Maajabu ya mtoto aliyeteswa na wazazi wake mbeya na kufungiwa ndani miaka 2....!!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Moto Joshua akiwa amekaa uwani kwenye nyumba yao huku wazazi wake wakiwa wamemwacha peke yake toka asubuhi bila ya kumpatia chakula mtoto huyo tumemkuta katika hali mbaya sana kwani tunemkuta amejisaidia haja ndogo na hana hata nguo za kubadilisha.
DSC00124.JPG
Kwa ujumla mtoto Joshua hata kutembea hawezi kwani simama yake ni ya kutetemeka migu tu

DSC00129.JPG
Hizi ni nguo za joshua na kaka yake nguo hizi hazifuliwi bali zikirowa na mkojo huwanikwa tu juani na kisha kuvaliwa tena

DSC00131.JPG
Mtoto Joshua akiwa ana tushangaa maana anaona amevamiwa kwakweli inasikitisha sana

DSC00139.JPG
Hapa ndiyo mtoto joshua huwa anacheza wakati wa mchana

DSC00148.JPG
Mlango ulio wazi ndimo mtoto Joshua hufungiwa humo

DSC00155.JPG
Hiki ndicho chumba mtoto Joshua hufungiwa kama picha unavyoiona kona hiyo ndiyo mtoto huyo hujibanza

DSC00162.JPG
Kushoto ni kaka wa Joshua yeye amesema huwa anashinda nyumba za jirani kucheza wakati mdogo wake amefungiwa ndani

DSC00169.JPG
Angalia picha hii kwa makini jinsi mtoto Joshua anavyomwangalia mama yake mlezi yaani mama wa kambo.

DSC00171.JPG
Sekera Watsoni (40) amembeba mtoto Joshua kuonyesha anampenda na kuwa anamhudumia vizuri mtoto huyo.

DSC00176.JPG
Huyu mama pamoja na mumewe ndiyo wanaomtesa mtoto Joshua.
DSC00196.JPG
Hawa kaka zake Joshua wakituonyesha sehemu wanayolala pamoja na joshua wakati mama huyo yeye amesema yeye huwa analala na joshua chumbani kwake

DSC00205.JPG
Baadhi ya majirani wakisimulia mkasa huo.

DSC00208.JPG
Amini usiamini mtoto Joshua baada ya kuona mkeka mzuri alijilaza kwa furaha kwani amezoea kulala sakafuni.
DSC00223.JPG
Mama mlezi wa Joshua akijiandaa kumpeleka joshua kituo cha afya akapate matibabu baada ya kuamriwa kufanya hivyo.
DSC00231.JPG

DSC00182.JPG
Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto mwenye umri wa zaidi ya miaka miwili amefungiwa ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka miwili sasa bila kutoka nje pamoja na kukosa matunzo muhimu hali ambayo imepelekea mtoto huyo kudhoofu kiafya.

Tukio hilo limetokea leo jijini mbeya katika mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga ambapo majirani wa karibu na mtoto huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa mtaa huo kufika nyumbani anapoishi mtoto huyo kwa lengo la kufahamu maendeleo yake .

Mtoto huyo amefahamika kwa jina la Joshua Joseph umri unao kadiriwa kuwa ni kati ya miaka miwili au mitatu ambaye alikutwa nyumbani hapo akiwa pekee yake huku wazazi wake wakiwa wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao.

Akizungumzia tukio hilo Kaimu barozi wa mtaa huo wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema kuwa hali hiyo imenza kujitokeza kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na maradhi ya utapiamlo.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2011 mwezi wa tatu alipokea taarifa kuhusiana na suala hilo ambapo baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni aliitwa katika ofisi za mtaa kwa lengo la kumhoji juu ya malezi ya mtoto huyo.

Aidha baada ya kuhojiwa alikiri kosa ambapo alipewa onyo na viongozi wa mtaa ambao walimtaka kuhakikisha anamtunza vema mtoto huyo kwa kumpatia chakula bora pamoja na huduma nyingine.

Mara baada ya mtu huyo kupewa kalipio na viongozi wa mtaa hali hiyo iliendelea tena ambapo wao kama viongozi wa shina pamoja na wananchi walimuita yeye pamoja na mke wake aitwaye Sekera Watsoni (40) kuhama mtaani hapo kwa kwa kipindi cha miezi sita ambapo walikaidi agizo hilo.

Amesema mara baada ya watu hao kugoma waliamua kuwaacha na kuwaondoa katika umoja wa ubarozi wao na kuto watambua tena kama wananchi wa eneo hilo kutokana na vitendo vyao vya kikatili dhidi ya mtoto huyo.

