Maalim Seif aiondoa familia yake Zanzibar

mshumbusi

JF-Expert Member
Oct 24, 2011
457
232
Mama-1.jpg

Pichani ni mkewe Seif Shariff Hamad, Bi Awena Sinani Masoud akiwa chumba cha VIP uwanja wa ndege na tiketi yake ya Oman Air, muda mfupi kabla ya kuondoka.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Shariff Hamad ameondosha familia yake katika Kisiwa cha Unguja na kuipeleka Muscat-Oman.

Familia hiyo ya Maalim Seif Shariff Hamad wameondoka jioni hii kwa kutumia ndege ya Shirika la ndege la Oman (Omar Air). Familia hiyo ya Maalim Seif wameondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport saa 5:50 jioni hii.

Haikuweza kufahamika mara moja sababu hasa za Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Shariff Hamad kuiondoa familia yake Zanzibar. Kwa sasa Makamu huyo wa Kwanza wa Rais yupo katika mapumziko katika Hoteli ya Kitalii ya Dar es Salaam Serena.

Chanzo: ZanzibarNews.net
 
Kazi ipo kama ni kweli...Zanzibar hakujatulia kwa kweli....nawaonea huruma Wazenji
 
MZenj yeyote MWENYE AKILI ATOKE huko sasa... Wasisubiri kimbunga. NImesoma leo kuwa waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akisema kuwa wazanzibari wanaoikimbia Inji yao yao SIYO WAKIMBIZI, bali wako kwenye ZIARA za MATEMBEZI. Bila shaka na Familia ya Seif IKO matembezini Dar. Sijawa na uhakika kama familia ya jecha bado iko Zanzibari ama walisha timkia Dubai kitambo...
 
Haya ndiyo masomo ya kuchukua sisi wananchi,kwamba wanasiasa hawaoni tabu kuleta fyoko fyoko kwa kuwa wanajua wakati wa kubomolewa ukifika watakuwa wameshahamisha familia zao na wao kukaa mbali na eneo la tukio,badala yake msala unabakia kwetu wananchi wanyonge tuliokuwa tunawashabikia.
 
Hivi wa zanzibar kukitokea hofu mbona wanakimbilia uarabuni?
Zanzibar ilitawaliwa na warabu wa Oman,bado kuna uhusiano wa wazanzibari na warabu wa Oman,uhusiano huo upo na utaendelea kuwepo,unatakiwe ujue kuwa warabu wa Oman walizaliana sana na wenyeji wa Zanzibar

Kwaufupi wazanzibari wakikimbilia arabuni wanakimbilia kwa dada,mama,mjomba,shangazi ,kaka zao ,nk, sio ajabu kwa mtu kupata shida na kukimbilia kwa yule wakaribu yake....
 
Huyu Maalim Seilf arudi kwao Zanzibar sasa wanachafua hali ya hewa halafu wanakimbia? viwanja vyote vya ndege vifungwe hamna mtu kutoka wala kuingia hadi uchanguzi utakapo malizika!
 
Viongozi wanakimbiza familia halafu wanaanzisha vurugu wakiwa ugenini hiyo sio sawa wangeshauriana wore wabaki zenji.
 
ohh!...my lost son,in 1964 you enter into Improper agreement that will saffocate you, and its tough to shift out! what remain for you is to follow instructions....
 
Zanzibar ilitawaliwa na warabu wa Oman,bado kuna uhusiano wa wazanzibari na warabu wa Oman,uhusiano huo upo na utaendelea kuwepo,unatakiwe ujue kuwa warabu wa Oman walizaliana sana na wenyeji wa Zanzibar

Kwaufupi wazanzibari wakikimbilia arabuni wanakimbilia kwa dada,mama,mjomba,shangazi ,kaka ,nk,,zao sio ajabu kwa mtu kupata shida na kukimbilia kwa yule wakaribu yake....

NI SAWA TUU, KIGOMA NDUGU WENGINE WAKO BURUNDI, BUKOBA NDUGU WAKO UGANDA/ RWANDA, TARIME WAKO KENYA, TANGA WAKO MOMBASA, MTWARA NDIYO USUSEME NCHUMBIJI WAKO TELE SASA AJABU YAKE NINI????????????
 
kwa hiyo amewaondoa halafu familia za wengine ndiyo waandamane .. kazi kweli kweli.. sasa si kapoteza kura hapo
 
watu wote wenye busara lazima waondoke Zanzibar kwa sasa nawashangaa wale wote wenye ndugu bara na bado wanaendelea kukaa Zanzibar wakati kila dalili zinapelekea umwajikaji wa damu, hivi wanashindwaje kuona dalili hizo wakati wanawaona asikari walivyojiandaa mitaani?
 
Mama-1.jpg

Pichani ni mkewe Seif Shariff Hamad, Bi Awena Sinani Masoud akiwa chumba cha VIP uwanja wa ndege na tiketi yake ya Oman Air, muda mfupi kabla ya kuondoka.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Shariff Hamad ameondosha familia yake katika Kisiwa cha Unguja na kuipeleka Muscat-Oman.

Familia hiyo ya Maalim Seif Shariff Hamad wameondoka jioni hii kwa kutumia ndege ya Shirika la ndege la Oman (Omar Air). Familia hiyo ya Maalim Seif wameondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport saa 5:50 jioni hii.

Haikuweza kufahamika mara moja sababu hasa za Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Shariff Hamad kuiondoa familia yake Zanzibar. Kwa sasa Makamu huyo wa Kwanza wa Rais yupo katika mapumziko katika Hoteli ya Kitalii ya Dar es Salaam Serena.

Chanzo: ZanzibarNews.net
Hawa ndio Viongozi wetu ambao wanajifanya wanatupenda sana lakini wako busy kuangalia maslahi ya Familia zao na ndugu zao kwanza.
saa hizi anakula bata hotelini
 
Back
Top Bottom