Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,499
- 9,279
Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, ameeleza kuanzishwa kwa mfumo mpya wa ajira ikiwa ni hatua za kutibu ubaguzi wa ajira visiwani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).
Amekiri kuwepo kwa ubaguzi wa ajira kwa baadhi ya Wazanzibari, unaotokana na misingi ya tofauti za kisiasa na kwamba, tatizo hilo linakwenda kupatiwa ufumbuzi.
“… kulikuwa na changamoto katika taasisi za kiserikali katika kuajiri, sasa serikali itaanzisha mfumo rasmi wa kimtandao kwa kuomba ajira na sio kama zamani,” amesema Maalim Seif wakati wa ziara yake kisiwani Pemba jana Jumatano tarehe 6 Januari 2021.
Kwenye ziara hiyo, Maalim Seif amesema, wananchi hususan vijana, wanatarajiwa kunufaika na uwekezaji ambao uko njia kufanyika katika uvuvi.
“Kuna uwekezaji unaotarajiwa kufanyika katika sekta ya samaki, uwekezaji huu utawanufaisha hususani vijana,” amesema.
Maalim Seif ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, anaendelea na ziara yake Pemba akikutana na viongozi mbalimbali wa serikali, chama chake na wakuu wa taasisi.