Maajabu ya Watanzania kuikashifu Kenya kwenye masuala ya haki na uhuru wa kujieleza

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,757
48,406
Watanzania wanafiki sana haswa wa mlengo wa CCM, huwa wana mazoea ya kuelekeza vidole vya lawama kwa kila taifa ila wao hujiona kama wastaarab walionyooka kuzidi mataifa mengine yote.

Leo wanakesha kwenye mitandao wakikashifu Wakenya kuhusu propaganda za kukamatwa kwa msanii King Kaka ambaye amewachana wanasiasa na serikali ya Kenya, ilhali ukweli wa mambo hamna ukweli wowote kwa hili, jamaa yuko salama na hakuna aliyemgusa maana kwetu Kenya tunaheshimu utawala wa sheria na uhuru wa kila mmoja kujieleza au kuachia hisia zake. Uhuru huu hatukuupata kihivi hivi, ilikua kwa mbinde.

Mwanasiasa mmoja tu ndiye amejitokeza na kuonyesha kukerwa na huyu msanii, ila ameahidi atafuata njia za kikatiba na sheria kupambana naye.

Wao huko Tanzania leo hii kuna mwanahabari anaitwa Kabendera anaozea gerezani kisa kaandika kuishutumu serikali yao. Visa vya wasanii kupata cha moto huwa tunavisoma kila pale wanaishutumu serikali au kuwasema vibaya wanasiasa, jamaa wanakamatwa au kutoweka, mifano kama Roma kutoweka, Nay wa Mitego kukamatwa, SHILAWADU kuvamiwa kituoni, kuna yule mwingine kupelekeshwa kisa amemtakia rais heri njema ya siku ya kuzaliwa kwa kutumia picha yake rais....mifano mingi sana inayoonyesha kwa hali gani Tanzania hawana jeuri ya kutusema kwa lolote, wao wako nyuma sana tena huko chini kwenyewe, mara bendera za chama cha upinzani zinashushwa.

Tanzania ya leo haina sifa wala jeuri ya kutukashifu kwa lolote, hata ukabila ambao ndio kete walikua wanashkilia miaka yote, leo hii kwa wale wanaifahamu Tanzania ya leo, ukabila umeshamiri kuliko wakati mwingine wowote. RC anadiriki kuwaagiza polisi wazunguke kila wakikuta vikundi vya kusadiana kwenye msiba vimekusanyika, wahoji ni kabila lipi, kama ni kabila la Kilimanjaro lifurushwe, jambo kama hili Kenya halijawahi kutokea, yaani dah! Hii video hapa.
 
Kuna uhuru wa kuongea lakini siwezi kukuhakikishia kuhusu uhuru baada ya kuongea," Idi Amin
 
Back
Top Bottom