Maajabu ya Ngorongoro: Gharama ya kumtunza Faru Fausta kwa mwezi ni Tshs.mil 64

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885

Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro imesema kuwa gharama za kumtunza na kumlisha faru Fausta ni TZS milioni 64 kwa mwezi.
 
64,000,000 *12=768,000,000 mara miaka kumi = 7,680,000,000.

Halafu huduma muhimu za kibinadamu nchini hazipatikani........

Bora huyo faru auliwe kuliko kutulisha hasara namna hii.

Bora wampeleke Sasakwa tulipwe mil 200 kama mme wake.
 
  • Thanks
Reactions: 911
64,000,000 *12=768,000,000 mara miaka kumi = 7,680,000,000.

Halafu huduma muhimu za kibinadamu nchini hazipatikani........

Bora huyo faru auliwe kuliko kutulisha hasara namna hii.
Kama huyo faru anaingiza 200M kwa mwezi why 64m asihudumiwe

Hizo muhimu za binaadamu zitatolewa kwa kodi zenu na njia zingine

Kwani mmeambiwa huyo faru anahudumiwa kwa kodi zenu?anahudumiwa na pesa inayoingia sababu ya uwepo wake
 
Labda wengine hatujui.......huyo Faru anaingizaje 200M?
 
  • Thanks
Reactions: 911
Watanzania tuanze kampeni nzito kuhakikisha. huyo Faru anauzwa nje au anauwawa kwa lazima ili tuokoe pesa zinazotumika kumtunza.

Kwa mahesabu rahisi kabisa, hizo milioni 64 kwa mwezi zinatosha kuwalipa mishahara wastani wa Walimu 120 wa shule za msingi au Sekondari kila mwezi hapa Tanzania AU Zingetosha kuwalipa zaidi ya Madaktari 60 kila mwezi kama mshahara.

[HASHTAG]#TumpotezeFaruFausta[/HASHTAG].
 
Mmh!tunalishwa matango pori labda mutuambie kuwa huyo faru anakunya midolari!
 
anatunzwa na serikali au mashirika ya wanyamapori duniani? maana sidhani kama serikali inaweza toa fedha hizo, wangefafanua hizo gharama zinatolewa na nani?
 
Huyo faru anaingiza shilingi ngapi kwa mwezi kama gharama ya kumtunza ipo hivyo
 
Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa Opportunity Cost! Watoa Maamuzi wasiopima opportunity cost mara nyingi wanaishia kuwa losers!!

Si ajabu endapo wangeandaa questionnaire na kuwauliza watalii wataje Top 5 ya mambo yaliyowasukuma kuja Tanzania si ajabu Faru Fausta asingetokea kwenye among Top 5 na hivyo ku-conclude tija ya hizo 64 million/month ni ndogo na busara ingepelekea kuwekeza hizo 64 million kule ambako kunawasukuma waje lakini kuna kasoro hizi na zile!

Anyway, inawezekana Faru Fausta ndie chanzo cha mvua kwenye kanda husika!!
 
is not about the money, ni endangered species mkuu, wamebaki wachache hivyo wanastahili care wasije potea kabisa, ila sidhani kama ni serikali wanatoa hizo fedha, kuna UNESCO,WWF na wengineo pengine ndio wanatoa hizo fedha
 
Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa Opportunity Cost! Watoa Maamuzi wasiopima opportunity cost mara nyingi wanaishia kuwa losers!!

Si ajabu endapo wangeandaa questionnaire na kuwauliza watalii wataje Top 5 ya mambo yaliyowasukuma kuja Tanzania si ajabu Faru Fausta asingetokea kwenye among Top 5 na hivyo ku-conclude tija ya hizo 64 million/month ni ndogo na busara ingepelekea kuwekeza hizo 64 million kule ambako kunawasukuma waje lakini kuna kasoro hizi na zile!

Anyway, inawezekana Faru Fausta ndie chanzo cha mvua kwenye kanda husika!!

is not about the money, ni endangered species mkuu, wamebaki wachache hivyo wanastahili care wasije potea kabisa, ila sidhani kama ni serikali wanatoa hizo fedha, kuna UNESCO,WWF na wengineo pengine ndio wanatoa hizo fedha
 
Kama huyo faru anaingiza 200M kwa mwezi why 64m asihudumiwe

Hizo muhimu za binaadamu zitatolewa kwa kodi zenu na njia zingine

Kwani mmeambiwa huyo faru anahudumiwa kwa kodi zenu?anahudumiwa na pesa inayoingia sababu ya uwepo wake
Aisee! Kumbe anaingiza pesa nyingi kiasi hicho!! Hebu tufafanulie hizo 200M zinaingia ingia vipi?! Ni kwamba hapo alipo watalii wanatozwa pesa kwenda kumwangilia au kuna watalii huwa wanakuja purposely kwa ajili ya Fausta au zinaingia ingia vipi hasa?!
 
Back
Top Bottom