Maajabu ya serikali ya CCM, Kiongozi wa Wilaya UVCCM ni Mtumishi wa Umma

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
140
1,000
Ninakishangaa sana chama ambacho ndicho kinatakiwa kua kinara katika kutii katiba ya nchi lakini kinafumbia na kukumbatia mambo ya ajabu kabisa.

Ni uvunjaji wa sheria na katiba ya nchi kuona kiongozi wa chama cha siasa tena mwenyekiti wa Wilaya kabisa bado ni mtumishi wa umma tena ni mkuu wa idara ya serikali. Hii siyo sawa na tunapaswa kukemea tabia kama hizi

Ndugu Ayubu Maandazi almaarufu kama Maandazi, mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Magu mkoani Mwanza ni mratibu Elimu kata anaendelea kupokea mshahara wa serikali huku ni kiongozi wa chama. Mtumishi wa aina hii atenda haki lini kwa watumishi wenzake wasiokua wana CCM?Je, katiba inaruhusu upuuzi kama huu?

Mtu unapokua kiongozi wa chama cha siasa unapaswa kua mtumishi wa umma? Huu siyo wizi ni kitu gani?

Tunaomba na kuvisihi vyombo vyetu vya kisheria kufuatilia jambo hili, nchi hii ni ya wote na hakuna aliye juu ya katiba.
 

promethus

JF-Expert Member
Feb 22, 2016
473
1,000
Mkuu mratibu elimu kata kuwa mkuu wa idara imeanza kuanzia lini?
Hebu nitoe tongotongo kidogo
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
31,289
2,000
Ati Mandazi
heh.png
 

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
300
1,000
Haya mambo aliendekeza Maheremu Magu na aliona haya ni sawa. Yaani kijana anakijua kua anavunja katiba ya nchi anapokea mshahara wa tumishi wa uma huku anakula posho za chama anajaza tumbo tu. Huu ni wizi kama wizi mwingine
 

balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
6,166
2,000
Mkuu mratibu elimu kata kuwa mkuu wa idara imeanza kuanzia lini?
Hebu nitoe tongotongo kidogo
Kuna uzi humu wa Maafisa Elimu Katq na Ukuu wa Idara
Hawa jamaa wanaaminika sana hadi kwenye Chama
Twende polepole tutaelewana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom