Maajabu ya siasa za Tanzania, CCM ikijiimarisha kuendelea kushika dola. Vyama vya Upinzani vinapambana visife

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
Hii ndio hali halisi ya siasa hapa nchini ,vyama vya upinzani vimesalimu amri mbele ya CCM. Kujua hili chunguzeni vyama hivyo ,havina mvuto, havina wagombea madhubuti wa kumtikisa Magufuli,kila kimoja kinajaribu kuwa zaidi ya kingine na si kushika dola.

Chadema ambacho ndio kilionekana kina uthubutu , kwa sasa kinapambana angalau kipate hata mbunge mmoja tu,

Vyama hivi visitafute mchawi ,wachawi ni viongozi na baadhi ya wanachama wao,ambao wapo kimaslahi zaidi na si kuwatumikia wananchi, badala ya kusambaa na kuanzisha mashina na matawi vijijin, vimejikita mijini na mitandaoni kufanya siasa za matukio na kudeal na personalities za mahasimu wao badala ya kunadi Sera, kiukweli mijini wapiga kura ni wachache na wengi wao huwa hawajiandikishagi wala hawapigagi kura.

CCM imejikita vijijini ambapo wapiga kura ndio wengi. Mfano, angalia wagombea wao ni wale wanaotemwa na CCM, vyama hivi haviandai viongozi madhubuti kwa ajili ya kushika dola, waliopo ubunifu ni zero ,hawatakia kuachia nafasi kupisha mawazo mapya ,wanahofia maslahi yao (ruzuku),ni vyama vya ruzuku. Wameandaa vijana mitandaoni kuwatetea kwa madhaifu walionayo.

Niwape pole wale wasiojua siri ya urembo wa vyama hivi,ambao hutokwa povu kitumwa. Namaliza kwa kusema ,wakati CCM inajiimarisha na kujizatiti kuendelea kuishikilia dola ,vyama vya upinzani vinapambana visife, au visishike mkia kwenye uchaguzi
 
Hakuna 'vyama' hapo, ni vikundi vya saccos ambavyo vimeua upinzani wa kweli Tanzania. CCM itaendelea kushika dola saaana tu.
 
Sijaisoma yote Ila kwa jinsi ulivyopanga ukweli nimekuelewa mno! Ila mMbulula watakutolea povu balaa! Vaa barakoa kabisa😂🤣😂!
 
HUU NI UKWELI AMBAO CHAMA AMBACHO KIMEJIVIKA UMALAIKA HAKITAKI KUUBALI.

Zaidi ya kushusha nondo walizofunzwa UFIPA mitusi iliyo jaa mafuta ya kitimoto.


Jana Leo... Kesho???? Ni ya MWENYEZI MUNGU.
 
Back
Top Bottom