Maalim Sef Shariff Hamad ameliambia jeshi la polisi yeye ndio rais aliyechaguliwa na Wazanzibar

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
Maalim Seif.jpg


KATIKA MAHOJIANO MAHUSUSI NA JESHI LA POLISI SEIF SHARIF HAMAD AMELIAMBIA JESHI LA POLISI KUWA YEYE NDIO RAIS ALIYECHAGULIWA NA WAZANZIBARI.

KATIBU Mkuu Wa Chama Cha Wananchi wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad alimeliyambia jeshi la polisi kuwa yeye ndie Rais wa wananchi wa Zanzibar aliyechaguliwa Octoba 25 katika Uchaguzi Mkuu na Dk Ali Mohamed Shein ni rais wa Tume ya uchaguzi Zanzibar.

Maalim Seif aliyasema hayo wakati alipohojiwa na jeshi la polisi jana na kutaka ajieleze kwa nini hamtambui Dk Shein kuwa ndio rais na badala yake anajitangaza kuwa yeye ndio Rais wa Zanzibar.

Katika Mahojiano hayo yaliyochukuwa muda wa masaa matatu kuanzia saa 3:30 hadi saa 6:20 baina yake na jopo la maafisa wa upelelezi wa jeshi hilo, Maalim Seif bila ya hofu wala woga aliliambia jeshi hilo kuwa yeye ndie rais wa Zanzibar na Dk Shein ni Dikteta.

Mwanasheria wake Awadhi Ali Said aliyeambatana na Maalim Seif katika mahojiano hayo, alisema hicho ndicho alichokiongea Maalim Seif mbele ya maafisa 12 wa upelelzi wa jeshi hilo .

Mahojiano hayo ambayo yalifanyika Makao makuu ya jeshi hilo, huku askari polisi wakiimarisha ulinzi maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar na kusababisha baadhi ya huduma kusimama kwa muda haswa maeneo ya Mtendeni ambapo ndio makao makuu ya CUF.

Awadhi alisema ,Maalim Seif aliulizwa na jeshi la polisi kwanini hakemei kitendo cha baadhi ya wananchi na wafuasi wa CUF kumtambua kuwa yeye ndie rais badala ya Dk Shein, aliwajibu kuwa ndio yeye ndie rais na wananchi ndio wanaoamini hivyo kwani walimchaguwa katika uchaguzi wa octoba 25 mwaka jana na sio Dk Shein.

Alisema pia aliulizwa kuwa amemuita Dk Shein ni Dikteta,Maalim Seif alikiri kuwa ni kweli ni Diktete kwa sababu uchaguzi wa huru na haki uliendeshwa octoba 25 na waangalizi wa ndani na nje wa Uchaguzi huo walithibitsha kuwa uchaguzi, ulikuwa ni huru na haki na yeye ndie aliyekuwa akiongoza katika uchaguzi huo kwa kupata kura nyingi na kumshinda Dk Shein.

Awadhi alimnukuu Maalim Seif alivyokuwa akihojiwa na jeshi hilo katika mahojiano hayo”mimi kama kiongozi wa CUF nasimamia maamuzi ya baraza kuu la chama changu ambayo kutoutambuwa uchaguzi wa marudio wa machi 20 mwaka huu na kuutambuwa uchaguzi wa octoba 25 mwaka jana na kuhakikisha kuwa tunafanya harakati za kisiasa ili serikali hii iliyopo ambayo imebaka demokrasia haimalizi muda wa miaka mitano”alisema Maalim Seif katika mahojiano hayo.

Aidha Awadhi alisema mahojiano hayo yalichukuiliwa maelezo ya kipolisi yaliyorikodiwa chini ya onyo la kisheria na Maalim Seif kutuhumiwa kwwa makosa ya kufanya uchochezi chini ya kifungu cha 45 sheria ya jinai ya Zanzibar.

Awadhi alieleza kuwa Maalim Seif alitakiwa ajieleze kwanni alifanya mikutano na maandamano kisiwani Pemba na kuoneshwa ushahidi wa picha za video za watu waliyojipanga barabarani lakini katibu mkuu huyo, alikanusha na kusema kuwa alikuwa akisherehekewa kama ni kiongozi wa kisiasa na hayakuwa maandamano na baadae alifanya mikutano ya ndani ya kuimarisha chama.

Pia Jeshi hilo lilimtaka ajieleze kutokana na matamshi aliyoyatoa katika mikutano hiyo kwa kutoa matamshi ya uchechezi ikiwemo kusema DK Shein hatomaliza muda wake, na alijibu kuwa ni kweli alisema DK Shein aliyoko katika mamlaka ambayo amewekwa na tume ya Uchaguzi hatomaliza miaka mitano ya uongozi .

Maalim Seif aliwahakikishia Maafisa hao wa jeshi la Polisi kuwa yeye na chama chake cha CUF, hakina dhamira ya kumdhuru DK Shein wala kuendesha taratibu nyengine zozote nje ya ulingo wa kisiasa bali watahakikisha kuwa Dk Shein atang’oka kupitia harakati za kisiasa.

Naibu Mkurugenzi wa upelelezi na Makosa ya jinai Salum Msangi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mahojiano hayo hakutaka kueleza kwa undani mahojiano hayo kati yao na Maalim Seif lakini alisema kuwa wamekamilisha mahojiano hayo na wamemuachia huru kwa dhamana ya watu wawili.

“tumemaliza mahojiano yetu kwa leo na tutakapomuhitaji tena tutamuita tena Maalim Seif na jeshi la polisi tunaendelea na upelelezi wetu na wote tuliowahoji watakaobainika kuwa wanahatia tutawapeleka mahakamani”alisema Msangi.

