Maajabu ya simulizi za kitabu kitakatifu cha biblia

Kuna siku Elisha aliwahi kuzungukwa na maadui wa mfalme mwingine ambaye alikuwa hasimu wake na mfalme wa Israel. Mfalme huyo alimvamia Elisha ili amuue, baada ya kuwa adui huyo kuwa anapanga mbinu za kwenda kumvamia mfalme wa Isrel, halafu kabla hawajafanya hivyo mfalme wa Israeli akawa anapata taarifa za maadui hao hata kabla hawajaenda kumvamia, na kazi hiyo ya kumjulisha taarifa hizo mfalme wa Isrel baadaye kuja kubainika kuwa ilikuwa inafanywa na nabii Elisha. Kwa hiyo kilichotokea baada ya hapo ni hawa madui kumfuata Elisha ili wakammalize kwanza yeye, halafu baada ya hapo ndiyo wakamvamie mfalme wa Israel. Walipowasili kwenye makazi ya Elisha, Elisha akawatia upofu wote halafu akaanza kuwaongoza njia kwenda kwenye himaya ya mfalme wa Israel. Walipofika huko akawafungua macho na kujikuta wako mateka tayari kwa mfalme wa Israel. Alichofanya mfalme baada ya hapo ni kuwapa chakula na maji, wakala wakanywa halafu baadaye akwaachia huru, hakuwaua.
Cha muhimu unachotakiwa kujua kuhusu Elisha ni kwamba wakati wanaachana na Eliya, wakati alipochukuliwa na gari la moto kwenda mbinguni, Elisha aliachiwa roho ya Eliya kwa kiwango cha mara mbili, yaani Eliya alimwachia Elisha roho yenye uwezo mara mbili ya ile aliyokuwa nayo yeye Eliya, na kutokana na hilo, Elisha alifanya miujiza mingi mara mbili zaidi ya miujiza aliyowahi kuifanya Eliya, ila nguvu ya kufanya miujiza hiyo aliipta kutoka kwenye roho ya Eliya!
Lete maneno
 
Elisha si alikuwa kipofu?
Hakuwa kipofu,,alukuwa ni kipara,siku moja akipita sehemu watoto wanacheza wakaanza kumzomea,"huyo kipara,huyo mzee kipara"
Mungu wa israel kusikua hivyo,nabii wake anazomewa,ghadhabu ikampanda,,wakatumwa fisi watatu,wakawararua raruwa wale watoto,,na huo ukawa ndo mwisho wao..
 
Swali la nyongeza; ikiwa Elisha aliachiwa baadhi ya nguvu au roho ya Eliya hii inamaanisha roho ya eliya haikuenda mbinguni? au iligawanyika nakuendelea kuishi kote duniani na mbinguni?
Je, kama ndivyo kuwa roho hii iliendelea kuishi kotekote basi eliya alijipa sifa sawa na ile ya Mungu kuwepo pote kwa muda mmoja? Je, hii inaruhusiwa kwa mwanadamu kuvaa uhusika au nguvu anazopaswa kuwa nazo muumba tu nakuwapa thawabu au kipawa wanadamu wenzake?
 
COSMOLOGY ina sound sanaa ndugu zanguu!! Universal laws zinasound sanaa matrix ndo usiseme. su Haya ndo mafundisho ya kisetani kama ilivyo andikwa kwa timoteo.
Timotheo ngapi ili tupate rejea? pia naomba uelezee kidogo japo brief tupate concept ya uhusiano uliopo kati ya hizo practise ulizozitaja na ushetani.
 
Swali la nyongeza; ikiwa Elisha aliachiwa baadhi ya nguvu au roho ya Eliya hii inamaanisha roho ya eliya haikuenda mbinguni? au iligawanyika nakuendelea kuishi kote duniani na mbinguni?
Je, kama ndivyo kuwa roho hii iliendelea kuishi kotekote basi eliya alijipa sifa sawa na ile ya Mungu kuwepo pote kwa muda mmoja? Je, hii inaruhusiwa kwa mwanadamu kuvaa uhusika au nguvu anazopaswa kuwa nazo muumba tu nakuwapa thawabu au kipawa wanadamu wenzake?
Roho sio nafsi. Usijichanganye.

Kila mwanadamu ana roho, aliyopewa na Mungu. Ndio connection tunayoitumia kwenye mengi, na nguvu yake (katika ibada au maombi) inatuunganisha na Mungu. Hii ndio inayobeba hazina na talanta zote ulizonazo, naturally, automatic. Inahitaji iungane na nafsi yako tuu ili ufanye maajabu unayotakiwa kuyafanya duniani. So, unapokufa, mwili unajitenga na nafsi na roho inaenda mbinguni.

Sasa nafsi ndio inayoenda kuzimu, na baadae mahala pa kupumzikia. Ikisubiri hukumu.

Kwa mfano wa eliya, inaonesha wazi kuwa Elisha amepata roho ya eliya yenye nguvu mara mbili (huku Elia akipaa mbinguni na Mwili na nafsi na roho kama kawaida.

Hii inamaanisha, roho inaweza kuji-duplicate mara nyingi iwezekanavyo endapo ukipata elimu sahihi. Mf. Unapotunga mimba, Reproduction inafanya kazi kwa mfumo maalum wa roho yako kujiduplicate pamoja na ya mwenza wako, na kupata mtoto mwenye roho mbili Ilizoungana, ya kwako na mwenzako.

So, it's possible kwa Nabii Eliya kupata huo uweza aliotunukiwa na Mungu na kumbariki Elisha kwa muda ule.
 
Mwanao akirithi tabia zako, wewe unabaki huna tabia? Mwanao akifanana na wewe kwa sura, wewe unabaki huna sura, au unakuwa unaishi in multiple places? Roho ya binadamu siyo maembe kwamba ukimpatia mwenzako embe moja kama ulikuwa nayo mawili basi unabaki na embe moja, hapana. Kwenye ulimwengu wa roho vitu havigawanyiki kama ilivyo kwenye ulimwengu wa mwili isipokuwa division or minus, means multiplication or addition. Inaonekana huna tabia ya kusoma Maandiko Matakatifu. Nakutia moyo uwe unayasoma mara kwa mara, na baada ya hapo, uwe unapata muda wa kuyatafakari
 
Roho sio nafsi. Usijichanganye.

Kila mwanadamu ana roho, aliyopewa na Mungu. Ndio connection tunayoitumia kwenye mengi, na nguvu yake (katika ibada au maombi) inatuunganisha na Mungu. Hii ndio inayobeba hazina na talanta zote ulizonazo, naturally, automatic. Inahitaji iungane na nafsi yako tuu ili ufanye maajabu unayotakiwa kuyafanya duniani. So, unapokufa, mwili unajitenga na nafsi na roho inaenda mbinguni.

Sasa nafsi ndio inayoenda kuzimu, na baadae mahala pa kupumzikia. Ikisubiri hukumu.

Kwa mfano wa eliya, inaonesha wazi kuwa Elisha amepata roho ya eliya yenye nguvu mara mbili (huku Elia akipaa mbinguni na Mwili na nafsi na roho kama kawaida.

Hii inamaanisha, roho inaweza kuji-duplicate mara nyingi iwezekanavyo endapo ukipata elimu sahihi. Mf. Unapotunga mimba, Reproduction inafanya kazi kwa mfumo maalum wa roho yako kujiduplicate pamoja na ya mwenza wako, na kupata mtoto mwenye roho mbili Ilizoungana, ya kwako na mwenzako.

So, it's possible kwa Nabii Eliya kupata huo uweza aliotunukiwa na Mungu na kumbariki Elisha kwa muda ule.
Biblia inakataa na wala haijawahi kusema juu ya uwepo wa roho kwenda mbinguni au popote pale au maisha mengine yakiroho au nafsi baada ya kufa, mtu aliyekufa atambui chochote ukaa kaburini akisubiri siku ile ya ufufuo, hili unalizungumziaje?
 
Naomba kuzungumzia mfanano wa visa vya biblia takatifu na jinsi ambayo havipishani katika kusudio la ujumbe na maana licha ya stori na wahusika kuwa tofauti ila kinachowasilishwa huwa ni kile kile, hivyo nitaandika summary tu ukitaka kuchimba zaidi utaenda kujisomea kulinganisha nakuja na majibu au mtizamo wako:-

Kisa cha anguko la adamu na hawa katika bustani ya edeni+ kisa cha samsoni na delila,sulemani na wanawake wa mataifa, n.k

(Ufanano = kushawishika,kutenda dhambi,kuanguka/mauti)

Kisa cha kaini kumuua nduguye abel kisa wivu+kisa cha daudi kumuonea wivu uria nakumuua kisha kumuoa bethisheba+kisa cha lameck na wake zake(kuua mtu)+kisa cha tamari na wivu wa kaka zake kulipiza kisasi+nakadhalika.
(Ufanano= laana,hatia,majuto)

Kisa cha yona kuagizwa ahende Ninawi nakuukomboa mji ule+ kisa cha kuja kwa yesu kuukomboa ulimwengu+ kisa cha yohana mbatizaji+kisa cha stephano+kisa cha wanafunzi wa yesu. (Ufanano=ukombozi,kukataliwa,kufa kwa hatia ya wengine,kukamilisha mission,kujua yatakayo tokea,kuurithi ufalme wa mbinguni)

Kisa cha nabii eliya +kisa cha musa katika mission yao

(Ufanano=hawakuonja mauti,walithibitisha uwezo wa nguvu ya Mungu,walizaliwa na wanadamu kama sisi,walihisi hawawezi kuyakabili majukumu makubwa wanayopewa,waliwasiliana na mungu wao,waliishi maisha matakatifu na utii wa sheria za mungu,walilishwa,kuhifadhiwa na mungu,walitenda miujiza n.k)

Kisa cha ibrahimu kuama nakwenda kuanzisha taifa jipya+kisa cha Noah na gharika kuu+yoseph na nduguze+kisa cha lutu na wanawe.

(Yaliyomo=kuokoa kizazi nakukiendeleza,kutoswa na watu au kutoaminika mwanzo,kuwa na imani thabiti,n.k)

Kisa cha Paulo kuua waliomwabudu mungu nabaadae kutokewa na yesu nakuokoka+ kisa cha nebukadneza kumrudia mungu nakusamehewa+kisa cha yona na watu wa Ninawi+kisa cha mwanamke kahaba kusamehewa dhambi na yesu,n.k

(Ufanano=kutenda maasi au kuanguka dhambini kiasi chakutoweza kusameheka,kujikosoa nakutubu,kusamehewa dhambi zao,kuwa kielelezo chema cha kusambaza habari njema za Mungu n.k)

Siwezi maliza ufanano huu wa visa hivi ndani ya simulizi hizi na jumbe zake pia, ambazo lengo lake kuu ni moja na stori kuu ni moja pia ikisimuliwa kwa mifano tofauti tofauti, hivyo nipe mtizamo wako wewe wakifiria nini juu ya hili.
Ulipoandika ahende ninawi ndo nikaacha kusoma. AHENDE?????
 
Kumbukumbu la Torati 34,

5 Basi Musa, mtumishi wa Bwana, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kwa neno la Bwana.

6 Akamzika bondeni, katika nchi ya Moabu, kukabili Beth-peori; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo”.

Musa alikufa akafufuka (Yuda 1:9); na hata hivyo Musa hakuzikwa na mtu ye yote, Eliya alipaa, Yesu alifufuka kwanza ndipo akapaa. Hakuna mtu aliyekufa akazikwa harafu akaenda mbinguni bila kufufuka kwanza.
Elijah na Enoch ni hawa tu ndio waliopaa mbinguni moja kwa moja
 
Mimi nina swali na naomba majibu yake, hivi kwanini mapadri wa Roman Catholic hawarusiwi kuoa

Nje ya mada

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani ni hawaruhusiwi au wao wenyewe ndio waliamua kuwa watawa?

Ile ni Optional na aliyetoa hiyo option ni Paulo kwakuwa nae hakuoa na alikuwa towashi.

Sidhani kama kuna mahala Biblia inamkataza Mwanaume kuoa.
 
Kumbukumbu la Torati 34,

5 Basi Musa, mtumishi wa Bwana, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kwa neno la Bwana.

6 Akamzika bondeni, katika nchi ya Moabu, kukabili Beth-peori; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo”.

Musa alikufa akafufuka (Yuda 1:9); na hata hivyo Musa hakuzikwa na mtu ye yote, Eliya alipaa, Yesu alifufuka kwanza ndipo akapaa. Hakuna mtu aliyekufa akazikwa harafu akaenda mbinguni bila kufufuka kwanza.
Yuda 1:9 Hata mikaeli, malaika mkuu hakufanya hivyo. Katika ule ubishi kati yake na ibilisi juu ya mwili wa musa, mikaeli hakuthubutu kumhukumu ibilisi kwa matusi, ila alisema; Bwana mwenyewe na akukaripie"

Ufafanuzi juu ya kifungu hiki katika lugha ya picha; hapa kinachojaribu kuoneshwa ni katika nyakati zile za mwisho ambapo waliyowake Mwenyezi Mungu yaani ambao walitimiza kadri ya sheria yake watakavyonyakuliwa(Eliya) na wale waliotereza/watenda dhambi(musa alipomuua mmisri,alipoagizwa na Mungu alikuwa mbishi, alijivuna alipoupiga mwamba na fimbo hili utoe maji n.k)

kwa kitendo hiki tiyari musa ni kiwakilishi cha wale ambao shetani atajaribu kuwapokonya kutoka mikononi mwa bwana kwa kigezo cha kuwa ni watu wake naye mwenyezi Mungu atawatetea mwenyewe kuwa walitubu nakuziacha njia zao ovu nakumfata(ndiyo maana malaika mkuu ajamkanya kwa maana shetani hapa anamadai ya msingi na haki ya kusikilizwa na mwenye maamuzi kamili ni mmiliki wa vitu vyote) hivyo atamkemea lucifa asiwaguse watu wake,

Kwanini anayo haki ya kumshinda na kumkemea shetani ni kwa maana ya ondoleo la dhambi na upatanishi wa Mwenyezi Mungu na watu wake waliokwisha angukia dhambini iliyofanywa na yesu kristo kupitia damu yake iliyomwagika msalabani ilikuwa upatanisho na ondoleo la dhambi kwa niaba ya wakosaji wote(binadamu wote walikwishakuwa na hatia sawa na shetani) hivyo walistahili kufa au kunywa kikombe kimoja cha ghadhabu ya Mungu pamoja na shetani.

"Kwa maana hiyo Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanaye wa pekee kama sadaka kwa ondoleo la dhambi zetu"

Ila kwa kufa kwake Yesu kwa niaba yetu kuliondosha ile dhambi iliyotutia hatiani sote nakumpa shetani haki yakumtaka Mwenyezi Mungu kuhukumu dunia nzima kwa haki kwa kuwahukumu wote waliopotoka na waliofata njia zake,

kwa sababu hii Yesu kristo akapewa mission yakuleta habari ya wokovu na uzima. Hili yeyote yule asikiaye na kutenda kwa kadri ya mapenzi yake muumba asipate kudhurika na wala kuhukumiwa sawa na shetani nyakati za mwisho wake zitakapotimia.

Ndiyo maana ya taswira ya uwepo wa utatu yaani;
+ Yesu kristo(upendo)=Mfano wa nafsi ya Baba(utenda kwa mamlaka kuu, ndiye mrithi wa kiti cha enzi, maombi yote upitia kwake,utoa hukumu,ubariki na kusamehe)

+Musa(mkombozi)=Mfano wa Nafsi ya Mwana/yesu (alitumwa kuwakomboa wanaisraeli, akatenda miujiza nakuponya kwa uwezo wake Mungu aliyempa mamlaka na akafanikiwa kuwakomboa toka utumwani(sawa na dhambini)wana Israeli(wanadamu wote) akakamilisha sheria za Mungu,akatoa maagizo ya Mungu(torati) nakuongoza watu wake kuenenda katika unyoofu nakufika nchi ya ahadi(uzima),alikufa akazikwa,akapiganiwa na malaika kwa kuwa yu haki akayashinda mauti akafufuka nakupaa mbinguni)

+Eliya(mnyoofu aliyenyakuliwa)=Mfano wa Nafsi ya Roho Mtakatifu(alitumwa kuthibitisha juu ya uwepo wa nguvu ya Mungu na kuwatia moyo na imani wale wote waliomwamini Mungu nakuaribu nguvu za uovu, ni kielelezo cha namna ya kuishi maisha matakatifu na zawadi yake ni kupata uzima nakwenda kuurithi ufalme wa mbingu pasipo adhabu ya mauti).
 
Hakuwa kipofu,,alukuwa ni kipara,siku moja akipita sehemu watoto wanacheza wakaanza kumzomea,"huyo kipara,huyo mzee kipara"
Mungu wa israel kusikua hivyo,nabii wake anazomewa,ghadhabu ikampanda,,wakatumwa fisi watatu,wakawararua raruwa wale watoto,,na huo ukawa ndo mwisho wao..
uyo atakuwa alikuwa shetani watoto kumtania tu atume fisi kuwaua.nipe iyo aya.
 
Why did Elisha kill the children?​

Names & Places

In 2 Kings 2, Elisha is confronted by a group of children mocking him, so he killed them. His response seems so excessive. Why didn't he forgive or just ignore them?
2wafalme 2:23-25
 
Hakuwa kipofu,,alukuwa ni kipara,siku moja akipita sehemu watoto wanacheza wakaanza kumzomea,"huyo kipara,huyo mzee kipara"
Mungu wa israel kusikua hivyo,nabii wake anazomewa,ghadhabu ikampanda,,wakatumwa fisi watatu,wakawararua raruwa wale watoto,,na huo ukawa ndo mwisho wao..
Mungu anararura vijitoto innocent ,kweli Mungu ana upendo mkuu
 
Why did Elisha kill the children?​

Names & Places

In 2 Kings 2, Elisha is confronted by a group of children mocking him, so he killed them. His response seems so excessive. Why didn't he forgive or just ignore them?
2wafalme 2:23-25
(2 Wafalme 2:23-24) 23 Akakwea kutoka huko mpaka Betheli naye alipokuwa akienda njiani, wakatoka vijana katika mji, wakamfanyizia mzaha, wakamwambia, paa wewe mwenye upaa! paa wewe mwenye upaa!

24 Akatazama nyuma akawaona, akawalaani kwa jina la Bwana, wakatoka dubu wawili wa like mwituni, wakawararua vijana arobaini na wawili miongoni mwao.

Alichokumbana nacho hapa Elisha kilikuwa ni kikwazo ambacho ni fedheha kutoka kwa vijana wale na yeye kama mzee asingepambana na umati wa watu isipokuwa aliwalaani na kwa kuwa alikuwa upande wa haki ombi lake likajibiwa. Hivyo uwezi ruhusu kukwamishwa na waovu kwa kuihurumia dhambi.

(Mathayo 18:7-8) 7 Ole wake ulimwengu kwa sababu ya vikwazo vinavyowaangusha wengine. Vikwazo hivyo ni lazima vitokee lakini ole wake yule atakayevisababisha.

8 Kama mkono au mguu wako ukikukosesha ukate. Afadhali kwako kuingia katika uhai bila mkono au mguu,kuliko kutupwa katika moto wa milele ukiwa na miguu yako miwili.
 
Back
Top Bottom