Maajabu ya ziwa la mifupa ya binadamu India

Bujibuji Simba Nyanaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
62,561
2,000
Mabaki ya watu wanaokadiriwa kuwa 600-800 yalipatikana kwenye eneo hilo

Juu katika milima ya Himalaya nchini India, ziwa lililo kwenye bonde lenye theluji, limetapakaa mamia ya mifupa ya binadamu.
Mto Roopkund uko umbali wa futi 16,500 juu ya usawa wa bahari chini ya mteremko mkali wa Trisul, moja ya milima mirefu, katika jimbo la Uttarakhand.

Mabaki yametapakaa kuzunguka na chini ya barafu katika ''ziwa la mifupa'', lililogundulika na walinzi wa misitu waliokuwa kwenye doria mwaka 1942.

Kutegemea na msimu na hali ya hewa, ziwa, ambalo huganda kwa karibu mwaka mzima, hutanuka na kusinyaa. Pale tu barafu inapoyeyuka, mifupa huonekana, wakati mwingine ikiwa imeshikamana na nyama. Mpaka sasa, mabaki ya mifupi ya watu 600-800 imepatikana hapa. Katika kutangaza utalii, serikali ya eneo hilo huliita ziwa hilo ''ziwa la ajabu''.

Kwa zaidi ya nusu-karne wanaanthropolojia na wanasayansi wamefanyia utafiti mabaki hayo na kuuliza maswali mengi.
Watu hawa ni nani? walikufa lini?, walikufa vipi? walikuwa wanatoka wapi?

Nadharia moja ya zamani inayohusisha mabaki hayo na mfalme wa India, mkewe na wahudumu wao, ambao wote waliangamia katika tufani kali ya theluji miaka 870 iliyopita.

Ziwa la mifupa

Mwingine amesema kuwa baadhi ya mabaki ni ya wanajeshi wa India ambao walijaribu kuvamia Tibet mwaka 1841, na kudhibitwa. Zaidi ya 70 kati yao kisha walilazimishwa kurudi kwao kupitia milima ya Himalaya na kupoteza maisha wakiwa njiani.

Lakini mwingine anafikiria kuwa haya yanaweza kuwa "makaburi" ambapo waathiriwa wa janga walizikwa. Katika vijiji katika eneo hilo, kuna wimbo maarufu wa watu unaozungumza juu ya jinsi mungu wa kike Nanda Devi alivyounda dhoruba ya mvua ya mawe "ngumu kama chuma" ambayo iliwaua watu wanaopita katika ziwa. Mlima wa pili kwa urefu nchini India, Nanda Devi, anaheshimiwa kama mungu wa kike.

Katika tafiti za mifupa za awali zilibaini kuwa watu wengi waliokufa walikuwa warefu- ''kuliko wastani ''. Wengi wao walikuwa wenye umri wa kati, miaka 35 na 40. Hakukuwa na watoto wachanga wala watoto wadogo. Baadhi yao walikuwa wanawake watu wazima. Wote walikuwa na afya njema.

Pia, kwa ujumla ilidhaniwa kuwa mifupa hiyo ilikuwa ya kundi moja la watu waliokufa wote mara moja katika tukio moja la maafa wakati wa Karne ya 9.

Utafiti wa hivi karibuni wa miaka mitano, unaojumuisha waandishi wenzi 28 kutoka taasisi 16 zilizo India, Marekani na Ujerumani, uligundua dhana hizi zinaweza kuwa si kweli.

Wanasayansi wamechanganua vinasaba na kutoa kaboni kwenye mabaki ya miili 38, pamoja na wanawake 15, waliopatikana ziwani - baadhi yao ni ya miaka karibu 1,200 iliyopita.

Wakati barafu inapoyeyuka mabaki huonekana kwenye eneo la ziwa

Hivyo wanasayansi wanaamini kuwa baadhi ya miili iliyopatikana eneo hilo ni sababu ya ''vifo vya watu wengi wakati wa hijja''.

Lakini ni kwa namna gani watu kutoka mashariki mwa Mediterranea walifika mbali hivi katika eneo la milima nchini India?

Inaonekana pengine watu kutoka Ulaya wanaweza kuwa walisafiri kutoka Roopkund kushiriki hija ya Hindu.

Au ilikuwa watu waliotengwa kutoka kwenye asili ya mbali ya mashariki mwa Mediterania ambayo ilikuwa ikiishi katika eneo hilo vizazi hadi vizazi?

''Bado tunatafuta majibu'' alisema mwanasayansi Eadaoin Harney, kutoka Chuo Kikuu cha Harvard
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,854
2,000
ni kweli Bujibuji nimeukuta huo mto na maajabu yake
1621191827167.png

pia ipo humuhumu JF
 

Bujibuji Simba Nyanaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
62,561
2,000
ni kweli Bujibuji nimeukuta huo mto na maajabu yake
View attachment 1787761
pia ipo humuhumu JF
Thanks bro
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom