Maalim Seif Aja na Mapya Z'bar

Cardinal06

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
963
326
Dar/Zanzibar. Siku moja baada ya Jeshi la Polisi kusema limemwita katibu mkuu wa CUF ijumaa kwa ajili ya kumhoji kuhusu masuala ambayo hayakuwekwa wazi, wanasiasa nchini wamekuja juu wakisema hatua hiyo inaashiria ukandamizaji wa kisiasa, huku chama hicho kikisema kinasubiri tukio hilo ili kitoe msimamo.

Wakati wanasiasa wengi waliozungumza na Mwananchi wakipinga kitendo hicho kwa maelezo kuwa hakitasaidia kutafuta suluhu ya kisiasa Zanzibar, Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa ameshauri wanasiasa kuiga utulivu wa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa licha ya kufanyiwa vitimbi.

Juzi, Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Hamdani Makame alisema, Maalim Seif Sharif Hamad ameitwa kuhojiwa huku Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msangi akisema kuna mambo mengi ambayo ofisi yake inahitaji kuyafahamu kutoka kwa mwanasiasa huyo ambaye alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kabla ya Uchaguzi Mkuu uliopita.

Lakini wanasiasa wanaona kitendo hicho hakifai. “Hawa watu wameingia katika njia ya ukandamizaji,” alisema Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki. “Wameiba kura wakati wa uchaguzi, sasa wanatumia mabavu kuwanyamazisha wote wanaodai haki.”

Msemaji huyo mkuu wa kambi ya upinzani bungeni alisema Serikali ya CCM inapaswa kujifunza kutokana na makosa na akasisitiza kuwa kumkamata mwanasiasa na kumpeleka Mahakamani si suluhisho, bali ni kuongeza uhasama na ugomvi.

“Maalim Seif aliwahi kuwekwa kizuizini kwa amri ya Mwalimu Nyerere (Rais wa Serikali ya Awamu ya Kwanza) mwaka 1987 hadi 1991, lakini hiyo haikusaidia chochote. Maalim aliwahi kufunguliwa kesi ya uhaini lakini haikusaidia chochote,” alisema Lissu.

“Yaani huo uamuzi wa polisi kumhoji Maalim unaonyesha kuwa hawa watu hawajifunzi kutokana na historia ya nchi yetu.”

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, JamesMbatia alikosoa njia ambayo polisi wametumia. Alisema badala ya kumuita kituo cha polisi, walitakiwa kuomba kukutana naye na kumfuata popote alipo na kuomba maelezo yake.

Alisema kitendo cha kumwita polisi na hali ya sasa ya Zanzibar ni kuchochea uhasama kati ya wananchi na Serikali.
Mbatia, ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, alimshauri Rais John Magufuli, ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, awatake polisi kusitisha mpango huo.

Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya alisema: “Tunaisubiri siku ya Ijumaa kwa hamu. Tutajua hatua ya kuchukuakama chama baada ya kuona hatua ambazo Maalim atachukuliwa.”

Kambaya alitaja makada wa CUF ambao alidai wamekamatwa na kuhojiwa na polisi kuwa ni Nassor Ahmed Mazrui, Mansoor Yussuf Himid na mwanamkakati wa Maalim Seif katika chaguzi zilizopita, Mohamed Sultan Mugheiry, maarufu kwa jina la Eddy Riyami.

Ismail Jusa Ladhu alisema sababu kubwa ni Uchaguzi Mkuu pamoja na ule uliofutwa, kauli ambayo iliungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho-Bara, Magdalena Sakaya.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF, Hamad Masoud Hamad alisema hatua hiyo ni njia mbadala ya kuwanyamazisha Wazanzibari ambao alidai kuwa wengi waliamua kumpa ridhaa Maalim Seif kuiongoza Zanzibar kwenye Uchaguzi Mkuu ambao matokeo yake yalifutwa.

Alisema katibu huyo mkuu wa CUF ni kiongozi aliyekubalika kwenye nyoyo za Wazanzibari wengi, hivyo hatua ya kujenga hofu na mazingira ya kumdhalilisha hayatawarudisha nyuma.

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Salim Abdalla Bimani alisema huu si wakati tena wa siasa za kutishana kwa kuitiana polisi kwa kuwa Wazanzibari wameshakuwa wanaelewa kila hatua na njia bora za kudai haki.

Mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya uchumi katika Chuo Kikuu cha Zanzibar, Habibu Ismail Rashid alisema: “Nahisi hii ni njia ya kutaka kumdhalilisha Maalim Seif ili atoke mioyoni kwa watu, lakini nawaambia hilo wasahau. Maalim Seif anapendwabwana!”

Viongozi wa upinzani, hasa kutoka CUF wamekuwa wakihojiwa na Jeshi la Polisi tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa marudio uliofanyika Machi 20.

Uchaguzi huo ulirudiwa baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa mbio za urais.

Alifuta matokeo hayo wakati ZEC ikiwa imeshatangaza matokeo ya majimbo 31, huku mengine tisa yaliyosalia yakiwa yameshahakikiwa.

Alisema sababu za kufuta matokeo hayo ni kukiukwa kwa sheria na kanuni za uchaguzi, lakini CUF ilipinga ikisema alichukua uamuzi huo peke yake na kususia kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio.[/COLOR][/SIZE]

Chanzo: Mwananchi
 
Hivi lisu anaijua historia ya nchi hii kweli?nyerere alikua madarakani 1987-1991?hiyo amri ya nyerere kumuweka seif kizuizin aliitio kama rais mstaafu au?

Wewe hujui kuwa alikuwa bado ni Mwenyekiti wa CCM wakati huo wa chama kushika hatamu? Alikuwa na nguvu mpaka alikuwa anamsema hadharani Rais aliyekuwepo wakati huo.

Sina hakika lakini sintoshangaa kama alihusika na hiyo korokoroni ya Maalim Seif
 
Ccm wamepora ushindi wa wazanzibàri sasa wanaongoza kwa kutumia vyombo vya dola, hiyo sio Serikali ya wazanzibari tena
 
Hii remix yako mbona haieleweki? Maalim Seif, Lowasa, Rungwe, Jusa, Lisu, Mbatia, who is who?
 
Nyerere alikuwa active sana wakati huo hata uchaguzi wa 1995 yeye ndie alieongoza maamuzi yote mazito umesahau??

Hivi lisu anaijua historia ya nchi hii kweli?nyerere alikua madarakani 1987-1991?hiyo amri ya nyerere kumuweka seif kizuizin aliitio kama rais mstaafu au?
 
Dar/Zanzibar. Siku moja baada ya Jeshi la Polisi kusema limemwita katibu mkuu wa CUF ijumaa kwa ajili ya kumhoji kuhusu masuala ambayo hayakuwekwa wazi, wanasiasa nchini wamekuja juu wakisema hatua hiyo inaashiria ukandam
Dar/Zanzibar. Siku moja baada ya Jeshi la Polisi kusema limemwita katibu mkuu wa CUF ijumaa kwa ajili ya kumhoji kuhusu masuala ambayo hayakuwekwa wazi, wanasiasa nchini wamekuja juu wakisema hatua hiyo inaashiria ukandamizaji wa kisiasa, huku chama hicho kikisema kinasubiri tukio hilo ili kitoe msimamo.

Wakati wanasiasa wengi waliozungumza na Mwananchi wakipinga kitendo hicho kwa maelezo kuwa hakitasaidia kutafuta suluhu ya kisiasa Zanzibar, Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa ameshauri wanasiasa kuiga utulivu wa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa licha ya kufanyiwa vitimbi.

Juzi, Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Hamdani Makame alisema, Maalim Seif Sharif Hamad ameitwa kuhojiwa huku Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msangi akisema kuna mambo mengi ambayo ofisi yake inahitaji kuyafahamu kutoka kwa mwanasiasa huyo ambaye alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kabla ya Uchaguzi Mkuu uliopita.

Lakini wanasiasa wanaona kitendo hicho hakifai. “Hawa watu wameingia katika njia ya ukandamizaji,” alisema Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki. “Wameiba kura wakati wa uchaguzi, sasa wanatumia mabavu kuwanyamazisha wote wanaodai haki.”

