Maajabu ya mazishi ya Kisukuma

fullcup

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
806
2,181
Habari za muda huu

Poleni na pilika za uchaguzi mkuu na mambo mengine yanayifanana nayo.

Leo asubuhi nimepigiwa sim kuwa kuna msiba kijijini 50 km toka main road ya Mbeya - Dar.

Tumefika na kujumuika katika kuchimba kaburi ili tumpumzishe mpendwa wetu. Kaburi limechimbwa na mazishi yamefanyika.

KILICHONISHANGAZA

Kaburi lina kimwana ndani(,kwa waislam wanaelewa). Tofauti na kimwanandani kinachoandaliwa na waislam huwa katikati ya kaburi, hawa wasukuma wameweka pembeni kwenye kingo ya kaburi.

Sanda; wakati waislam wanatumia sanda za kawaida hizi nyeupe wao wanatumia mashuka na NGOZI. Ndio ni ngozi ya ng'ombe ambae huandaliwa kwaajili ya kumvika marehemu.

Huyu ng'ombe anaetoa ngozi ya kuzikia hachinjwi!. Kinachofanyika anafungwa miguu yote na kuangushwa kisha anapigwa rungu za kisogo kama tatu hivi na kukata moto ndipo uchunaji unaendelea.

Mazishi yanahisisha wanaume tu kama kwenye uislam isipokuwa huku vifaa vinavyotumika katika kuandaa kaburi na kuzikia huachwa juu ya kaburi kwa siku tatu.

Nyama ya ng'ombe anaetoa ngozi ya kuzikia haipikwi bali huchomwa tu mpaka inaisha. Nyama hiyo wafiwa hawali na wala hairuhusiwi kuingia nayo kwenye nyumba za marehemu.

Ng'ombe mwingine huchinjwa kwaajili ya mboga hiyo hutumiwa na watu wote. Hivyo katika msiba mmoja lazima ng'ombe wawili wapoteze uhai.

NILICHOJIFUNZA

Imani na mila haviingiliwi yaani yote hayo yanafanyika na viongozi wapo. Mchango wa ndugu na wa serikali unakuwepo lakini hakuna kuzikia sijui vinini ni ngozi tu!.

Ngoja Nile nyama kwanza nitakuja kuendelea.
 
Duh hayo sio maziko ya chifu wao kweli?

Maana kama kila msiba zinaenda ngozi nzimanzima mbili na saivi watu wanavyokata moto hivi daah
 
Sio chifu ni mkulima wa kawaida tu na ng'ombe wenyewe wamenunua tu kwaajili ya kukamilisha taratibu za kijamii.
 
Alikua ana uganga huyo au la kuna aina flan ya uchawi alikua anautumia sio raia wa kawaida naamini hivyo Mkuu
 
KILICHONISHANGAZA
Kaburi lina kimwana ndani(,kwa waislam wanaelewa). Tofauti na kimwanandani kinachoandaliwa na waislam huwa katikati ya kaburi, hawa wasukuma wameweka pembeni kwenye kingo ya kaburi.
Mwanandani kwa Waislamu pia hua pembezoni mwa kaburi haiwi katikati ya kaburi.
Kama uliwahi kuona Waislamu wamechimba mwanadani katikati ya kaburi ujuwe watu hao wanahitaji kuelimishwa.
 
Habari za muda huu

Poleni na pilika za uchaguzi mkuu na mambo mengine yanayifanana nayo.

Leo asubuhi nimepigiwa sim kuwa kuna msiba kijijini 50 km toka main road ya Mbeya - Dar.

Tumefika na kujumuika katika kuchimba kaburi ili tumpumzishe mpendwa wetu. Kaburi limechimbwa na mazishi yamefanyika.

KILICHONISHANGAZA

Kaburi lina kimwana ndani(,kwa waislam wanaelewa). Tofauti na kimwanandani kinachoandaliwa na waislam huwa katikati ya kaburi, hawa wasukuma wameweka pembeni kwenye kingo ya kaburi.

Sanda; wakati waislam wanatumia sanda za kawaida hizi nyeupe wao wanatumia mashuka na NGOZI. Ndio ni ngozi ya ng'ombe ambae huandaliwa kwaajili ya kumvika marehemu.

Huyu ng'ombe anaetoa ngozi ya kuzikia hachinjwi!. Kinachofanyika anafungwa miguu yote na kuangushwa kisha anapigwa rungu za kisogo kama tatu hivi na kukata moto ndipo uchunaji unaendelea.

Mazishi yanahisisha wanaume tu kama kwenye uislam isipokuwa huku vifaa vinavyotumika katika kuandaa kaburi na kuzikia huachwa juu ya kaburi kwa siku tatu.

Nyama ya ng'ombe anaetoa ngozi ya kuzikia haipikwi bali huchomwa tu mpaka inaisha. Nyama hiyo wafiwa hawali na wala hairuhusiwi kuingia nayo kwenye nyumba za marehemu.

Ng'ombe mwingine huchinjwa kwaajili ya mboga hiyo hutumiwa na watu wote. Hivyo katika msiba mmoja lazima ng'ombe wawili wapoteze uhai.

NILICHOJIFUNZA

Imani na mila haviingiliwi yaani yote hayo yanafanyika na viongozi wapo. Mchango wa ndugu na wa serikali unakuwepo lakini hakuna kuzikia sijui vinini ni ngozi tu!.

Ngoja Nile nyama kwanza nitakuja kuendelea.
tuseme: mambo ya kizungu na kiarabu tupa kuleeeeeee. Si tunaendelea na mila zetu
 
Shemeji zangu hawa sio watu. Kaa nao utawajua. Ila ndio hivyo ndoa Ni kuvumiliana. Tako liliniponza
 
Back
Top Bottom