Maajabu ya Tanzania: Kumbe bomba la gesi linatumika kwa 6% tu na 94% halina kazi

Hii ni aibu kwa kukuwa bado Watanzania waliowengi wa kipato cha chini wanasumbuka mno na matatizo ya ukosefu wa mitaji, huduma za mbovu za afya na Elimu, ukosefu wa maji safi na tatizo la viongozi kuwalaghai kila uchaguzi ukifika. Halafu wao wamekazani na vitu visivyogusa maisha yao ya kila siku kuwekeza pesa nyingi. Ni aibu na uonevu kwa Binadamu. Ipo siku Mungu atasikia kilio cha wanyonge wasio na hatia. Mungu tunakuomba utusaidie sana waja wako dhidi utawala dhalimu!
Teeeeeeeeh teeeeeeeee teeeeeeeeeh alafu tunajisifu tumenunua ndege kwa keshiii na tutajenga tureeni kwa keshiiii
 
Hii ni aibu kwa kukuwa bado Watanzania waliowengi wa kipato cha chini wanasumbuka mno na matatizo ya ukosefu wa mitaji, huduma za mbovu za afya na Elimu, ukosefu wa maji safi na tatizo la viongozi kuwalaghai kila uchaguzi ukifika. Halafu wao wamekazani na vitu visivyogusa maisha yao ya kila siku kuwekeza pesa nyingi. Ni aibu na uonevu kwa Binadamu. Ipo siku Mungu atasikia kilio cha wanyonge wasio na hatia. Mungu tunakuomba utusaidie sana waja wako dhidi utawala dhalimu!
there is no God as you can imagine...ndo mana wajanja walishajua hilo toka miaka na miaka...ukipata gepu la maisha piga ...there is no judgement after what you do either wrongly or right way but only the universe does to you every thing through its law of Karma...".what goes around comes around"
meang that malipo ni hapa hapa duniani...
 
si
Kwa ufupi:
Bomba la gesi toka Mtwara hadi Dar ambalo limeigharimu serikali zaidi ya Tshs Trilion Mbili na nusu imebainika kwa zaidi ya 94% halina kazi.

Kwa mujibu wa report ya CAG inasema ni 6% za bomba hilo ghari zaidi Afrika mashariki ndio inafanya kazi huku ikighubikwa na ufisadi mkubwa.

Kwa lugha rahisi kuwa 94% ya bomba haitumiki.
Hints:
1. Bei ya watumiaji ni sawa ingawa watumiaji wako umbali tofauti.
2. Kutolipwa ankara za mauzo toka Tanesco kwenda TPDC
3. Utata kwenye mikataba ya mkopo
4. Kulipia gesi hata kama haijatumika (kama ilee ya IPTL)
5. Mkopo ulitarajiwa kulipwa kwa uuzwaji wa gesi lakini haifanyiki hivyo
6. Bomba limejengwa bila kujua au kutafta wateja ( yale yale ya ATCL hakuna business plan)
7. Kiasi kinachozalishwa ni kidogo kulipa mkopo
8. Mpaka sasa mteja pekee ni tanesco anyetumia futi za ujazo 46.61 badala ya 80 milioni kwa siku
9. Lengo ilikuwa kuuza viwandani, majumbani lakini haifanyiki hivyo hivyo ni underutilized
10. Tanesco inadaiwa USD million 61.35 na TPDC na hawajalipa mpaka leo
11. Hivyo deni linqzidi kuwa kubwa kwa kutolipa mkopo kwa wakati

HABARI KAMILI: CAG akosoa bomba la gesi



Other data:
UFISADI katika Mradi wa Bomba la Gesi: Serikali imechakachua bei(?)

si mlimshangilia
 
Hivi uyo JPM hakuwa waziri? Hakuepo kwenye baraza la mawaziri wanaojadili mikataba mikubwa kama hiyo? Hakua mbunge? Yeye sindio alikua anaongoza kwa kupiga meza kule bungeni wakati upinzani wakilalamikia huo mradi? Yeye sindio alikua waziri wa wizara ya ujenzi?
Aisee... sikujua hili, kumbe mawaziri na Raisi wanafanana ktk maamuzi serikalini. Yaani waziri ana mamlaka sawa na Raisi? Sasa kwa nini hivi sasa lawama za utendaji serikalini anapewa Magufuli badala ya mawaziri? Kumbe wanamuonea aisee....
 