Msemaji huyo mkuu wa kambi ya upinzani bungeni alisema Serikali ya CCM inapaswa kujifunza kutokana na makosa na akasisitiza kuwa kumkamata mwanasiasa na kumpeleka Mahakamani si suluhisho, bali ni kuongeza uhasama na ugomvi.

“Maalim Seif aliwahi kuwekwa kizuizini kwa amri ya Mwalimu Nyerere (Rais wa Serikali ya Awamu ya Kwanza) mwaka 1987 hadi 1991, lakini hiyo haikusaidia chochote. Maalim aliwahi kufunguliwa kesi ya uhaini lakini haikusaidia chochote,” alisema Lissu.

“Yaani huo uamuzi wa polisi kumhoji Maalim unaonyesha kuwa hawa watu hawajifunzi kutokana na historia ya nchi yetu.”

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, JamesMbatia alikosoa njia ambayo polisi wametumia. Alisema badala ya kumuita kituo cha polisi, walitakiwa kuomba kukutana naye na kumfuata popote alipo na kuomba maelezo yake.

Alisema kitendo cha kumwita polisi na hali ya sasa ya Zanzibar ni kuchochea uhasama kati ya wananchi na Serikali.
Mbatia, ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, alimshauri Rais John Magufuli, ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, awatake polisi kusitisha mpango huo.

Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya alisema: “Tunaisubiri siku ya Ijumaa kwa hamu. Tutajua hatua ya kuchukuakama chama baada ya kuona hatua ambazo Maalim atachukuliwa.”

Kambaya alitaja makada wa CUF ambao alidai wamekamatwa na kuhojiwa na polisi kuwa ni Nassor Ahmed Mazrui, Mansoor Yussuf Himid na mwanamkakati wa Maalim Seif katika chaguzi zilizopita, Mohamed Sultan Mugheiry, maarufu kwa jina la Eddy Riyami.

Ismail Jusa Ladhu alisema sababu kubwa ni Uchaguzi Mkuu pamoja na ule uliofutwa, kauli ambayo iliungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho-Bara, Magdalena Sakaya.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF, Hamad Masoud Hamad alisema hatua hiyo ni njia mbadala ya kuwanyamazisha Wazanzibari ambao alidai kuwa wengi waliamua kumpa ridhaa Maalim Seif kuiongoza Zanzibar kwenye Uchaguzi Mkuu ambao matokeo yake yalifutwa.

Alisema katibu huyo mkuu wa CUF ni kiongozi aliyekubalika kwenye nyoyo za Wazanzibari wengi, hivyo hatua ya kujenga hofu na mazingira ya kumdhalilisha hayatawarudisha nyuma.

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Salim Abdalla Bimani alisema huu si wakati tena wa siasa za kutishana kwa kuitiana polisi kwa kuwa Wazanzibari wameshakuwa wanaelewa kila hatua na njia bora za kudai haki.

Mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya uchumi katika Chuo Kikuu cha Zanzibar, Habibu Ismail Rashid alisema: “Nahisi hii ni njia ya kutaka kumdhalilisha Maalim Seif ili atoke mioyoni kwa watu, lakini nawaambia hilo wasahau. Maalim Seif anapendwabwana!”

Viongozi wa upinzani, hasa kutoka CUF wamekuwa wakihojiwa na Jeshi la Polisi tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa marudio uliofanyika Machi 20.

Uchaguzi huo ulirudiwa baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa mbio za urais.

Alifuta matokeo hayo wakati ZEC ikiwa imeshatangaza matokeo ya majimbo 31, huku mengine tisa yaliyosalia yakiwa yameshahakikiwa.

Alisema sababu za kufuta matokeo hayo ni kukiukwa kwa sheria na kanuni za uchaguzi, lakini CUF ilipinga ikisema alichukua uamuzi huo peke yake na kususia kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio.

Chanzo: Mwananchi
Hivi kuna ubaya gani kwa Maalim Seif kuhojiwa Polisi? Kitu gani kinachomfanya awe juu ya sheria? Yeye ni raia kama wengine
izaji wa kisiasa, huku chama hicho kikisema kinasubiri tukio hilo ili kitoe msimamo.

kwa hyo hata Diamond alivyo active saiv anaweza kukuweka wewe kizuizini

Acha muitwage nyumbu tu maana hata ujinga mnatetea

kumuweka kizuizini mtu ni suala la kisheria halitegemei ushawishi wa mtu au uactive wa mtu acha kupotosha. hapo ni kwamba mnazimu wa kambi ya upinzani alichapia baaasi
 
Kisiasa Seif Mwenyewe anaitafuta hiyo kick ambayo hawa Polisi Hawaijui.

