Maalim Seif amkaribisha Bernard Membe ACT-Wazalendo huku akimuonya kuwa asiwe na masharti

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mshauri mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amemkaribisha katika chama hicho aliyekuwa mwanachama wa CCM, Bernard Membe lakini akimuonya asiwe na masharti.

Maalim amtoa kauli hiyo siku chache baada ya Membe katika mahojiano na Mwananchi kudai kuwa alifukuzwa CCM kutokana na nia yake ya kutaka kupambana na mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Membe na makatibu wakuu wawili wastaafu, Abdulrahman Kinana na Yusufu Makamba walifikishwa mbele ya kamati ndogo ya udhibiti na nidhamu kujibu mashtaka ya kinidhamu.

Makada hao waliingia matatani baada ya sauti zao pamoja na za wanachama wengine watatu, kusambaa katika mitandao ya kijamii ikizungumzia kuporomoka kwa umaarufu wa chama hicho na uenyekiti wa Magufuli.

Makamba alisamehewa makosa yake wakati Kinana atakuwa chini ya matazamio kwa miezi 18, kipindi ambacho hataruhusiwa kugombea uongozi, wakati Membe amevuliwa uanachama na hivyo hataweza kutimiza ndoto yake ndani ya chama hicho.

Alipoulizwa na timu ya wahariri wa Mwananchi kuhusu Membe kujiunga ACT, Maalim Seif ambaye alifukuzwa CCM mwaka 1988, amemkaribisha Membe huku akisema yeye hawezi kurudi chama tawala.

“Ya ndugu yangu Membe sisi chama chetu kitampokea yoyote atakayekuja mradi asije na masharti,” amesema Maalim Seif.

Alipoulizwa kuhusu kuomba msamaha ili arejee CCM, Maalim Seif angeweza kuomba msamaha tangu wakati wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa Mwenyekiti wa CCM.

“Wakati huo kulikuwa na mawazo hayo kwamba tumewaonea hawa vijana tumewafukuza, kwamba wakiomba radhi tutawarejesha. Mimi nikasema sijasahau kitu CCM nirudi kutafuta nini? Kwanza watuondoe, kwamba nitarudi CCM No, never. Sitorudi CCM,” amesema.
 
Leo tarehe 04/03/2020 Maalim Seif Sharif Hamad ambaye ni Mshauri Mkuu wa ACT-Wazalendo amemkaribisha Membe kujiunga na chama chao akisema kinachotakiwa ni Membe kutokuwa na masharti yoyote. Maalim ameyasema hayo alipokuwa anaongea na jopo la Wahariri wa MCL.

MCL wameweka ujumbe huo katika akaunti yao ya Twitter yenye jina Mwananchi Newspapwers (@MwananchiNews) ambapo Zitto Kabwe ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Chama hicho ame-retweet ujumbe huo hali inayoashiria kuwa Maalim amefikisha ujumbe ambao kimsingi ndio msimamo wa chama. Kinachoandaliwa hapa ni namna ya kumpokea Membe ndani ya chama hicho na pengine ACT-Wazalendo nao wakabadili gia angani kama ilivyokuwa kwa CDM mwaka 2015. Yajayo yanafurahisha.
 
Hii kitu hii imepangwa...... Haingii akili Jasusi mbobezi apelekwe pelekwe....

Huu Ni mkakati wa kuiua CDM....kuipa nguvu kidogo cuf,nccr na act......

Ila Ila Ila ...................
Sasa mku wewe ulitaka kama Membe amefukuzwa ccm asiende kwenye chama chochote akae tu nyumbani? Wanasiasa wana ndoto zao za mbali acha usiwabanebane maisha yao ni kutokana na karata za siasa. Angeomba kwenda Chadema watasema Lowasa alituacha nawewe usije.
 
Naona kosa lililofanywa mwaka 2015 linataka kuhirudia ..chonde chonde msirudie makosa ACT
Believe me Membe hawezi kwendana na Chadema walishapokea mawazili wakuu 2 na wote walisharudi CCM acha aende ACT labda atafaulu kupitia huko.
 
Hivi vyama acha tu. Yaani Maalimu anaongea kama mtu ambaye tayari ana mamlaka sio "mshauri wa chama". Maana yake anatuma ujumbe kwa wanaogombea nae uenyekiti kuwa ni wasindikizaji tu😃😃
 
Back
Top Bottom