Maalbino, wastaafu eac, walimu, madaktari, manesi na wanasheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalbino, wastaafu eac, walimu, madaktari, manesi na wanasheria

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by akili, Oct 30, 2008.

 1. a

  akili Member

  #1
  Oct 30, 2008
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HUKO Niger, sio Nigeria kama watangazaji fulani Tanzania wasiojua jiografia wanavyokosea kuna dada mmoja kaishtaki serikali yake kwa kushindwa kumlinda.

  Ninauliza, je, kwa hapa Tanzania haiwezekani ndugu zangu Maalibino mkaishataki serikali yetu kwa kushindwa kuwalinda. Hebu waoneni wanasheria wawashauri!

  Msikubali kufanyiwa usanii wa kucheza mpira wakati wa jua huku nyie hamuwaoni au kushibishwa na hotuba nzuri ambazo ukiamkia asubuhi yake tayari mwenzenu mwingine kamalizwa.

  Maana serikali yenyewe na wizara yenyewe ilivyokaa ni kwamba inalichukulia jambo hili kama ni uahalifu wa kawaida. La, hasha. Hilo hata kwa kipofu na kiziwi wanajua sio sawa. Huu ni uhalifu wa aina yake na unataka dhamira na mkakati maalum wa kushughulikia.

  Nyie msipokuwa mstari wa mbele katika hili niaminini hamtafika popote. Na serikali yenyewe ndio hii? Na viongozi wenyewe ndio hawa? Labda iwe maajabu!

  Watu wa ofisini na tai na viyoyozi toka lini wakawa wa msaada wa raia wa kawaida?

  Hakikisheni mnakuwa mstari wa mbele ili mauaji ya ALBINO yasienee pembe nyingine za Kiafrika. Mnajua tena kwa umasikini wetu kuna mamilioni ya wajinga wanaoamini wanaweza kutajirika kwa nguvu za kishirikina bila kutumia akili na maarifa.

  Wastaafu wa EAC acheni kulala barabarani tafuteni NGOs na taasisi nyingine za kisheria kupeleka dhuluma mliyofanyiwa na serikali toka ile ya awamu ya 1 hadi ya 4 ili washughulikiwe na mahakama na vyombo vya sheria vya kimataifa.

  Mahakama za kimataifa haziwashughulikii tu viongozi wezi na wauaji bali pia hata serikai na viongozi wanaowadhulumu watu wao. Watakwenda wapi na wao kwa utegemezi ndio namba moja!

  Walimu, madaktari na manesi tafuteni wataalamu wa masuala ya mishahara na haki za wafanyakazi toka ILO na kwingineko na kuishtaki serikali kwa kuwanyonya kutokana na mishahara isiyofika hata tarehe tano ya mwezi.
   
 2. m

  msanii.namba1 New Member

  #2
  Oct 30, 2008
  Joined: Oct 30, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAUNGA mkono wanasheria wasaidieni maalbino, wastaafu mbalimbali, wazee, mayatima, walemavu na wanaostahili kulindwa na jamii/serikali kushtaki serikali, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, serikali za mitaa, wabunge na polisi kwa kushindwa kuwalinda.

  Hii sio miaka ya watu kukaa na kula tu bila kufanya kazi eti. Tupeni kazi muone. Kwani ni wanasheria wa BOT tu wanaoweza kuwa mamilionea. Wanasheria msidharau mlo hata ukiwa ugali na dagaa au wali kwa kauzu au baada kwa mlenda!
   
 3. w

  wajinga Senior Member

  #3
  Oct 30, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  There is a war against Albinos in this country and it should be understood that this is a crime against humanity and there are several courts which can address this issue i.e abroad and in the country. They should go to the UN OAU and anywhere where their cries will be heard.
   
 4. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  TUNDU LISSU tafadhali okoa jahazi
   
Loading...