Maajabu ya trafiki Mombo korogwe kusimamisha magari kupisha msafara wa Waziri Mkuu

Babeli

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
6,659
3,233
JF,

Jambo Holi nalitoa ili traffic wetu wakati mwingine wawe wanatumia busara zaidi katika kufanya maamuzi.

Tukio limetokea maeneo ya kati ya Mombo na Korogwe ambapo magari ya kutoka Arusha Moshi yamesimamishwa kwa zaidi ya saa nzima sababu tu Waziri Mkuu yupo Lushoto kikazi. Sasa cha kuniuliza Mhe Waziri Mkuu yupo Lushoto.

Magari yote ambayo yamepita Mombo yanakaribia Korogwe yamesimamishwa kusubiri msafara wa WM. hii ni sahihi kweli..nadhan hata mwenyewe Wazir Mkuu akiambiwa situation hii atakasirika.

Askari wetu muwe mnaangalia mazingira msiwakosanishe viongozi wetu na wananchi. Wananchi walitegemea magari yote ambayo yalishapita yako mbali yaendelee na safari ili kusafisha njia na sio kukusanya magari yoote barabarani kitu ambacho ni risk kubwa sana.

Kiusalama zaidi barabara inatakiwa iwe nyeupe na sio iliyojaza magari na watu barabarani.

Nawasilisha maoni ya wengi wananchi walio katika jam hizo.
 
Lengo ni kuwapatieni ndugu wananchi fursa ya kuweza kuiona misafara ya viongozi wenu wapendwa.
 
Mkuu hii misafara tunashukuru siku hizi kadhia imehamia Dodoma.

Maana mwanzo huku kulikuwa vurugu tupu.
 
Mkuu hii misafara tunashukuru siku hizi kadhia imehamia Dodoma.

Maana mwanzo huku kulikuwa vurugu tupu.
Ya lengo Ni kuwakumbusha askari wetu wakati mwingine viongozi wetu hawapendi kuona wananchi wanateseka bila sababu..wajaribu kutumia busara na akili nyingi bila kuleta kadhia kwa wananchi .kwa pale kila mwananchi alilalamika kwa sababu walikuwa mbali mno na mkutano..the best and logic way Ni kuhakikisha waliokwisha pita mbele wanapotea na kuacha njia nyeupe kwa sababu magari yalisimama kwa zaidi ya saa nzima..
 
Back
Top Bottom