Elimu inatakiwa itumike sambamba na akili ya kuzaliwa (common sense).
Elimu ya kukariri darasani ikiwekwa mbele sana (kwa sababu ya ulimbukeni tu) kuna madhara.
 
Prof aliondolewa awamu iliyopita, na karudishwa awamu hii, alidai yete ndie mtaalamu wa maswala haya. Nchi hii!
 
Gas ni compressive fluid, najaribu kuwaza...inawezeka vipi isafiri kwenye bomba kwa 6% cross section area ya bomba hilo!? Hapa naomba nguli wa mambo hayo anisaidie.
Jamaa una swali zuri sana. Ni kwamba kinachoongelewa ni uwezo wa bomba kupitisha certain amount of gas (in volume), na sio cross section ya bomba times length ( V=Area × Length). Design capacity ya bomba ikiwa 1000mmscfd na ukapitisha 80mmscfd bado gesi itajaa kwenye bomba ( kwa sababu ni compressible) lakini ni under-capacity. I hope umenielewa
 
Huyu si ei ji huyu, kabakiza siku chache sana ofisini..... kwani mazuri hayaoni mbona madudu tu kila kona ndo anataka kutuambia nyumba imegoma kusafishika? au wanatumia mbinu mbovu kusafisha?
 
Hata magufuli alikuwepo kwenye baraza la mawaziri so na yeye ni muhusika tena mkubwa tu!! mwache msoga airline atulie, magufuli aseme huu ufisadi umetokeaje!

Alikuwepo ndio ila nani alikuwa muamuzi wa awamu hiyo? Na ukiambiwa ushauri wake na wengine walioitakia nchi yetu mazuri haukusikilizwa utasemaje hapo?

Ukimuona anavyowajibika anaonyesha mengi aliyaona ila ni kuwa Raisi tu ndio angepambana nayo, na hapa kazi tu inazidi kupaaaaa.
 
Alikuwepo ndio ila nani alikuwa muamuzi wa awamu hiyo? Na ukiambiwa ushauri wake na wengine walioitakia nchi yetu mazuri haukusikilizwa utasemaje hapo?

Ukimuona anavyowajibika anaonyesha mengi aliyaona ila ni kuwa Raisi tu ndio angepambana nayo, na hapa kazi tu inazidi kupaaaaa.
Yeye si alikua mbunge??
Mbona hatukumsikia bungeni akiwa anatetea huu ujinga usifanyalike??
 
Huu mkataba ni wa kifisadi ambao Tanzania hatukustahili kuwanao. Waliosaini kwanini wasipandishwe kizimbani kwa kuingiza walipa kodi kwenye mkataba wa kifisadi!?

CAG akosoa bomba la gesi
www.ippmedia.com/sw/habari/cag-akosoa-bomba-la-gesi-0

CAG, Prof. Mussa Assad, katika ripoti yake alisema matumizi ya bomba hilo yapo chini ya kiwango na wateja wa gesi asilia hulipa bei inayofanana ilihali wapo umbali tofauti.

Mengine ni kutokulipwa kwa ankara za mauzo ya gesi asilia kutoka Shirika la Umeme (Tanesco) kwenda Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), kuwapo kwa kipengele cha mkataba wa mkopo kisichoridhisha na tofauti ya bei ya gesi kwa wauzaji wa gesi kwa Tanesco.

Pia, CAG amegundua mapungufu ya mifumo ya usalama katika kituo cha kinyerezi, mikataba ya uuzaji wa gesi yenye kipengele cha serikali kulipia gesi hata kama haijatumia gesi hiyo na mgogoro usio na ufumbuzi wa bei ya mabaki yaliyotokana na uzalishaji wa gesi.

Katika ripoti hiyo, CAG alisema bomba hilo lilijengwa na kampuni ya maendeleo ya petroli na Teknolojia China (CPTDC) kwa gharama ya dola za kimarekani bilioni 1.283 ambapo kati ya hizo, dola za Kimarekani bilioni 1.225 zilipatikana kama mkopo wa masharti nafuu kutoka benki ya Exim ya China.

Alibainisha marejesho ya fedha za mkopo huo yalitegemea kupatikana kwenye mauzo ya gesi asilia baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa bomba na kuanza kutumika kibiashara.

