Maajabu ya Tanzania: Kumbe bomba la gesi linatumika kwa 6% tu na 94% halina kazi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,883
Nipashe.jpg
Kwa ufupi:
Bomba la gesi toka Mtwara hadi Dar ambalo limeigharimu serikali zaidi ya Tshs Trilion Mbili na nusu imebainika kwa zaidi ya 94% halina kazi.

Kwa mujibu wa report ya CAG inasema ni 6% za bomba hilo ghari zaidi Afrika mashariki ndio inafanya kazi huku ikighubikwa na ufisadi mkubwa.

Kwa lugha rahisi kuwa 94% ya bomba haitumiki.
Hints:
1. Bei ya watumiaji ni sawa ingawa watumiaji wako umbali tofauti.
2. Kutolipwa ankara za mauzo toka Tanesco kwenda TPDC
3. Utata kwenye mikataba ya mkopo
4. Kulipia gesi hata kama haijatumika (kama ilee ya IPTL)
5. Mkopo ulitarajiwa kulipwa kwa uuzwaji wa gesi lakini haifanyiki hivyo
6. Bomba limejengwa bila kujua au kutafta wateja ( yale yale ya ATCL hakuna business plan)
7. Kiasi kinachozalishwa ni kidogo kulipa mkopo
8. Mpaka sasa mteja pekee ni tanesco anyetumia futi za ujazo 46.61 badala ya 80 milioni kwa siku
9. Lengo ilikuwa kuuza viwandani, majumbani lakini haifanyiki hivyo hivyo ni underutilized
10. Tanesco inadaiwa USD million 61.35 na TPDC na hawajalipa mpaka leo
11. Hivyo deni linqzidi kuwa kubwa kwa kutolipa mkopo kwa wakati

HABARI KAMILI: CAG akosoa bomba la gesi

Other data:
UFISADI katika Mradi wa Bomba la Gesi: Serikali imechakachua bei(?)
 
Hii ni aibu kwa kukuwa bado Watanzania waliowengi wa kipato cha chini wanasumbuka mno na matatizo ya ukosefu wa mitaji, huduma za mbovu za afya na Elimu, ukosefu wa maji safi na tatizo la viongozi kuwalaghai kila uchaguzi ukifika. Halafu wao wamekazani na vitu visivyogusa maisha yao ya kila siku kuwekeza pesa nyingi. Ni aibu na uonevu kwa Binadamu. Ipo siku Mungu atasikia kilio cha wanyonge wasio na hatia. Mungu tunakuomba utusaidie sana waja wako dhidi utawala dhalimu!
 
Ni utawala wa awamu ya 4, na aliambiwa plant iwe kule kule Mtwara lakini Mkwe Marwa angepata wapi cha juu? Inasikitisha na inahuzunisha mbele ya macho ya Mola kuona watu wanammis jk, angetumaliza huyu mtu! Mwenye Enzi Mungu ametuhurumia sana sana na ametupa upendeleo wa hali ya juu kutuletea rais wetu JPM!
 
Ndiyo tatizo za nchi zetu, miradi mingi haina faida kwa nchi kama hili bomba pamoja na gesi ipo nchini kusini mwa Tanzania, ununuzi wa ndege za ATCL, kuhamia makao makuu Dodoma 2017, Kiwanja kipya cha ndege cha kimataifa, mikataba mibovu ..... listi ndefu ya miradi ya gharama kubwa bila kwanza kuangalia hali halisi
CAG Report madini, bomba la gesi Mtwara -DSM, PANAFRICA ENERGY, TPDC, STAMICO taarifa inaliza ukiisikia, sikiliza mwenyewe
 
Back
Top Bottom