Maalim Seif: ACT-Wazalendo ipo na itaendelea kuwepo, ACT is here to stay!

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema Chama hicho kipo na kitaendelea kuwepo, akisisitiza "ACT is here to stay"

Amesema, "Nguvu za ACT-Wazalendo si silaha wala mabomu bali ni Umoja wa Wanachama wake na mshikamano ambapo upo katika Chama"

Vilevile, Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa, kwa ufahamu wake, yeye ana jukumu la kutekeleza ambayo yameamuliwa kwenye vikao vya kitaifa, na atasimamia katika hilo

Aidha, amezungumzia suala la baadhi ya Vijana katika Chama hicho kusema anataka king'ora tu. Amesema, vijana hao wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kulinda maamuzi ya Chama

1607605915539.png


1607606004360.png


1607606003540.png
 
Hiki chama sasa kimekuwa cha Kizanzibari. Wanatakiwa pia kuwaangalia wanachama wao wa upande wa Bara maana wao ndio waliowakaribisha.

Kuwapuuza na kusema kuwa hawana cha kuchangia kwa sababu wao sio Wazanzibari ndio mwanzo wa kurudia kule kule walikokuwa CUF. Viongozi wa ACT Wazalendo ni Maalim na Zitto. Wakisahau hilo, watagawana fito.

Amandla...
 
Hivi mwaka 2025 ACT Wazalendo itaweza kusimamisha mgombea urais Zanzibar kwa sifa hizi walizommwagia Rais wa sasa? Wakifanikiwa kuigeuza Zanzibar kuwa kama Mauritius chini ya uongozi wake kutakuwa na sababu gani ya kubadilisha uongozi?

Hata kama watashindwa, watawezaje kunyooshea kidole serikali kwa kutokufanikisha adhma yao wakati walikuwa sehemu ya hiyo serikali? Inaelekea ACT Wazalendo wamekubali kuwa siku zote, kwa msemo wa Fatma Karume, watakuwa wabeba shela na sio mabibi harusi.

Maalim anauliza, walipata faida gani waliposusia uchaguzi uliopita. Faida kubwa ilikuwa ni kutohusika na mapungufu yeyote yaliyotokea katika kipindi hicho. Mapungufu kama ukosefu wa ajira, huduma duni za mahospitalini, kushindwa kuigeuza Zanzibar kuwa Dubai n.k. Sasa hivi wanakuja na hadithi za Ali Nacha za kuigeuza kuwa Mauritius. Tusubiri 2025.

Amandla...
 
Lengo kubwa la Truth and Reconciliation Commissions ni kupata ukweli wa mambo mabaya yaliyotokea ili yasirudiwe tena. Lengo kuu sio kuwaadhibu wakosaji au kuwafidia waliokosewa. Cha muhimu zaidi ni wale waliowakosea wenzao kukiri hadharani walichokifanya, kuomba msamaha na kuahidi kuwa hawata rudia tena.

Maalim inaelekea anaamini kuwa kitu cha msingi ni watu kulipwa fidia bila jamii kutambua kuwa walikosewa.

Watu wengi wangefarijika zaidi kumsikia Rais wao akikiri kuwa watu waliumizwa na kuuawa bila sababu ya msingi na kuahidi kuwa matukio kama hayo hayatajitokeza tena wakati wa utawala. Angekiri wazi kuwa kuna watu walikuwa wanawabagua wenzao kutokana na tofauti za kisiasa, na kuwa atahakikisha kuwa ubaguzi huo hautakuwepo chini ya utawala.

Kauli za "tusifukue makaburi au yaliyopita si ndwele" kutoka pande zote mbili hazitii matumaini.

Ni miaka zaidi ya 56 toka Mapinduzi lakini watu hawajasahau machungu yake. Itakuwa haya ya mwezi uliopita?

Amandla...
 
Lengo kubwa la Truth and Reconciliation Commissions ni kupata ukweli wa mambo mabaya yaliyotokea ili yasirudiwe tena. Lengo kuu sio kuwaadhibu wakosaji au kuwafidia waliokosewa...
Umemaliza. Wapinzani kwa kuonyesha uroho wa madaraka wataendelea kuibiwa tu kitulizo kikuu ni kupewa vyeo kwa kisingizio Cha maridhiano. Mbaya zaidi ajenda zao hazitafanyiwa kazi
 
SUK bila major changes kwenye mfumo mzima wa uchaguzi na kwa ZEK ileile ni kwamba CCM wameshinda hii vita kiulaini sana. Ushindi wao utaendelea kwa miaka mingi ijayo

Mwaka 2025 Dr. Mwinyi atajichukulia/atapewa Nchi mapema asubuhi na atamkabidhi mwana CCM mwingine chaguo kutokea Chamwino mwaka 2030.

ACT/CUF kama kawaida wataambulia post isiyo na chochote ya first VP na Wizara 2-3 hivi baada ya kuzuga kususia kwa wiki 1-2. Vicious cycle will continue
 
Unawapa watu hamasa, wanakuamini, wanakufuata, wewe jamaa wakithubutu kukuua wataulizwa, hawakutoi uhai, wanakukamata tu kijanja, utaachiwa jioni, wanawapiga risasi viherehere wanaoimba jina lako. Wanaumizwa, Wanakufa. Baadae unaleta hadithi za "TUNALIPONYA TAIFA".
 
Mkuu beth , asante sana kwa hii.

Nimefarijika sana na uamuzi wa busara wa Maalim Seif kukubali yaishe na kujiunga na CCM ndani ya SUK kwasababu mimi ni miongoni mwa tulioshawishi hili

Na Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane!

Na

P
 
Unawapa watu hamasa, wanakuamini, wanakufuata, wewe jamaa wakithubutu kukuua wataulizwa, hawakutoi uhai, wanakukamata tu kijanja, utaachiwa jioni, wanawapiga risasi viherehere wanaoimba jina lako. Wanaumizwa, Wanakufa. Baadae unaleta hadithi za "TUNALIPONYA TAIFA".
Maalim kaleta ukhanithi
 
Back
Top Bottom