Maajabu yatokea shule ya msingi Tingi ,Wanafunzi wakumbwa na ugonjwa wa ajabu.

Mr Suprize

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
818
842
Kuna hali ya taharuki imeikumba shule ya msingi Tingi iliyopo wilaya ya nyasa mkoani Ruvuma.
4c9e381abc56721753a3507e74d6e0ed.jpg

Shule hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1947 imekumbwa na tatizo la wanafunzi wake kuzirai, kupatwa na mapepo ya ajabu na baadhi ya wanafunzi kuwa katika hali ya ukichaa na kuanza kuwapiga wanafunzi wenzao pamoja na walimu wao. Hali hiyo hutokea tu muda ambao wanafunzi wanakuwa shuleni.

Taharuki hiyo imeanza kutokea wiki hii ambapo siku ya kwanza walianguka wanafunzi 25 wote jinsia ya kike, siku iliyofuata takribani wanafunzi 50 walikumbwa na ugonjwa wa kuanguka na kuzirai wakiwa darasani , na leo wanafunzi 6 pia wamekumbwa na tatizo wakiwa shuleni hapo. Asilimia kubwa ya wanaokumbwa na tatizo hilo ni wanafunzi wakike. Na tatizo hilo huendelea kutokea kwa baadhi ya wanafunzi hata wakiwa nyumbani kwao.

Kutokana na hali hiyo mahudhurio ya wanafunzi yamepungua kwa asilimia kubwa sana , ambapo mahudhurio ya leo yanaonyesha wanafunzi 45 tu ndio waliohudhuria shuleni kati ya wanafunzi 760.

MKUU WA SHULE AFUNGUKA.
Alipoulizwa mkuu wa shule hiyo alidai kuwa baada ya tukio hilo kutokea siku ya kwanza waliitwa madaktari bingwa kutoka wilayani kuwapima wanafunzi hao na kubaini kuwa baadhi ya wanafunzi walikumbwa na vimelea vya ugonjwa wa malaria, na wanafunzi wengine walikula chakula kisicho bora kutoka nyumbani kwao. Kwa mujibu wa mkuu wa shule anaendelea kusema madaktari pia walibaini chanzo cha tatizo hilo ni population ya wanafunzi katika shule hiyo , hali inayosababisha kukosekana kwa upatikanaji wa hewa safi kwa wanafunzi.

AFISA ELIMU WILAYA.
Akizungumza na baadhi ya wazazi shuleni hapo Afisa elimu wilaya ya nyasa amewaeleza wazazi kuwa hali hiyo hutokea sana hasa katika mazingira ambayo yanakutanisha watoto wengi na kudai kuwa hali hiyo itatoweka muda si mrefu.
Baadhi ya wazazi wameshindwa kumwelewa na kuiomba serikali isitishe ratiba za masomo shuleni hapo mpaka tatizo lipatiwe ufumbuzi.

JAMII INASEMAJE?
Baadhi wa wadau mbalimbali wanalichukulia suala hilo kwa jicho la kipekee huku wakidai linaukishirikina ndani yake.
Habari ambazo siyo rasmi Inasemekana shule hiyo ina mzee wa mila mmoja tu ambapo wazee wengine wanadai ameishiwa nguvu ajiuzuru nafasi apewe mzee mwingine. Kutokana na madai hayo mzee wa mila aliyepo madarakani amegoma kujiuzuru cheo hicho na kuwataka wazee wenzake wanaodai ameishiwa nguvu wapambane na hali yao.
Majibu hayo yamepandisha hasira kwa wazee hao na kuamua kumkomoa mzee wa mila aliyepo madarakani kwa kuleta ugonjwa wa ajabu kwa wanafunzi wanaosoma shule hiyo, huku wakimtaka mzee wa mila aliyepo madarakani kama ana nguvu basi atatue suala hilo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom