Nimekuwa nikifatilia mijadala ya UKIMWI humu kwa muda mrefu na haya ninayotaka kuyasema humu yalishasemwa na mimi nimeyashuhudia siku chache zilizopita kwa majirani zangu.
Jirani yangu huyu aliugua sana na kulazwa, Dokta akaamuru aje na mke wake na watoto wote wapimwe (hapa nahisi alikuwa na mashaka ya ugonjwa).Wakafanyiwa vipimo wote ndio jamaa kugundulika ana VVU tayari, mke na watoto wakawa wapo salama wakaenda hadi hopitali ya mkoa majibu yakawa vilevile. Basi, mme akaendelea na matibabu na kupata nafuu na sasa hivi anaendelea na dozi.
Sasa navyoandika hapa ndoa ilishavunjika familia ya mwanamke ilimlazimisha aachane na jamaa asije akamwambukiza na mwanamke akafanya hivyo. Jamaa alipata maumivu mara mbili akataka ajiue kilichomsaidia ushauri mzuri kutoka kwa marafiki.
Swali. Je, inakuwaje wanandoa mmojawapo ameathirika na nwingine yupo salama? Huu ugonjwa una maswali mengi bila majibu.
Karibu wadau kwa hoja zenu.
MAONI YA WADAU:

Hapa ndipo penye mkanganyiko wa ajabu kuhuhu UKIMWI. Theory zinazoletwa na akina kimsboy na Deception ndiyo zinapata nguvu nakuonekana UKIMWI is Just a Myth tuloletewa na wazungu.
Kipimo kinapima uwepo wa Kinga (sijui ndiyo Serology) Mwilini na sio uwepo wa Virus, kwamba kinga zikipungua ndiyo mtu anaukimwi wakati hata Mgonjwa TB kinga pia zinapungua.
Inamaana hapo Baba alikua anaumwa so kinga lazima zipungue na kipimo lazima kitasoma positive, mke na watoto hawaumwi ndio maana walikua negative.
Kuna Msemo niliupata unasema
USIENDE KUPIMA UKIMWI WAKATI UNAUMWA HATA KAMA NI MAFUA