Kwa upande wao Maafisa maaendeleo ya jamii kata ya Igawilo na Iyunga ambao ndio waliofika katika eneo hilo wamesema kuwa matukio kama hayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ndani ya jamii hasa kwa vitendo vya kunyanyaswa kwa watoto wanawake.

Mmoja wa Maafisa hao Ndugu Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo.
Amesema hali ya kiafya ya mtoto si ya kulizisha kutokana na kusumbuliwanna maradhi mbalimbali yanayotokana na kukosekana kwa lishe bora pamoja na huduma nyingine.

Amesema anawashukuru majirani pamoja na viongozi wengine wa serikali ya mtaa ambao wamekuwa karibu na mtoto huyo kwa kipindi chote cha miaka miwili licha ya kutokuwepo kwa ushirikiano toka kwa wazazi wa mtoto ambaye kwa sasa amefikishwa katika kituo cha afya Inyala Kata ya Iyunga jijini hapa.

Awali inaelezwa kuwa baba na mama wa mtoto huyo wamekwisha tengana kwa kipindi kirefu sasa kutokana na kutokuwepo kwa maelewano ndani ya nyumba hiyo hali ambayo ilimfanya baba huyo kuoa mwanamke mwingine ambaye ndiye anaye ishi na mtoto kwa sasa kama mama wa kambo.

DSC00117.JPG

Amesema kutoka na kuwepo kwa mgawanyiko huo ndani ya familia baba pamoja na mama huyo ambaye ni mke wa pili walichukua jukumu la kuishi na watoto wote walio achwa na mwanamke wa kwanza ambapo kwa asilimia kubwa ndiko kuliko sabababisha kuwepo kwa hali hiyo ya manyanyaso ya mtoto.
Hata wakati wa tukio hilo la kumtoa mtoto huyo ndani baba mzazi wa mtoto hakuwepo katika maeneo hayo ya nyumbani ambapo maafisa ustawi wa jamii pamoja na majirani waliamua kuchukua jukumu la kumpeleka mtoto huyo katika kituo cha afya Inyala kilichopo Kata ya Iyunga kwa lengo la kumfanyia uchunguzi na kutambua nini kinacho msumbua mtoto huyo.

MAAJABU YA MTOTO ALIYETESWA NA WAZAZI WAKE MBEYA NA KUFUNGIWA NDANI MIAKA 2....!! - GUMZO LA JIJI
 
mijitu mingine imelaaniwa. hivi hawa nao walipata uchungu wa kuzaa, ni bora wangemtoa for adoption kama hawakutaka kulea. sad in deed. wazazi kama wakifungwa jela roho yangu hainiumi.
 
Na ukiangalia sana chanzo ni mwanaume
kamwacha aliyezaa hao watoto
kaamua kuoa mwanamke mwingine,

Ona sasa matokeo yake, MziziMkavu ndo zenu hizo.

hapo sasa, wengine wanaenda hadi kwa waganga wa kienyeji, kula hadi uchafu alimuradi tu wapate watoto, wengine wanapata watoto kiulainii halafu wanawatesa, wanawatupa n.k, hii dunia hii.....

bofya hapa kupata kitabu bora kabisa cha haki za watoto ili tuelimishe jamii. SHERIA KWA KISWAHILI

View attachment 105186

View attachment 105187
 
Last edited by a moderator:
huyo mama mzazi wa mtoto ana akili timamu.....?....mtoto mdogo hivi unamwachaje na mama wa kambo.....?
 
....wale wanaowanywesha watoto PIRITONI/valium usiku then wanaenda Disco au kujinadi mbona hamuwateti?
 
huyo mama mzazi wa mtoto ana akili timamu.....?....mtoto mdogo hivi unamwachaje na mama wa kambo.....?
Kwa kweli mama mzazi wa mtoto ndio mjinga kupindukia! Hata iweje hakutakiwa kumwacha mtoto mdogo hivyo kulelewa na mama wa kambo! Yaani wote watatu ni wanyama! Baba, mama na mama wa kambo wote hawana huruma wala upendo.
 
unyanyasaji wa watoto Tanzania umezidi sana. ni wajibu wa kila raia kufichua maovu ambayo watoto wanafanyiwa either na wazazo wao wa kuwazaa, wazazi wa kambo au raia wengine tu. tusisubiri hadi ustawi wa jamii wafichue mambo, majirani na yeyote anayejua ovu lolote linalotendeka kwa watoto ni wajibu wake kwa Mungu na kwa wanadamu pia kufichua maovu hayo kwa maslahi ya watoto wetu jamani.

kwenye kitabu hiki nimeandika baadhi ya haki za watoto kulingana na sheria ya watoto No. 21 ya mwaka 2009. hatutakiwi kuwatelekeza watoto, kuwafungia ndani kwasababu wanahitaji association na ulimwengu wa nje, wanahitaji kujiexpress, hawahitaji kupigwa (bali kuonywa), hawahitaji kunyimwa chakula, hata wakiwa zaidi ya miaka 10 wakikamatwa na polisi kuna haki zao, watoto hawatakiwi kuwekwa ndani hata wakipatikana na kosa la jinai na mambo mengi kama hayo...pata nakala hii hapa ili tuelimishe jamii...bofya hapa SHERIA KWA KISWAHILI

View attachment 105181

View attachment 105182View attachment 105182View attachment 105182

mkuu naona unakinadi kitabu chako hasaaaaaaaaaaaa
Safi
 
hii story imenihuzunsha sana mtu mzima. Hapo ndo naelewa kumbe kuitwa baba ni jambo zito sana duniani.
Ndugu zangu msikurupuke kuzaa kama hamjajiandaa kuwa wazazi.
Kuitwa baba na mama sio kulipia mahitaji ya mtoto pekee. Malezi yanahusika sana. Kama unabisha muulize nini Mtambuzi alipitia alipompoteza mwanae kwa masaa kadhaa
 
Last edited by a moderator:
huyo mama mzazi wa mtoto ana akili timamu.....?....mtoto mdogo hivi unamwachaje na mama wa kambo.....?
Preta huyu mama Mzazi hana akili kabisa.mtoto siku zote ni mama.hakupaswa kumwacha mtoto wake hata Kama hana uhakika wa kula yake.nimechukia sana.
 
Moto Joshua akiwa amekaa uwani kwenye nyumba yao huku wazazi wake wakiwa wamemwacha peke yake toka asubuhi bila ya kumpatia chakula mtoto huyo tumemkuta katika hali mbaya sana kwani tunemkuta amejisaidia haja ndogo na hana hata nguo za kubadilisha.
DSC00124.JPG

Kwa ujumla mtoto Joshua hata kutembea hawezi kwani simama yake ni ya kutetemeka migu tu

DSC00129.JPG

Hizi ni nguo za joshua na kaka yake nguo hizi hazifuliwi bali zikirowa na mkojo huwanikwa tu juani na kisha kuvaliwa tena

DSC00131.JPG

Mtoto Joshua akiwa ana tushangaa maana anaona amevamiwa kwakweli inasikitisha sana

DSC00139.JPG

Hapa ndiyo mtoto joshua huwa anacheza wakati wa mchana

DSC00148.JPG

Mlango ulio wazi ndimo mtoto Joshua hufungiwa humo

DSC00155.JPG

Hiki ndicho chumba mtoto Joshua hufungiwa kama picha unavyoiona kona hiyo ndiyo mtoto huyo hujibanza

DSC00162.JPG

Kushoto ni kaka wa Joshua yeye amesema huwa anashinda nyumba za jirani kucheza wakati mdogo wake amefungiwa ndani

DSC00169.JPG

Angalia picha hii kwa makini jinsi mtoto Joshua anavyomwangalia mama yake mlezi yaani mama wa kambo.

DSC00171.JPG

Sekera Watsoni (40) amembeba mtoto Joshua kuonyesha anampenda na kuwa anamhudumia vizuri mtoto huyo.

DSC00176.JPG

Huyu mama pamoja na mumewe ndiyo wanaomtesa mtoto Joshua.
DSC00196.JPG

Hawa kaka zake Joshua wakituonyesha sehemu wanayolala pamoja na joshua wakati mama huyo yeye amesema yeye huwa analala na joshua chumbani kwake

DSC00205.JPG

Baadhi ya majirani wakisimulia mkasa huo.

DSC00208.JPG

Amini usiamini mtoto Joshua baada ya kuona mkeka mzuri alijilaza kwa furaha kwani amezoea kulala sakafuni.
DSC00223.JPG

Mama mlezi wa Joshua akijiandaa kumpeleka joshua kituo cha afya akapate matibabu baada ya kuamriwa kufanya hivyo.
DSC00231.JPG

DSC00182.JPG

Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto mwenye umri wa zaidi ya miaka miwili amefungiwa ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka miwili sasa bila kutoka nje pamoja na kukosa matunzo muhimu hali ambayo imepelekea mtoto huyo kudhoofu kiafya.

Tukio hilo limetokea leo jijini mbeya katika mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga ambapo majirani wa karibu na mtoto huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa mtaa huo kufika nyumbani anapoishi mtoto huyo kwa lengo la kufahamu maendeleo yake .

Mtoto huyo amefahamika kwa jina la Joshua Joseph umri unao kadiriwa kuwa ni kati ya miaka miwili au mitatu ambaye alikutwa nyumbani hapo akiwa pekee yake huku wazazi wake wakiwa wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao.

Akizungumzia tukio hilo Kaimu barozi wa mtaa huo wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema kuwa hali hiyo imenza kujitokeza kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na maradhi ya utapiamlo.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2011 mwezi wa tatu alipokea taarifa kuhusiana na suala hilo ambapo baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni aliitwa katika ofisi za mtaa kwa lengo la kumhoji juu ya malezi ya mtoto huyo.

Aidha baada ya kuhojiwa alikiri kosa ambapo alipewa onyo na viongozi wa mtaa ambao walimtaka kuhakikisha anamtunza vema mtoto huyo kwa kumpatia chakula bora pamoja na huduma nyingine.

Mara baada ya mtu huyo kupewa kalipio na viongozi wa mtaa hali hiyo iliendelea tena ambapo wao kama viongozi wa shina pamoja na wananchi walimuita yeye pamoja na mke wake aitwaye Sekera Watsoni (40) kuhama mtaani hapo kwa kwa kipindi cha miezi sita ambapo walikaidi agizo hilo.

Amesema mara baada ya watu hao kugoma waliamua kuwaacha na kuwaondoa katika umoja wa ubarozi wao na kuto watambua tena kama wananchi wa eneo hilo kutokana na vitendo vyao vya kikatili dhidi ya mtoto huyo.

Kwa upande wao Maafisa maaendeleo ya jamii kata ya Igawilo na Iyunga ambao ndio waliofika katika eneo hilo wamesema kuwa matukio kama hayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ndani ya jamii hasa kwa vitendo vya kunyanyaswa kwa watoto wanawake.

Mmoja wa Maafisa hao Ndugu Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo.
Amesema hali ya kiafya ya mtoto si ya kulizisha kutokana na kusumbuliwanna maradhi mbalimbali yanayotokana na kukosekana kwa lishe bora pamoja na huduma nyingine.

Amesema anawashukuru majirani pamoja na viongozi wengine wa serikali ya mtaa ambao wamekuwa karibu na mtoto huyo kwa kipindi chote cha miaka miwili licha ya kutokuwepo kwa ushirikiano toka kwa wazazi wa mtoto ambaye kwa sasa amefikishwa katika kituo cha afya Inyala Kata ya Iyunga jijini hapa.

Awali inaelezwa kuwa baba na mama wa mtoto huyo wamekwisha tengana kwa kipindi kirefu sasa kutokana na kutokuwepo kwa maelewano ndani ya nyumba hiyo hali ambayo ilimfanya baba huyo kuoa mwanamke mwingine ambaye ndiye anaye ishi na mtoto kwa sasa kama mama wa kambo.

DSC00117.JPG

Amesema kutoka na kuwepo kwa mgawanyiko huo ndani ya familia baba pamoja na mama huyo ambaye ni mke wa pili walichukua jukumu la kuishi na watoto wote walio achwa na mwanamke wa kwanza ambapo kwa asilimia kubwa ndiko kuliko sabababisha kuwepo kwa hali hiyo ya manyanyaso ya mtoto.
Hata wakati wa tukio hilo la kumtoa mtoto huyo ndani baba mzazi wa mtoto hakuwepo katika maeneo hayo ya nyumbani ambapo maafisa ustawi wa jamii pamoja na majirani waliamua kuchukua jukumu la kumpeleka mtoto huyo katika kituo cha afya Inyala kilichopo Kata ya Iyunga kwa lengo la kumfanyia uchunguzi na kutambua nini kinacho msumbua mtoto huyo.

MAAJABU YA MTOTO ALIYETESWA NA WAZAZI WAKE MBEYA NA KUFUNGIWA NDANI MIAKA 2....!! - GUMZO LA JIJI

But, Joshua has always been the winner.This innocent, poor kid is going to win,..., believe me!
 
Inasikitisha jamani.
Hii inaonesha mama yake mzazi na Joshua hajawahi kuja kumtembelea Joshua kwa miaka yote hiyo,hivi mimi ningeweza kweli kumuacha mtoto wangu ateseke hivi?
 
Back
Top Bottom