Maalim ataelemewa vipi na hali kakaribishwa sebuleni tu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalim ataelemewa vipi na hali kakaribishwa sebuleni tu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Dec 11, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wadau: Ni kweli asemayo huyu mjamaa, kwamba ana majukumu mengi? Kufuatana na katiba iliyorekebishwa, majukumu yake ni kiduchu sana – vipi ataelemewa? Ama anaanza kupora majukumu ya wengine? CCM waangalie hapa, wanaweza kujikuta wao wako sebuleni na yeye wakamkuta yuko jikoni!


  Maalimu Seif: Nimeelemewa


  na Bakari Kimwanga

  MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya umoja ya kitaifa ya Zanzibar na ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuwa majukumu ya kiserikali yamemuelemea na kuwaomba wajumbe wa baraza kuu la uongozi wa chama hicho kumtafutia msaidizi.

  Seif, aliyasema hayo jana katika mkutano wa ufunguzi wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF, uliofanyika katika Hoteli ya Trez Motel, iliyoko Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam ambapo aliwasili katika mkutano huo akiwa na ulinzi mkali wa maofisa wa serikali na polisi, huku akisindikizwa na msafara maalum wa magari matano pamoja na pikipiki ya polisi.

  Akizungumza katika mkutano huo mbele ya wajumbe, Seif alisema majukumu ya kiserikali yamekuwa ni makubwa, lakini pamoja na ombi lake, alisisitiza kuwa bado ataendelea kuwa Katibu Mkuu kwa mujibu wa katiba ya CUF.

  Alisema umefika wakati ni lazima kwa wanachama na viongozi wa CUF, kutambua thamani na dhamana waliyopewa na wajumbe ya kuhakikisha chama kinashika hatamu ya uongozi hali ambayo hivi sasa imekuwa ni sehemu ya mafanikio ndani ya chama hicho.

  Mbali na hilo pia katika mkutano huo Maalimu Seif, alimsifia mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba, kwa juhudi kubwa anazozifanya ili kuhakikisha CUF inasonga mbele na kueleweka mbele ya macho ya Watanzania wa ndani na nje.

  Akizungumzia mkutano huo alisema kupitia kikao hicho cha Baraza Kuu la uongozi watafanya tathmini ya kina na kujadili namna walivyoshiriki uchaguzi na mapungufu yake huku wakiweka malengo na mikakati kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

  Maalim Seif, alionya na kusema kuwa mafanikio yaliyopatika na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ni moja ya njia ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu na viongozi hawana budi kuunga mkono hatua hiyo baada ya kukosa chaguzi tatu mfululizo.

  Awali akimkaribisha Maalim Seif kuhutubia, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, alisema kitendo cha Rais wa Zanzibar kuheshimu katiba na maamuzi ya Wanzibari ni jambo la kujivunia na anastahili kupongezwa na kila mpenda demokrasia ya kweli nchini.

  Profesa Lipumba, alisema kama sio burasa na hekima za Maalim kukubali matokeo ya uchaguzi huo Zanzibar, ingekosa mwelekeo na kuacha makovu kwa wananchi visiwani humo na kutoa wito kwa mawaziri hasa kupitia CUF, kuwa waadilifu na kutunza rasilimali za taifa kwa manufaa ya Wazanzibari wote.

  “Leo tunafanya kikao cha Baraza Kuu huku tayari tukiwa na Makamu wa Rais na mawaziri katika sehemu moja ya Tanzania na hakika Zanzibar sasa imedhihirika kuwa ni mlango wa demokrasia nchini,” alisema Profesa Lipumba.

  Alisema matatizo ya msingi yanayoikabili Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ni kukosekana kwa huduma za afya, umaskini na ujinga; ni mambo muhimu ambayo kila waziri anatakiwa kuyashughulikia bila kujali itikadi za wananchi na vyama vyao.

  Chanzo: T. Daima
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Ameanza ku-prove bila ya chembe ya doubt kwamba daima amekuwa ni mtu mwenye uchu mkubwa wa madaraka. kakaribishwa sebuleni sasa anataka kuingia jikoni!
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huwa najiuliza mara nyingi hili swali: Hivi huyu mjamaa, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, anaweza kuyasimamia masilahi ya watu wa huku Bara kwa kupitia hicho chama? Mimi nadhani madhali kisha ula katika serikali ya mapinduzi ya zanzibar, basi automatically kapoteza sifa za kuwa kiongozi wa chama cha upinzani -- hivyo CUF wanatakiwa wachague Katibu mkuu mwingine.
   
 4. C

  Calipso JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kwani kaupata umakamo wa Rais kupitia wapi? kupitia ccm? then angalia uzuri speech yake, anasema haya ni mafanikio makubwa kwetu ktk harakati zetu za kushika khatamu.. sasa ujue hilo ndio lengo letu Cuf,na kwa kua sasa tumo serikalini ni wajibu wetu sasa kuonesha sisi ndio chama mbadala,na jengine kuhakikisha tunaweka mazingira mazuri ya uchaguzi ujao,ili ufanyike kwa huru na wa hakki...
   
 5. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Maalim Seif ni mwongo sana. Kwanza anatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo aimuhusu sasa ataelemewa vipi na majukumu? Hizi ni siasa za maji machafu ambazo zinatakiwa zisitupotezee muda hapa JF. Alichotaka ni madaraka na ameshayapata basi kwake imetosha.
   
 6. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ameelemewa kukata tepe au,mpunguzie mikasi mfukoni
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  wakuu,


  Ninyi mumesomea siasa chuo kipi? au ndio siasa za vitabuni tu? hamutaki uhalisia katika jamii na mitaani.


  Kama ameingia sebuleni huyu mzee inabidi apongezwe. Ninyi hamujuwi nini kilitokea Zanzibar 2001?


  Mulipendelea uwepo mgogoro mwengine kule?


  Mimi nampongeza sana Seif na CUF kwa chenga safi, chenga ya mwili waliyowapiga CCM.
  Sifikirii kuwa CCM walitegemea CUF watakubali compromise waliyoitoa.

  Kuwa CCM lazima iongoze serikali na wao CUF ingawa wameshinda ila wawe washindwa.
  CCM hawakuwa wanataka GNU na kama CUF wangekataa wangerudi "skweya 0, sio 1", Sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano ingekuwa hamkani, damu kumwagika, watu kuteswa.


  Hili lilikwishatokea, sisi tunaosema jamaa kaisha, jamaa mpenda madaraka, tuliwaunga mkono vipi walipotuonesha kuwa haki pia hudaiwa kwa kuingia mitaani.

  Tulikaa tukawa tunachekelea tu, tuliona hayatuhusu. yamekuja kwetu sasa, Kila mpenzi wa Upinzani huku Bara anasema tu CCM wamechakachuwa. Tumechukuwa hatuwa gani?


  Tunadai katiba mpya... Kule zenj wamebadili katiba kidogo tu, tunawapigia kelele kuwa wamekiuka katiba ya jamhuri ya muungano.

  Ukweli unabakia CUF wamepiga hatua moja mbele.


  Pia nampongeza sana Dr. Slaa kwa kuwataka na kuwasihi wanachadema na wananchi wadai mabadiliko kwa amani.

  Misimamo mikali katika siasa za kileo hazina nafasi, watu ni lazima wawe pragmatic na flexible.

  Kauli ya Seif ya Kukataa matokeo Zanzibar ingeingiza Tanzania nzima katika hamkani, piga ,nguo chanika.


  Na siasa si maneno tu. si hamasa na ushabiki tu.


  Isionekane kuwa ninapendwezwa na wanachokifanya CCM. CCM ni ving'ang'anizi wa madaraka, na wana vyombo vya dola behind.

  Tusijifanye vipofu. suala vipi tutaweka a level playing ground katika siasa za TZ?

  Kama muna majibu hapa tafadhalini ,leteni michango yenu.

  Musifanye character assassination. Hiyo ielekezeni kwa CCM na viongozi wake, Inawastahikia wao. Sio Seif au Dr, Slaa. au yeyote katika upinzani.


  Mulipendelea damu imwagike kwa mara nyengine? au...!!??
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Dec 12, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Nimemuona hivi juzi kati nikakumbuka kuwa kila kitu kina mahala pake. Huyu bwana mkubwa yake ni yale madaraka. Sijui kama tutamsikia tena.
   
 9. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,466
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Maalimu Seif siyo mjinga au mpenda madaraka kama wengine wanavyofikiri,akiwa ndani ya serikali anakuwa na nafasi nzuri, itakuwa rahisi kwake kusukuma agenda za CUF kuliko akiwa nje,kwani kinachotakiwa ni maelewano,haki za msingi za mwananchi,na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.Zipo njia nyingi za kumaliza migogoro ndani ya jamii zetu,mmoja wapo ni hiyo ya Maalim Seif.Tumpe muda.
   
Loading...