Uchaguzi 2020 Maalim Seif: ACT Wazalendo hatuna mpasuko lakini Membe anataka kuwaaminisha Watanzania hivyo. Adai Mzee wa Ubwabwa ni bora kuliko Mgombea wao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Habari wana jf, maalim seif ameongea na waandishi wa habari na kuzungumzia suala la Membe huku akimtolea maneno makali sana.

Nimeshindwa kushangaa, leo hii maalim seif unasema Membe katumwa? Mbona siku ya kumpitisha pale chamani kuwa mgombea uraisi ulimsifia sana? Membe unalo la kujifunza, pole sana

===

1603256716819.png


MGOMBEA urais wa chama cha ACT Wazalendo visiwani Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, ameeleza kusikitishwa kwake na tamko la jana la mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Bernard Membe, kuwa yeye ni mgombea halali wa urais, hivyo ataipeperusha bendera ya chama na ana uhakika atashinda.

Akifafanua Kuhusu suala hili, Maalim Seif amesema “Nasikitika sana kwa aliyoyazungumza Membe jana. ACT-Wazalendo kupitia mkutano mkuu wa Taifa tuliamua tunataka mabadiliko katika nchi yetu. Mkutano mkuu ukabariki tushirikiane na vyama makini kuiondoa CCM madarakani. Membe alipokuja tulimwambia uamuzi wa mkutano mkuu ni tushirikiane na vyama vingine. Tukamuuliza tukiamua kushirikiana utakubali, akasema “Naam.” Tulipoona kampeni zetu zimesuasua, tukaamua, na Membe akiwepo, tumuunge mkono Tundu Lissu.”

Ameongeza kuwa, “Mgombea wetu Bernard Membe haonekani. Ni afadhali mzee wa ubwabwa Hashim Rungwe anaonekana. Kamati ya uongozi kwa kauli moja pamoja na Membe tulikubaliana tumuunge mkono Tundu Lissu. Sio kwamba hatumpendi Membe. Mimi nam-challenge, afanye hizo kampeni zake tuone hizo kampeni ziko wapi. Nia yake ni kutaka kuwachanganya Watanzania.”

Kuhusu kuwapo kwa mpasuko ndani ya Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif amesisitiza kuwa “Hakuna mpasuko ndani ya ACT-Wazalendo. Membe anataka iaminike hivyo, lakini hakuna. Chama kimefanya uamuzi, wewe unaenda kinyume. Tukuelewe vipi? Si umeletwa ACT kwa mission (shughuli) maalum.”

PIA SOMA
= > Uchaguzi 2020 - Bernard Membe: Watanzania mkae macho na mkae chonjo. Nafunga bao la Ushindi dakika ya 89 kwenye Uchaguzi huu 2020
 
Fedha za Kampeni za Membe zimedhibitiwa Airport akitokea Dubai na wasaidizi wake wamekamatwa!

Sasa hizo kampeni atafanyaje peke yake bila ya sapoti ya secretariet ya ACT?

Lipumba mara zote za uchaguzi alikuwa anasimama kwa miguu yake na wajanja wenzie wa mjini, pesa zote za kampeni mnapeleka Znz kunajisi Mapinduzi mnataks Jasusi afanyaeje?
 
Mwenyekiti wa Act taifa anaongea na wanahabari jijini dar es salam

--

Nimesikitika sana kwa aliyoyazungumza ndugu yangu Bernard Membe, ACT-Wazalendo kupitia mkutano mkuu wa Taifa ulisema tunataka mabadiliko, mkutano mkuu ukatoa mamlaka kwa uongozi ili kuhakikisha tunashirikiana na vyama vya wenzetu ambavyo ni makini

Membe alipokuja kwenye chama chetu, tulimwambia lengo letu ni kushirikiana na vyama makini na tulimwambia uko tayari akajibu yupo tayari. Mgombea wetu Bernard Membe haonekani. Ni afadhali mzee wa ubwabwa (Hashim Rungwe) anaonekana. Kamati ya uongozi kwa kauli moja pamoja na Membe tulikubaliana tumuunge mkono Tundu Lissu.

Sio kwamba hatumpendi Membe. Mimi ‘nam-challenge’ afanye hizo kampeni zake tuone hizo kampeni ziko wapi. Nia yake ni kutaka kuwachanganya Watanzania.

Alilosema Zitto si lake! Nililosema mimi Seif Sharif Hamad si langu! Bali ni maamuzi ya Chama. Ni msimamo wa ACT Wazalendo anayekaribia kumshinda Magufuli ni Tundu Lissu na huyo ndiyo tunamsapoti"

Zimebaki siku sana kwa wananchi kufanya maamuzi ya kuwachagua viongozi wanaowataka wao. Tunaelekea katika Uchaguzi Mkuu wakati wagombea wetu kadhaa wameenguliwa katika kinyang’anyiro hicho lakini tukafanye maamuzi

Nyakati zote mimi nilikua nawazuia watu wasiingie Barabarani! Sasa mwaka huu simzuii mtu. Yoyote atakayeamua kufanya lolote Afanye hiyo Tarehe 27 na 28. Wazanzibar wamepanga kulinda Demokrasia kwa gharama yoyote! Wamevuta subira kwa muda mrefu. Sasa Imetosha

Tulimwambia Benard Membe mapema wakati anakuja, kuwa tunashirikiana na chama makini na alikubali. Tuliona mgombea wetu haonekani bora, hata Mzee wa Ubwabwa (Hashim Rungwe) ni bora kuliko mgombea wetu, tukakubaliana kumuunga mkono Tundu Lissu

Kuna njama za wazi za kukamata viongozi wetu wa ACT Wazalendo na inasemekana yako maeneo yaliyotafutwa ili kuwaficha viongozi hao ili wasijulikane walipo mpaka uchaguzi uishe, sasa tunajiuliza serikali ya Chama cha Mapinduzi inaogopa nini?

Kuna minong'ono kuwa kuna vijana wa ACT Wazalendo wamevalishwa nguo za askari ili wakapige kura ya mapema. Kwa taarifa tulizonazo kuna zaidi ya wazanzibar 50,000 walionyimwa haki yao ya msingi ya kikatiba ya kupiga kura Zanzibar.
Kumbe! Basi wana ACT wote tusepe na Lissu.
 
Kwa nini usuburi mpaka uchaguzi upite? Tunataka kujua sasa ili tuamue kuwapigia kura au tusiwapigie
Wacha waendelee kutupiana maneno, tujue kama tuna wapinzani wa kweli
..ugomvi wao wasubiri baada ya uchaguzi.

..muda huu utumike kuwatafutia kura Maalim Seif, Tundu Lissu, wabunge, na madiwani wetu.
 
Fedha za Kampeni za Membe zimedhibitiwa Airport akitokea Dubai na wasaidizi wake wamekamatwa!

Sasa hizo kampeni atafanyaje peke yake bila ya sapoti ya secretariet ya ACT?

Lipumba mara zote za uchaguzi alikuwa anasimama kwa miguu yake na wajanja wenzie wa mjini, pesa zote za kampeni mnapeleka Znz kunajisi Mapinduzi mnataks Jasusi afanyaeje?
ACT hawana hela ya ruzuku, hela zilizopo ni michango toka kwa marafiki wa Maalimu ili washinde urais Zanzibar.
 
Back
Top Bottom