Maajabu ya ulimwengu wa Mapenzi, kwanini kadri muda uendavyo wapenzi wanachukiana, mahusiano kuvunjika au kuuana?

Mkiwa mumeungana (wapenzi) kwa sababu ya mapenzi pekee mwisho wa siku mtachokana kwa sababu kuna maisha mengine na mambo mengine ya kujadili nje ya mapenzi.

Ila wanandoa mkiwa ni watu mnaelewana mnapiga stori wote,mnashare experience za maisha,mnapeana umbea wa makazini yaani mnaishi kama mtu na rafiki yake hapo maana yake mkiwa bored na mapenzi basi urafiki wenu unawaunganisha maisha yanaendelea.

Jiulize kwamba yule rafiki yako hasa ushawwahi kuwa bored ama ukamchoka kwamba hujiskii kukaa naye ?
Wengi watasema hapana kwa maana rafiki haboi rafiki hachoshi kwa sababu muna mambo mengi ya kushare na kuzungumza yanayowafanya muendelee kuhitaji kuwa pamoja.

Ila imagine tu huyo huyo rafiki yako mkawa kila mkikaa mnazungumzia urafiki wenu tuu mlianzaje kuwa marafiki namna mnavyopendana na urafiki wenu basi mkiwa na stori za mfumo huu tuu lazima mtachokana maana mtakuwa hamna jambo jipya..

Na kadhaalika mkeO ndio hivyo hivyo,ikiwa wewe na mkeo stori zenu ni mapenzi tuu hamna stori zingine basi itafika hatua mtachokana kwa sababu binadamu anatakiwa awe na mambo mengi ya kuzungumza sio ngono tuu muda wote na mkeo.

mkiwa mnaunganishwa na ngono tu utakuta mkiwa bored na mapenzi mnakuwa kama mabubu ndani hakuna extra stories za kupiga.

Hii ni kwa sababu mtu akiwa na rafiki wanaendana wanaweza kukaa na wasichokane kwa sababu wana mambo mengi ya kushare

,ila mpenzi wako hamuwezi kukaa muda wote mkaongea mapenzi,that's why ni bora sana wanandoa wawe na urafiki kwa 85% then 15% ndio waingize hayo mapenzi as an emergency tu.

Ndio kuna misemo unasema

"Ndoa si mahusiano ya mume na mke katika mapenzi pekee,bali ni mahusino ya mume na mke katika mambo yote yahusuyo maisha"

Hivyo kila kinachohusu maisha basi wanandoa wanatakiwa kujadili suala hilo ikiwa mahusiano yao yana afya.

Juzi nilikuwa na wife tukawa tunajadili kuhusu ile clip ya fanta na mirinda,

leo tulikuwa tunajadili majibizano ya spika na ccm wenzie na sisi tukawa tunaweka mawazo yetu mimi na mke wangu,ni kuonesha tu kwamba tunajadili mambo yote yahusuyo maisha.

Umeupiga mwingi sana
 
Priorities changes over time

Sio upendo unaopungua ni priorities ndo inasababisha yote hayo.
 
Back
Top Bottom