Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa Songwe, Ayubu Sikagonamo alikamatwa na Polisi kwa tuhuma za uchochezi (kutumia mitandao kuikashifu serikali ya Rais JPM). Baadae akapandishwa mahakama ya Wilaya Momba kujibu mashtaka yanayomkabili. Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Zabibu Mpangule akamnyima dhamana.
Upande wa mlalamikiwa ukiongozwa na Wakili Msomi Rose Kayumbo ukakata rufaa mahakama kuu, kudai haki ya dhamana kwa mteja wao. Baada ya kupitia shauri hilo, mahakama kuu (masijala ya Mbeya) jana ikabatilisha uamuzi wa mahakama ya wilaya Momba na kumpa Ayubu dhamana. Kwa hiyo Ayubu akaachiwa kwa dhamana jana.
Lakini katika hali ya kustaajabisha, leo Polisi wamefika nyumbani kwake na kumkamata kwa maagizo ya Hakimu Zabibu Mpangule. Hakimu Mpangule anasema ameagiza Ayubu akamatwe tena kwa kuwa hana taarifa kama alishinda rufaa yake, kwa kuwa hajapewa nakala ya 'ruling' kutoka mahakama kuu.
Sasa wanasheria njooni mtoe ufafanuzi kwenye mambo yafuatayo:
1. Je Hakimu anayo mamlaka ya kuagiza mtuhumiwa akamatwe tena baada ya kuachiwa na mahakama ya juu yake?
2. Je Hakimu wa Mahakama ya wilaya anayo 'mandate' ya kuchallenge maamuzi yaliyotolewa na Jaji wa mahakama kuu?
3. Kama Hakimu hakupata nakala ya 'ruling' hilo ni kosa la mtuhumiwa au kosa la Mahakama iliyomuachia huru?
4. Kukosa nakala ya "ruling" kunajustify mtuhumiwa kurudishwa rumande?
5. Ikiwa Hakimu Mpangule atapewa nakala ya 'ruling' je atamuachia Ayubu huru? Na kama akimuachia, je Ayubu anaweza kumshtaki Hakimu huyo kwa usumbufu alioupata?
6. Kitendo cha Hakimu Mpangule kufuatilia na kujua Ayubu ameachiwa na kuagiza akamatwe tena, lakini Hakimu huyohuyo akashindwa kufuatilia nakala ya 'rulling' haitoi tafsiri kuwa ana 'maslahi' na kesi hii?
7. Na kama ameanza kupambana na mtuhumiwa just kwenye dhamana, je ataweza kutenda haki kesi ya msingi (ya uchochezi) itakapoanza kusikilizwa?