Maajabu ya Wahenga na tiba zao, usipite bila kusoma huenda ikakusaidia na wewe

shankal

JF-Expert Member
Jul 11, 2013
299
250
Habari za majukumu wakuu,

Miezi miwili iliyopita nilikuwa nasumbuliwa sana na mafindofindo(tonsils) yani yalikua yana vimba na kuuma sana nikitumia dawa yana pona, baada ya siku mbili yana rudi miezi miwili mfululizo.

Sasa mwezi huu mwanzoni yakanianza tena, kabla sijaenda hospitali, kuna mahali nikaenda kunyoa ilikua mida ya jioni hivi, katika maongezi maongezi pale saloon, nikaanza kulalamika kuhusu tatizo langu.

Kuna jamaa akaniambia mbona dawa ndogo tu wala haiitaji pesa, tena yeye aliwahi kutumia zamani akiwa mdogo kwa kuelekezwa na babu yake hadi leo hii hajawahi kuumwa mafindofindo na anatafuna hadi mabarafu.

Akaanza kunielekeza, nichukue maji kwenye kikombe na kaa lenye moto alafu lile kaa la moto nilitumbukize kwenye kikombe chenye maji alafu ninywe yale maji haraka huku lile kaa la moto likiwa ndani linachemka.

Nilipo rudi tu nyumbani nikafanya kama alivyo nielekeza jamaa alafu nikaenda kulala maana ilishakua usiku.
Nilipoamka asubuhi siku amini, yani koo lipo safi hakuna hata chembe ya maumivu na hadi sasa nipo freshi kabisa.

Hivyo nimeona nishee na nyie wakuu kama kuna mwenye hilo tatizo ajalibu huenda na yeye ikamsaidia.

Wasalam.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

kirikou1

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
4,063
2,000
Safi sana mkuu. Mwenyewe nataka nije kuchukua mwaka mmoja kufanya utafiti wangu wa hizi dawa kutoka kwa wazee tofauti kutoka jamii tofauti kwa kuzingatia jografia zao(weather)

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom