Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
Wadau: Ni kweli asemayo huyu mjamaa, kwamba ana majukumu mengi? Kufuatana na katiba iliyorekebishwa, majukumu yake ni kiduchu sana vipi ataelemewa? Ama anaanza kupora majukumu ya wengine? CCM waangalie hapa, wanaweza kujikuta wao wako sebuleni na yeye wakamkuta yuko jikoni!
Maalimu Seif: Nimeelemewa
na Bakari Kimwanga
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya umoja ya kitaifa ya Zanzibar na ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuwa majukumu ya kiserikali yamemuelemea na kuwaomba wajumbe wa baraza kuu la uongozi wa chama hicho kumtafutia msaidizi.
Seif, aliyasema hayo jana katika mkutano wa ufunguzi wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF, uliofanyika katika Hoteli ya Trez Motel, iliyoko Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam ambapo aliwasili katika mkutano huo akiwa na ulinzi mkali wa maofisa wa serikali na polisi, huku akisindikizwa na msafara maalum wa magari matano pamoja na pikipiki ya polisi.
Akizungumza katika mkutano huo mbele ya wajumbe, Seif alisema majukumu ya kiserikali yamekuwa ni makubwa, lakini pamoja na ombi lake, alisisitiza kuwa bado ataendelea kuwa Katibu Mkuu kwa mujibu wa katiba ya CUF.
Alisema umefika wakati ni lazima kwa wanachama na viongozi wa CUF, kutambua thamani na dhamana waliyopewa na wajumbe ya kuhakikisha chama kinashika hatamu ya uongozi hali ambayo hivi sasa imekuwa ni sehemu ya mafanikio ndani ya chama hicho.
Mbali na hilo pia katika mkutano huo Maalimu Seif, alimsifia mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba, kwa juhudi kubwa anazozifanya ili kuhakikisha CUF inasonga mbele na kueleweka mbele ya macho ya Watanzania wa ndani na nje.
Akizungumzia mkutano huo alisema kupitia kikao hicho cha Baraza Kuu la uongozi watafanya tathmini ya kina na kujadili namna walivyoshiriki uchaguzi na mapungufu yake huku wakiweka malengo na mikakati kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Maalim Seif, alionya na kusema kuwa mafanikio yaliyopatika na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ni moja ya njia ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu na viongozi hawana budi kuunga mkono hatua hiyo baada ya kukosa chaguzi tatu mfululizo.
Awali akimkaribisha Maalim Seif kuhutubia, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, alisema kitendo cha Rais wa Zanzibar kuheshimu katiba na maamuzi ya Wanzibari ni jambo la kujivunia na anastahili kupongezwa na kila mpenda demokrasia ya kweli nchini.
Profesa Lipumba, alisema kama sio burasa na hekima za Maalim kukubali matokeo ya uchaguzi huo Zanzibar, ingekosa mwelekeo na kuacha makovu kwa wananchi visiwani humo na kutoa wito kwa mawaziri hasa kupitia CUF, kuwa waadilifu na kutunza rasilimali za taifa kwa manufaa ya Wazanzibari wote.
Leo tunafanya kikao cha Baraza Kuu huku tayari tukiwa na Makamu wa Rais na mawaziri katika sehemu moja ya Tanzania na hakika Zanzibar sasa imedhihirika kuwa ni mlango wa demokrasia nchini, alisema Profesa Lipumba.
Alisema matatizo ya msingi yanayoikabili Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ni kukosekana kwa huduma za afya, umaskini na ujinga; ni mambo muhimu ambayo kila waziri anatakiwa kuyashughulikia bila kujali itikadi za wananchi na vyama vyao.
Chanzo: T. Daima