Yaani kama kuna mtego hivi polisi wanakaribia kunasa. Sipati picha hali ilivyo kule Zanzibar halafu umwite Maalim seif awemo ndani ya ofisi za Polisi eti anahojiwa hiyo tension yote itakuwaje?

Nawashauri Polisi watazame mbinu mbadala badala ya kufuata mihemko ya wanasiasa.

Kumbukeni ni juzi tu CUF ilisema wanazo taarifa za Polisi kusindikizwa na CCM ili iwachukulie hatua viongozi wa CUF.

Mimi nasema kama kuna kosa Polisi wafanye kazi yao Lakini watumie "Weledi"

Hali ya Zanzibar kumwita Maalim Seif Polisi unachochea uvunjifu wa amani usio wa lazima kwa sasa.
 
Nyerere alikuwa active sana wakati huo hata uchaguzi wa 1995 yeye ndie alieongoza maamuzi yote mazito umesahau??
Unataka kuhalalisha mkuu!si kweli!hakua na madaraka hayo!si kila anachosema lisu basi kichukuliwe kama katekisimu au msaafu!
 
Hitler hakukosea ule usemi wake....'.kuna watu wamezaliwa ili wafikiri kwa niaba ya wengine'....kizaz hiki hatutafakari mambo kwa undani.....tunasubiri nani kasema basi alichosema tunakichukulia kama msaafu au katekisimu vile!

Tundu lisu ajifunze historia ya nchi hii....asipoteshe kwa malengo yao kisiasa!
 
Bila tume huru ya uchaguzi hapa kila siku tutakuwa tukicheza ngoma ile ile ya waburudishaji walewale tuliowachoka.
 
kwa hyo hata Diamond alivyo active saiv anaweza kukuweka wewe kizuizini

Acha muitwage nyumbu tu maana hata ujinga mnatetea

kumuweka kizuizini mtu ni suala la kisheria halitegemei ushawishi wa mtu au uactive wa mtu acha kupotosha. hapo ni kwamba mnazimu wa kambi ya upinzani alichapia baaasi
Utaelewaje hilo wakati umri na elimu yako haikuruhusu?
Nyerere katika mambo yanayo husu siasa mpaka anakufa alikuwa ndio final say, tena kuhusu Zanzibar ndio usisene kabisa
 
Wawe makini sana na Seif kuliko kipindi chochote.. Kitendo cha kumuita na kumuhoji polisi kinaweza kusababisha damu kumwagika Zanzibar koz yule ni kipenzi cha wanzanzibar Cuf wakisema wahamasishe maandamano hakuna atayebaki salama
 
Sefu anatoa matamshi ya hovyo ili akamatwe apande kisiasa
Alisema hakuna uchaguzi,umefanyika
Alisema atapewa urais kama anapewa boksi la tende,mpaka leo kimya.

Kaona anakosa sapoti ya ndani na kimataifa,kaja na mpya,Shein hafiki 2020,hapo anajua lazima akwaruzane na dola arudi front page,ebo!kila siku magufuli tu?
 
Unataka kuhalalisha mkuu!si kweli!hakua na madaraka hayo!si kila anachosema lisu basi kichukuliwe kama katekisimu au msaafu!
Una umri gani wewe?? Nyerere ndio alikuwa anaamua mambo yote mazito! Hata kubadili na kukataa ushindi wa Seif ni yeye alianzisha! Ilikuwa hali tete akaruka kwenda Zbar na kubadili......

kumbe ni mtoto kiasi hicho! Lisu anachosema ndio kilitokea! Mwinyi hana ujanja huo! Maalim alikuwa na nguvu sana na JKN ndie aliemtengeneza Maalim hadi hapo alipo! Mtoto w Nyerere pamoja na Salim! Hawana usemi kwa JKN
 
Back
Top Bottom