Chanzo : Mwandishi Wetu
 
Wanabodi, hii ya Maalim Seif kali!, majibu yake yanaonyesha ni mtu aliyetayari kwa lolote!, kama serikali ya CCM na kwa jinsi isivyo makini, inaweza kumpata Seif kile anachokitaka, akaiingiza Zanzibar katika sintofahamu nyingine!.

Seif anachotaka ni kuleta chokochoko ili atiwe ndani, kisha wafuasi wake wapate sababu za kisingizio cha kuyafanya waliopanga kuyafanya!.

Ningekuwa ni mimi Jeshi la Polisi, ningelibaini hilo, hivyo kamwe nisingeshulika naye kabisa bali kumpuuzia kwa jumla!, mwacheni ajiite yeye ndio rais as long as hana dola, wafuasi wake waachwe waandamane usiku na mchana, wafanye mikutano mfulululizo kila siku, waachewe wafanye kila wanachotaka hata wakiamua kutanguliza boda boda kwenye misafara yake ba blue guard wampigie saluti, mwacheni, kwa sababu yote hayo ni kujifurahisha tuu, rais wa kwenye ni yule mwenye mamlaka aliyeko ikulu ambae anatawala nchi, huyu ais wa mioyo ya watu, mwacheni aongoze mioyo!.

Hili la kumtambua Shein au kutokumtambua ni immaterial, kwa sababu uwepo wa rais ni uwepo wa kitu kinachoitwa being, yaani kipo, kujidai kuwa hukitambui kitu kilichopo ni kujifuahisha tuu, mwanacheni Maalim Seif na wafuasi wake wajifurahishe kwa raha zao!, if that is what that will make them happy, let them be happy!.

Ila katika kujifuahisha huko, kama wataingilia usalama, amani na utulivu wa Zanzibar, then hapo hawamchokozi Shein, bali watakuwa wanamchokoa Amiri Jeshi Mkuu, na aliisha sema hataki fyoko fyoko!.

Pasco
 
Kwa jinsi Polisi walivyofunga barabara jana na shughuli za kawaida kusimama kwani Polisi wenyewe hawaoni kuwa hali hiyo ya mahojiano kuwa ilikuwa ni Presidential?
Mkuu
Ben Saanane, .

Ningekuwa mimi Seif, hizo VIP treatment za mahojiano huko akimbelezwa na kudekezwa na polisi, zingenitia mashaka kuliko hata mahojiano yenyewe!,

Pasco
 
Mfa Maji tu huyo:
Kama yeye Rais wa Znz. basi ni vyema angejiapisha ili akalie kiti cha Ikulu.
Asilete porojo zisizo na msingi wowote, Taratibu anazifahamu vyema na afanye kama kweli yupo serious else apuuzwe hilo ni debe tupu.
 
Pasco unachosema ni kuwa Zanzibar iwe na Marais wawili, Shein aongoze ofisi na Maalim aongoze watu.
Hebu tafsiri maana ya uongozi kisha urudi.
Mkuu , hivi mimi nikiijiita ndio rais wa JMT with nothing!, kuna sababu yoyote ya Magufuli kuogopa au kutishika!, urais ni taasisi "presidential institution' na ina derive the powers from the instruments, sasa mtu asiye na lolote wala chochote kuibuka na kujitangaza kuwa yeye ndio rais with nothing, anafanya hivyo ili kumtia asira aliyepo, amtie ndani wapate uhalali wa kutimiza kile walichokipanga!. Aachwe tuu ili asipate sababu!.
Mwache aongoze mioyo mwingine aongoze nchi, hata hao waongozwa mioyo akiwemo Seif mwenyewe ni subject wa nchi chini ya anayeongoza nchi!.

Pasco
 
Mkuu , hivi mimi nikiijiita ndio rais wa JMT with nothing!, kuna sababu yoyote ya Magufuli kuogopa au kutishika!, urais ni taasisi "presidential institution' na ina derive the powers from the instruments, sasa mtu asiye na lolote wala chochote kuibuka na kujitangaza kuwa yeye ndio rais with nothing, anafanya hivyo ili kumtia asira aliyepo, amtie ndani wapate uhalali wa kutimiza kile walichokipanga!. Aachwe tuu ili asipate sababu!.
Mwache aongoze mioyo mwingine aongoze nchi, hata hao waongozwa mioyo akiwemo Seif mwenyewe ni subject wa nchi chini ya anayeongoza nchi!.

Pasco
Pasco ilo ni hatari zaidi
Hivi unajua madhara ya maandamano?
 
Mfa Maji tu huyo:
Kama yeye Rais wa Znz. basi ni vyema angejiapisha ili akalie kiti cha Ikulu.
Asilete porojo zisizo na msingi wowote, Taratibu anazifahamu vyema na afanye kama kweli yupo serious else apuuzwe hilo ni debe tupu.
Shida kubwa la Vijana wengi ktk Taifa letu ni kutokuwa na upeo mkubwa wa uchambuzi ktk masuala ya Kisiasa, Kiuchumi,Kiutamaduni n.k na hatimaye kuongozwa na HISIA.
Kama hoja yako hapo juu inaonyesha ni MAHABA YA LUMUMBA, speed without Brain.
Never discuss heavy things that is beyond you're Brain capacity & require deepthinking.
 
Saddam Hussein alipokuwa anahojiwa na Jaji kule Baghdad nae kwa kibri na jeuri alikuwa akimhoji Jaji eti umepewa na nani haki ya Kumhoji Rais wa Jamhuri ya Iraq, majibu hayo mepesi mepesi hayakumnusuru asinyongwe Muda ulipo taraddadi!
 
Back
Top Bottom