Prof. Assad alisema katika mapitio ya mkataba wa mikopo, hata hivyo, amebaini bomba hilo lilijengwa kabla ya kutafuta wateja.

Alisema mapungufu hayo yanaathiri malipo ya mkopo kwa vile mauzo halisi ya gesi asilia yatakuwa chini ya kiwango cha makadirio ya awali cha futi za ujazo milioni 138.8 kwa siku.

Pamoja na hayo, CAG alisema kwasasa Tanesco ndiyo mteja pekee wa gesi ambapo anatumia wastani wa futi za ujazo milioni 46.61 kwa siku ambapo makubaliano yalikuwa ni kutumia futi za ujazo milioni 80 kwa siku.

“Nashauri jitihada zaidi ziongezwe katika kuhakikisha wateja zaidi wa gesi asilia wanapatikana ili mkopo uweze kulipwa kabla ya marekebisho ya ulipaji ambayo yataongeza gharama kubwa kwa serikali,” alisema Prof. Assad.

CHINI ASILIMIA 94

Aidha, Prof. Assad alisema matumizi ya bomba hilo yapo chini ya kiwango kwa asilimia 94 kwa sababu lilijengwa ili kuwezesha usafirishaji wa gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme, viwandani, kupikia majumbani na kwenye magari.

Katika mapitio ya CAG, aligundua ingawa gesi ilikusudiwa kuwa na matumizi mengi, Tanesco ndiyo mteja pekee aliyeunganishwa kwenye bomba hilo na anatumia asilimia sita.

“Kiasi hicho ni pungufu futi za ujazo milioni 737.39 kwa siku ili kujaza bomba," anasema CAG katika ripoti. "Hii ni tofauti na mkataba wa mauziano na Tanesco inatumia gesi kwenye mitambo sita ya uzalishaji umeme.”

Alishauri TPDC iwasiliane na Tanesco na Wizara ya Nishati na Madini ili wajadiliane ni namna gani mitambo ya uzalishaji umeme ya Tanesco itaweza kumalizika kwa wakati ili bomba la gesi litumike kwa ufanisi na kuweza kulipa mkopo wa bomba hilo kutoka benki ya Exim ya China kwa wakati.

CAG pia alitaka nguvu zaidi zielekezwe kutafuta wateja zaidi wa gesi asilia ili kuongeza mapato ya gesi na kuiwezesha TPDC kutimiza wajibu wa kulipa madeni inapostahili.

Aidha, CAG alisema kutoza bei ya gesi inayolingana kwa wateja wa gesi asilia waliopo Dar es salaam na waliopo jirani na chanzo cha gesi sio njia sahihi ya kuhamasisha upatikanaji zaidi wa wateja.

Prof. Assad alishauri TPDC kuandaa rasimu ya bei ya gesi itakayotofautisha bei za gesi zitakazokuwa zikilipwa na wateja mbalimbali kulingana na umbali kutoka chanzo cha gesi.

CAG alibainisha Tanesco haijailipa TPDC kiasi cha dola za Kimarekani milioni 61.35 za ankra ya mauzo ya gesi asilia.

Alisema TPDC na Tanesco walikubaliana serikali iweke dhamana benki kiasi kinachoweza kulipa mauzo ya gesi kwa miezi mitatu au zaidi kwa ajili ya TPDC na dhamana hiyo iwepo hadi pale Tanesco itakapolipa madeni yanayohusu mauziano ya gesi hiyo.

“Serikali haijaweza kuweka dhamana hiyo, (na) hadi Desemba 2016 jumla ya deni la mauzo kiasi cha dola za kimarekani milioni 61.35 sawa na Sh. bilioni 133.4 kilikuwa kimelimbikizwa bila kulipwa na Tanesco,” alisema.

Alisema hali ya kuchelewa kuilipa TPDC inasababisha TPDC kuchelewa kuyalipa makampuni yanayouza gesi na hivyo kuongeza hali ya sintofahamu kwenye ulipaji wa mkopo wa benki ya Exim ya China.

Kadhalika, alisema kuchelewa huko kwa malipo kunaweza kusababisha gharama zaidi za riba ambayo itatakiwa kulipwa na TPDC kwa wadai wake na kushauri TPDC iandae mpango wa kufanya malipo kwa wauzaji wa gesi na mkopo kutoka benki hiyo ili kuepuka riba kubwa.
 
Back
Top Bottom