Maajabu ya Wahenga na tiba zao, usipite bila kusoma huenda ikakusaidia na wewe

shankal

JF-Expert Member
Jul 11, 2013
372
324
Habari za majukumu wakuu,

Miezi miwili iliyopita nilikuwa nasumbuliwa sana na mafindofindo(tonsils) yani yalikua yana vimba na kuuma sana nikitumia dawa yana pona, baada ya siku mbili yana rudi miezi miwili mfululizo.

Sasa mwezi huu mwanzoni yakanianza tena, kabla sijaenda hospitali, kuna mahali nikaenda kunyoa ilikua mida ya jioni hivi, katika maongezi maongezi pale saloon, nikaanza kulalamika kuhusu tatizo langu.

Kuna jamaa akaniambia mbona dawa ndogo tu wala haiitaji pesa, tena yeye aliwahi kutumia zamani akiwa mdogo kwa kuelekezwa na babu yake hadi leo hii hajawahi kuumwa mafindofindo na anatafuna hadi mabarafu.

Akaanza kunielekeza, nichukue maji kwenye kikombe na kaa lenye moto alafu lile kaa la moto nilitumbukize kwenye kikombe chenye maji alafu ninywe yale maji haraka huku lile kaa la moto likiwa ndani linachemka.

Nilipo rudi tu nyumbani nikafanya kama alivyo nielekeza jamaa alafu nikaenda kulala maana ilishakua usiku.
Nilipoamka asubuhi siku amini, yani koo lipo safi hakuna hata chembe ya maumivu na hadi sasa nipo freshi kabisa.

Hivyo nimeona nishee na nyie wakuu kama kuna mwenye hilo tatizo ajalibu huenda na yeye ikamsaidia.

Wasalam.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kalibu mkuu, kiukweli tunadharau tu kwaajili ya usasa lakini tiba zake hazina madhara kama unapona vizuri, maana haubugii makemikali
Safi sana mkuu. Mwenyewe nataka nije kuchukua mwaka mmoja kufanya utafiti wangu wa hizi dawa kutoka kwa wazee tofauti kutoka jamii tofauti kwa kuzingatia jografia zao(weather)

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tiba kwa wanaokojoa kitandani.
Tafuta kisiki cha mti mkubwa wowote uliokatwa ambao maji yanaweza kutuama kwa juu,siku mvua ikinyesha nenda uchote kidogo maji yake kwa mkono unywe, dozi ni mara moja tu.
Rejea:
Watu wazima wengi hukojoa kitandani mara mojamoja sana kwa bahati mbaya, hasa wanandoa .
 
[QUOTE="Tetragrammaton, post: 39933072, member: 641352
Rejea:
Watu wazima wengI hukojoa kitandani mara mojamoja kwa bahati mbaya, hasa wanandoa .[/QUOTE]

watu wazima wanakojoa kitandani??? Sure??
 
Tiba kwa wanaokojoa kitandani.
Tafuta kisiki cha mti mkubwa wowote uliokatwa ambao maji yanaweza kutuama kwa juu,siku mvua ikinyesha nenda uchote kidogo maji yake kwa mkono unywe.
Rejea:
Watu wazima wengI hukojoa kitandani mara mojamoja kwa bahati mbaya, hasa wanandoa .
unakunywa mara moja tu mkuu au
 
Ngoja wasomi uchwara wenye PHD,& Degrees za kuakalili past papers waje wakosoe hii thread, kuwa dawa za kienyeji hazina vipimo wala hazina ubora..hawa wapuuzi ndyo wanaoturudsha nyuma afrika aiendelei sabb ya wajinga wachavhe kudharau makuu ya afrika na kukimbatia ugeni wakishenzi....hata kwenye covid19 mmewaona weng wao akili zakijinga yaan akili za chafu(mental slavery)...jarbu kugusia uviko uone madalali watakavyokuja hapa kutukana
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom