maajabu ya mh. Eugine mwaiposa!

Kanuniya68

Senior Member
May 26, 2013
157
44
Wakati wenzetu wakenya wakianza kukabidhi laptop kwa wanzafunzi, Mbunge wa CCM, Eugine Mwaiposa anadai watoto wamefeli kwa sababu ya kutumia internet! Hivi, kule Ileje, Nkasi, Nanyumbu n.k kumejaa internet cafe?. Hakuishia hapo,anadai wanafeli pia kwa kusoma magazeti..hasa ya siasa! Kaaz kwel kwel!.,.mtoto akisoma tzdaima,uhuru ,nipashe n.k, anaongeza upeo, au ndo anafeli?
 
Watu wa Ukonga hawana mbunge kwa sasa ila wana mwakilishi mwanamama kichaa anaitwa Eigen Mwaiposa.
Huwa haongeaji mara nyingi bungeni ila siku akiongea ni uchafu mtupu ataropoka.
Hili ni gamba bovu, gumu na chafu kabisa la CCM.

Nina uhakika 2015, Ukonga ni ya CHADEMA chini ya Kamanda Michael Aweda.
 
Viongozi wetu ni janga, hususani wawakilishi wetu wabunge, nimekuwa siku zote naishagaa hii kauli ya watoto wengi kufeli ni kwa sababu ya simu na internet, ndugu yangu hachilia mbali hayo maeneo uliyoyataja, ni juavyo mimi zaidi ya asilimia 90 ya wanafunzi wa o level wa kitanzania hawana access na internet wala kumiliki simu
 
Si mzima huyo.Anatokea kijiji gani? yuko enzi za ugeni wa pool table,hadi likapigwa marufuku muda wa kazi,te te te te te,hii nchi!
 
Niliwahi kumsikia Waziri husika wa elimu Dr Shukuru akisema watoto wamefeli kwa sababu hakukuwa na leakage ya mitihani. Sasa kama hiyo ndiyo sababu ana maanisha kuwa wanafunzi wa TZ ni vilaza na hawana uwezo wa kufaulu. Ila ameonesha kabisa udhaifu mkubwa katika sekta ya elimu kushindwa kufundisha watoto wakawa na uelewa mzuri zaidi ya kusubiri mitihani kuleak. Huyu mama kusingizia internet ni kukosa hoja. Kwani amejaribu kugeneralize negative effects za internet kwa wanafunzi bila kuchambua upatikanaji wa huduma ya internet haswa vijijini ambapo hata huko umeme upatikanaji ni kwa kiwango cha 15% tu. Hawa ni baadhi ya wabunge wanaojadili hoja kwa udaku bila kuwa na facts wala knowledge ya kinachozungumzwa. Kwa ufupi amekosa cha kuchangia.
 
Ngoja nisome tena Rasimu ya katiba inapendekeza nini kuhusu wabunge kama huyo home girl.

Baadaye tutakuwa na uwezo wa kuwapiga chini wabunge viazi kabla ya uchaguzi.
 
Mama huyu Jimbo aonekani, Bungeni kuongea kwa nadra na zaidi ya yote yupo likizo toka Mwanzo wa Mwaka hadi Mwisho. Madibwi ya maji yaliyokuwa jamejaa Kitunda, kivule, Moshi Bar na sasa Vumbi yeye kwake ni Kheri tu. Ukongo hakuna Mbunge bali tuna Mwakilishi wa Wanawake bungeni.
 
Viongozi wetu ni janga, hususani wawakilishi wetu wabunge, nimekuwa siku zote naishagaa hii kauli ya watoto wengi kufeli ni kwa sababu ya simu na internet, ndugu yangu hachilia mbali hayo maeneo uliyoyataja, ni juavyo mimi zaidi ya asilimia 90 ya wanafunzi wa o level wa kitanzania hawana access na internet wala kumiliki simu

Inawezekana baadhi ya hao wawakilishi wala hawana accounts. Lakini pia huku ni kujisahau kwa hali ya juu sana kwani baada ya kuchaguliwa hawarudi vijijini kujionea hali halisi. Wanabaki Dar es Salaam na ndiyo maana wanadhani maisha wanayoishi wao ndiyo ya kila Mtanganyika. This is serious. Hakuna mtu anayetoka kwenye kijiji per se anaweza kuzungumza utumbo kama huo. Baadhi ya shule ziko machakani hata njia, licha ya barabara y akufika huko ni mgogoro. Leo mtu anasimama anazungumza habari za internet. Anasahau mwenzie alitumia machozi strategy ili apatiwe mtandao. Mtu mzima hovyo!
 
​Hana habari kuwa hata serikali yake inahamia digitali!
 
majanga,mbona majanga.Tanzania tuna ombwe la fikra ambalo tusipokuwa makini vizazi vijavyo vitarithi nchi ya matahira
 
hakuna sababu ya kumjadili huyo mama Jamani , haya ni matokeo ya ile Sera ya Mwanamke 'akiwezeshwa ' anaweza !
 
Heee huyu nae mbunge au!! Ajui kwamba kuna materia mengine yanapatikana kwenye mtandao? Aujui kwamba mnaweza mkabadilishana maujuzi na nondo kupitia intaneti? Wish watoto wake waje wamwambie mama pale ulichemka
 
Wakati wenzetu wakenya wakianza kukabidhi laptop kwa wanzafunzi, Mbunge wa CCM, Eugine Mwaiposa anadai watoto wamefeli kwa sababu ya kutumia internet! Hivi, kule Ileje, Nkasi, Nanyumbu n.k kumejaa internet cafe?. Hakuishia hapo,anadai wanafeli pia kwa kusoma magazeti..hasa ya siasa! Kaaz kwel kwel!.,.mtoto akisoma tzdaima,uhuru ,nipashe n.k, anaongeza upeo, au ndo anafeli?

Hawa watoto wa kitanzana ukiwapa laptop umewaua kabisaaaaa, mama hajakosea.
 
Heee huyu nae mbunge au!! Ajui kwamba kuna materia mengine yanapatikana kwenye mtandao? Aujui kwamba mnaweza mkabadilishana maujuzi na nondo kupitia intaneti? Wish watoto wake waje wamwambie mama pale ulichemka

materia???
 
Kwahiyo solution anataka iwe nini?!
Anaongea kwa takwimu gan?
Au kawaangalia wanae nyumbani?
Kungekuwa na research imefanyika na kubainisha ni percent ngapi ya wanafunzi waliomaliza wana simu na internet,na wangap wamefaulu wangapi wamefeli hapo ningemuona mwakilishi!
Ila kuropoka tu haisaidii

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
majanga,mbona majanga.Tanzania tuna ombwe la fikra ambalo tusipokuwa makini vizazi vijavyo vitarithi nchi ya matahira

upokeaji wa michango ya wabunge pia ni tatizo humu JF.Kama umemsikiliza vizuri Mwaiposa, alijikita zaidi kuelezea matumizi mabaya ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa wanafunzi na hilo ni tatizo kweli sasa tukianza kujadili michango ya wabunge kisiasa ni kupotezeana muda leteni mada zingine zenye uhai.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom