Maajabu ya nafasi za kazi UDOM... Kuna nini hapa?

Siendi nimegairi maana itakua upotevu wa nauli ndio maana wanataka kuwapiga watu paper,kazi kweli kweli
 
bwana mbweta nakushauri uende tu u never know, ila nimejifunza nini kutokana hizo data? ni kwamba huko tunakoelekea hali itakuwa si shwari. inabidi serikali ifanye kila liwezalo kutengeneza ajira hizo figure zinatisha hapo bado graduates wa mwaka huu hawajaingia katika soko la ajira
 
Mimi nina rafiki yangu alituma maombi hapo UDOM kwenye nafasi ya Administrative officer,nilipoona haya majina nikagundua kuwa hizi ni siasa,nimemwambia asije tu maana anapoteza muda wake,hapo kuna udini na watu wanapeana kazi kwa ground za kidini sana...hiki kitu kinaniuma sana basi tu,watu watapoteza pesa zao kwa kitu ambacho hawatafanikiwa kabisa...kumbuka hapo kila mkubwa ana watu wake kama watano hivi...sasa wewe mkulima kama mimi utapigana kweli?

Una ushahidi?
 
kaka we inaonyesha sio wa bongo...hapo hamna haja ya kutangaza watu wengi hawana kazi yaani baada ya mwaka tutakuwa kama matapeli waliosoma nigeria
 
kila m2 na bahati yake ktk hili never gvup kiasi hicho wapendwa mwaminini sir GOD ye akisema yes o no hata mpaka hapo ume2pa sh. Ngapi ulh
 
mliomba kaz mlijua kitatokea nini mtawaza ajira mpaka ln mmeondoa ujinga msimind kukaa kwenye viyoyoz ujasiriamali unatoa bila hata mkono wa m2
 
Mim nipo safarin naenda,,,,,hiyo idad hainiogopesg,,,naskia walioomba jumla ilikua elf 15 ndo wamewapunguza hadi elf 8
 
Data umepewa kama unataka analysis fanya mwenyewe. Naona wewe ni mzito kuelewa jamaa anamaanisha ilikuwa haina haja ya kuita watu wote hao kwani mtawala MWENYE AKILI anafanya uchambuzi wa awali kupata cream anayotaka then hiyo cream inashindanishwa yenyewe kupata watu wanaohitajika. HAWA JAMAA WANAFANYA WATU WAZIMA KAMA WANATAKA KWENDA FORM ONE
 
Uwingi wa watu walioomba si tatizo, kumbukeni wapo walioomba japo tayari wana kazi zao lakini wanataka kuziacha na kufanya UDOM. kwa hiyo kama umeitwa kwenye interview isiogope uwingi wa watu, peleka timu unaweza jikuta upo peke yako. Unabisha??????.
 
Uko sawa mtu wangu, lakini kama mtu anatoka mbali sana na kahela kenyewe hana ASIJISUMBUE kwani safari hii atakwenda kupata uzoefu tu, hawa jamaa nawafahamu kwani wamewahi kuajiri watu dili lilipo wekwa wazi wasio na sifa wakakimbia kazini wenyewe kulinda heshima za waliowaweka
 
inatisha na inasikitisha, nafasi 5 wanaomba watu 600! anyway nawatia moyo mkafanye huwez jua wewe ndo unasindikizwa
 
Kumbe huu usaili ndo umetuletea balaa la kwenda kusajiliwa kule jamhuri eeh? Dah! Kila la heri watumishi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom