Maajabu ya Rais Samia

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
✓ Ameendeleza elimu bure tena idadi ya wanafunzi ikiongezeka hivyo kutumia takribani shilingi bilioni 26 kila mwezi badala ya shilingi bilioni 23

✓Anaendeleza miradi mikubwa ya kimkakati kwa kasi ya aina yake
¶ SGR Dar-Moro ipo mbioni kuanza
¶ SGR Moro-Makutopora Singida ujenzi unaendelea kwa kasi na ujenzi upo zaidi ya asilimia 70
¶ SGR Makutopora-Tabora mkandarasi amekwishapatikana na kusaini mkataba kwa sasa amekwishakabidhiwa eneo la mradi anaendelea na kazi
¶ SGR Mwanza-Isaka ujenzi umeanza
¶SGR Isaka-Tabora zabuni inakamilishwa taratibu muda wowote mkandarasi atapatikana

✓Mradi mkubwa wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Rufiji (Stieglers gorge) au JNHPP unaendelea vizuri na upo karibu asilimia 60 kwa sasa... utakamilika 2024

✓ Serikali ya CCM awamu ya sita anayoiongoza Rais Samia Suluhu Hassan imelipa shilingi bilioni 560 kama malipo ya awali ya ndege mpya tano kati yake moja ya mizigo. Ndege hizo ni aina ya Bombardier, Boeing Dreamliner na Airbus.

✓ Tangu Uhuru hospitali za umma kulikuwa na CT Scan 2 tu Rais Samia kupitia serikali anayoiongoza kaagiza 29 yaani kila hospitali ya rufaa ya mkoa itakuwa nayo. Wananchi wakigoma hawatafuata CT Scan Benjamin Mkapa Dodoma tena wataipata mkoani kwao...Kagera hawataifuata Bugando Mwanza wataipata mkoani kwao...

✓ Amejenga shule mpya za kata 214 katika kata ambazo hazikuwa na shule kabisa au miundombinu yake haikuwa inakidhi mahitaji. Shule hizi zinagharimu shilingi milioni 700 zipo kamili... Januari 2023 zinapokea wanafunzi. Shule hizi atajenga Elfu moja mpaka ifikapo 2025.

✓ Amejenga shule za wasichana kumi moja kwa kila mkoa za kidato cha 1-6 zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,000. Kila shule inajengwa kwa gharama ya shilingi bilioni tatu tayari ujenzi umeanza na upo hatua nzuri... shule hizi zitajengwa katika kila mkoa mpaka ifikapo 2025.

✓ Amejenga vituo vya afya 222 kwenye tarafa zilizokuwa hazina vituo vya afya kabisa tangu uhuru lengo mpaka 2025 tarafa zote ziwe na vituo vya afya huku ngazi ya kata nayo ikiendelea kufikiwa.

✓Ameongeza bajeti ya ujenzi wa barabara vijijini toka shilingi bilioni 267 hadi shilingi bilioni 966 ili miundombinu ya vijijini ipitike.

✓ Ameimarisha sana mahusiano ya nchi yetu na dunia kidiplomasia hali iliyoifungua sana nchi yetu kiuwekezaji na kibiashara.

✓ Uamuzi wake wa kuridhia chanjo ya Uviko-19 kumeifanya Nchi yetu kuondokewa kwenye orodha ya nchi hatari kutembelewa hali iliyoinua utalii wetu, imewapa nafuu wafanyabishara na wanafunzi waliokuwa wakisafiri Nchi jirani kuchoma chanjo...

✓ Ameongeza bajeti ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu toka shilingi bilioni 464 hadi shilingi bilioni 570.

✓Amesikika mara kadhaa akiitaka TRA ikusanye kodi kwa weledi na kuacha ubabe na mabavu bali wawe rafiki na wafanyabishara ili wastawi.

Huyu ndio Rais Samia Suluhu Hassan...hajasemei sana wala hana makuu.

Nitaendelea kuwaletea maajabu ya Rais wa awamu ya sita Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan..... Itaendelea.

%2B255%20738%20969%20820%2020220226_093149.jpg
 
Mtu yoyote anayemsifia mtu ambaye ameiingiza nchi kwenye madeni makubwa, inflation nk huku mtu huyo akisema kupanda kwa bei kunatokana na vita ya Ukraine 🇺🇦 na Russia 🇷🇺, na hataki kupeleka mwenge uletao amani ukakimbizwe Ukraine 🇺🇦 huwa simpatii jibu.

Je, ni kwamba huu mfumuko wa bei tunaupenda sana au mwenge wetu ni feki kabisa tukiupeleka Ukraine 🇺🇦 hautaweza kamwe kuleta amani, ila bongo tunautumia kuwanufaisha wajanja wachache?
 
Kama ni hivyo basi tubadilishe na jina la Nchi liwe "Nchi ya Maajabu"

Maana hayo maajabu naona hayaishi! Kila siku ni maajabu tu.
 
Yote ni kazi ya Magu, wizi na uporaji wa kazi ya mwingine is crime, ya kwake ni madrasa ya mkopo!
 
Mtu yoyote anayemsifia mtu ambaye ameiibgiza nchi kwenye madeni makubwa, inflation nk huku mtu huyo akisema kupanda kwa bei kunatokana na vita ya Ukraine na Russia , na hataki kupeleka mwenge uletao amani ukakimbizwe Ukraine huwa simpatii jibu.
Je ni kwamba huu mfumuko wa bei tunaupenda sana au mwenge wetu ni feki kabisa tukiupeleka Ukraine hautaweza kamwe kuleta amani, ila bongo tunautumia kuwanufaisha wajanja wachache?
Kwan n bongo tu mkuu mfumuko wa bei ya kilaa ktu umepanda ???kilaa ktu kinakuja na mabadiliko uwezi jua uruc na ukraen ktk uchumi wetu tunanufaika vp na ss majanga yametokea uwezi jua tuaadhirika vp km taifaaa,tozo ilikuja na tukapiga kelele na mwishowee tumezoea na miamalaa tunatuma km Kawa tena nayakutoleaa kbs,.MAISHA LZM YAENDELEEEE kwa stail yyt ilee....
 
Yote ni kazi ya Magu, wizi na uporaji wa kazi ya mwingine is crime, ya kwake ni madrasa ya mkopo!
Una msingiziaaa kablaa ya magu na baada ya magu ilishapangwa na MUNGU kuwa hv,hata ajee malaikaa atuongozee bado lawamaa hataachaa kupewaaa,safari n ndefu nchi inapitia matatizo ambayo hata ww unapitiaa kwenye maisha yakoo,tushukuru kwa yoteee mkuuu ingali tupo hai,
 
Mtu yoyote anayemsifia mtu ambaye ameiibgiza nchi kwenye madeni makubwa, inflation nk huku mtu huyo akisema kupanda kwa bei kunatokana na vita ya Ukraine 🇺🇦 na Russia 🇷🇺, na hataki kupeleka mwenge uletao amani ukakimbizwe Ukraine 🇺🇦 huwa simpatii jibu.
Je ni kwamba huu mfumuko wa bei tunaupenda sana au mwenge wetu ni feki kabisa tukiupeleka Ukraine 🇺🇦 hautaweza kamwe kuleta amani, ila bongo tunautumia kuwanufaisha wajanja wachache?
Lunyasi vipi Tena nani kakuchefua🏃
 
Upuuzi wa vijana wa CCM ndio huu, kusifia kuabudu hata kama hawaijui kesho Yao ipoje!!. Mtu mwenye akiri timamu hawezi kuandika uchafuu huu. Na yote haya akiyaanzisha jiwe kusifiwa na kuabudiwa hata katika wakati ambao anahitaji kusemwa ili abadilike. Poor CCM!!
 
Kwan n bongo tu mkuu mfumuko wa bei ya kilaa ktu umepanda ???kilaa ktu kinakuja na mabadiliko uwezi jua uruc na ukraen ktk uchumi wetu tunanufaika vp na ss majanga yametokea uwezi jua tuaadhirika vp km taifaaa,tozo ilikuja na tukapiga kelele na mwishowee tumezoea na miamalaa tunatuma km Kawa tena nayakutoleaa kbs,.MAISHA LZM YAENDELEEEE kwa stail yyt ilee....
Ili vita ikome maisha yarudi kawaida si mpeleke huo mwenge huko Ukraine 🇺🇦? Si huwa mnasema kwamba amani iliyopo Tanzania 🇹🇿 ni matokeo ya mbio za mwenge nchi nzima?

Sasa pelwkwni mwenge Ukraine 🇺🇦 tukaone efficiency ya mwenge kwenye kuleta amani acheni kuwafanya watu mazombi
 
Back
Top Bottom