali kuchezewa chezewa," alisema na kuongeza: "Ikiwa saini yako haina nguvu unaambiwa basi hata hicho cheo chako hakithaminiwi katika chama chako."
Kauli hiyo ya Maalim Seif ilikolezwa na bango lililokuwa limewekwa mbele ya mkutano likiwa limebeba ujumbe uliofanana na matamshi hayo ya katibu mkuu wa CUF kuhusu nafasi ya uu ya Katibu Mkuu wa CCM katika chama chake.
"Ikiwa Makamba wewe hujielewi ni nani basi Seif ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF)," alisema na kuongeza: "Kiongozi mzuri na mwenye upeo na mwenye kusikiliza na kusikilizwa na kuheshimiwa mawazo yake na yeye kuheshimu na wengine lakini sio kiongozi kudharauliwa na hata watu wa chini yake.
"Mimi hao kina Jussa, Hamad Rashid, wabunge na wengine ni wakubwa lakini wanaheshimu ninachozungumza. Inakuwaje wewe huheshimiwi?" alihoji Maalim Seif na kuwaambia
wanachama wake kwamba anakumbuka alipokuwa mwanachama wa CCM chini ya mwenyekiti wake, Mwalimu Julius Nyerere,
jinsi vikao vilivyoendeshwa na kuwa mwenyekiti alipotaka jambo hakuna aliyepinga.
Alisema leo hii ndani ya CCM kiongozi wake anapozungumza na kutoa maamuzi wanachama wanashindwa kuheshimu vikao na hakuna thamani ya kiongozi mkuu wa chama kama ilivyotokea kwa Rais jakaya Kikwete kuyumbishwa na vikao vyake.
"Nilikuwa CCM, najua mwenyekiti akitaka jambo, lakini leo Kikwete anayumbishwa na wahafidhina wachache eti kwa kisingizio cha kulinda Mapinduzi. Ni hoja za kibumbavu kabisa," alisema Maalim Seif.
Seif alisema viongozi wa Serikali ya Zanzibar wana hoja za kitoto za kwamba atakapoingia madarakani huenda akawafunika serikali nzima kutokana na rekodi yake ya utendaji kazi.
Source: Mwananchi
Makamba hajiamini sio kwamakusudi ila nikweli cheo chake ni kikubwa yaani hakiwezi. Huku nyuma watu walipiga sana kelel kuwa Makamba hauwezi ukatu mkuu wa CCM lakini tuliona jinsi alivyo wachekesha kina Kikwete mbele ya NEC wakati wakiteuliwa kina Msekwa. Kwa kuwa Mwenyekiti wao ni mtu wa kupenda kucheka cheka naona ndio maana amemweka mchekeshaji mhe mgosi wa ndima Yusuph Makamba. Hawa watu wanafanya hivi kwakuwa hapo serious na masuala ya nchi. Kucheka na vichekesho ni moja ya sanaa na wao ni wasanii. Mpo hapo wanaCUF?