Zanzibar 2020 Maalim Seif aahidi kupambana na Dawa za Kulevya

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mgombea urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharrif Hamad amesema akifanikiwa kuingia Ikulu atahakikisha watu wanaojishughulisha na biashara ya dawa za kulevya wanadhibitiwa ili kuwaokoa vijna katika janga hilo.

Akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni katika viwanja vya Welezo, Unguja, mgombea huyo alisema vijana wengi Zanzibar wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya kutokana na kukosekana kwa mikakati ya kudhibiti tatizo hilo.

Alisema kazi inayofanywa na kikosi cha kupambana na dawa za kulevya ni kuwakamata wauzaji wadogo na kuwaacha wahusika wakubwa wakiendelea kufanya biashara hiyo bila ya wasiwasi.

‘’Nikifanikiwa kuingia Ikulu nataka kukomesha mara moja biashara ya dawa za kulevya, tutaweka udhibiti kuanzia uwanja wa ndege hadi katika bandari mbalimbali zilizopo Unguja na Pemba,” alisema.

Alisema hivi sasa vijana wengi wanaugua ugonjwa wa akili kutokana na athari za dawa za kulevya ambazo hupoteza nguvu kazi ya taifa.

Awali, Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Nassor Mazrui, alisema wanakusudia kukikamilisha kituo cha kutoa huduma kwa waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya kilichopo Kidimni, wilaya ya Kati Unguja na kuanza kutoa huduma kwa walengwa.

Alisema ujenzi wa kituo hicho umechukua muda mrefu huku fedha zake zote zipo, hivyo ACT-Wazalendo kupitia mgombea wake akifanikiwa kuingia madarakani kazi hiyo ataikamilisha.

‘’Mgombea wetu akifanikiwa kuingia madarakani atamaliza kazi ya ujenzi wa kituo cha kurekebisha vijana wanaotumia dawa za kulevya kilichopo Kidimni, kituo kile fedha zake zipo sasa sijui kwa nini kimechukua muda mrefu kumalizika,’’ alisema.

Aidha, aliwataka wanachama wa chama hicho mkoa wa Magharibi Unguja kuwachagua viongozi wa majimbo wa ACT-Wazalendo ili kuingia katika vyombo vya kutunga sheria na kuzifanyia kazi sheria zilizopitwa na wakati ambazo zinahitaji marekebisho.

‘’Wanachama na wafuasi wa ACT-Wazalendo baada ya kumchagua mgombea wa urais wa Zanzibar ambaye ni Maalim Seif, mnatakiwa muwachague wabunge na wawakilishi pamoja na madiwani ili waweze kuingia katika vyombo vya kutunga sheria na kufanya marekebisho ya sheria zilizopitwa na wakati,’’ alisema.
 
Muda huu yupo Kizimkazi. Mi naona huyu shughuli za uganga ndio inampendeza zaidi kuliko hayo wanayoyataka. Wanamtembeza kwa miguu na jua kali.
WP_20201009_11_36_20_Pro (2).jpg
 
Back
Top Bottom