Maajabu ya Magufuli: Uchumi wa Tanzania wakua zaidi ya nchi zingine za Afrika Mashariki

Ebu acha ujinga hivi unajua budget ya Kenya ni kiasi gani kwa mwaka? na umelinganisha na ya TZ ukaona kwamba jamaa wamelala nyie mnaokaba boda boda kukusanya kodi ndio mnakuwa. Wewe ulivyosikia ukashindwa kuchanganya na za kwako na kuona takwimu.

Kiongozi wenu kesha sema hajalibiwi wewe unamjaribu wenzio walikuwa TBC walisema kasifiwa na Donard kawafumua fasta ngoja wakutafute na wewe.
uelewa wako ni hafifu..jifunze kutofautisha ukubwa wa uchumi na kasi ya ukuaji wa uchumi..kenya yaweza kuwa na uchumi mkubwa, lakini ikawa na kasi ndogo ya ukuaji wa uchumi. Tanzania inakua kwa kasi ya wastani wa asilimia 7 kila mwaka, hii inaonesha kuna uwezekano wa Tanzania kuwa na uchumi mkubwa kwa haraka zaidi na hata kuipita kenya kwa miaka michache ijayo. Ni kama China na Marekani, China inaonesha kukua kwa kasi kubwa ukilinganisha na Marekani, na wachambuzi wamesema China inaweza kuja kuipita Marekani kama itaendelea kukua kwa kasi hii.
 
Kukua kwa uchumi wa Tanzania kwa juu au kidogo ya 7% kulianza zaidi ya miaka 10 awamu ya Mkapa, JK aliikuta hali hivyo na kuiacha. Kumsifia Magufuli kwa hilo sio sahihi.
7% ya kukua kwa uchumi imezeeka hapa kwetu huku kila mara kilio kimebakia kwa nini kukua huko hakuonekani kwa watu?
 
Guys muwe mnaangalia mnaongea na watu wenye uelewa wa level gani. Wao wanajua kukua kwa uchumi ni kuwa na individual wealth, kwa mzee mgabe uchumi upo chininkuliko nchi yyt africa ila watu wana pesa balaa. Uchumi unakuwa mkubwa pale pesa inapoadimika. Hii ndo formula ktk uchumi. Na pesa inapokuwa nyingi sana mikononi mwa raia basi uchumi wa nchi husika hushuka. Kama huamini uliza profesor yyt wa uchumi atakwambia hili. Ndo maana unaona kina lipumba hawaongelei kubeza hii hali iliyopo. Labda kitu ambacho magu ameshindwa kukidhibiti ni mfumuko wa bei za vyakula, Na hii imechangiwa na mafuriko na ukame ulioikumba nchi toka aingie on power. Mi naamini rais wangu anafanya vizuri sana maana anasifiwa kila kona ya dunia. Nyie watu mnaotaka kuvuna msipopanda ndo mnaolalamika kila kukicha. And salam yangu kwenu hii hapa. Mpaka kufika 2020 sidhani kama upinzani utaendelea kuwepo na hisi utakuwa kama saccos tu. Maana mmeungana kuiangusha ccm bila kujua kuwa ndo mlikuwa mnachimba kaburi lenu wenyewe. Kwa sasa opp hakuna sera mnapiga makelele kama mtoto mwenyenjaa ukimpa hata kidole ananyonya tu. Mlikuwa na gia ya mafisadi awamu hii nyie mmegeuka mafisadi hamuwezi tena kuwambia watu habari ya ufisadi. OVA
 
Sembe ikipanda bei maana yake ni kuwa mkulima anapata fedha nyingi zaidi kutokana na jasho lake la kulima sembe. Mlizoea kuwapunja na kuwanyonya wakulima kwa kununua mazao yao kwa bei ya peanut. Acha wakulima wetu wauze sembe yao hata kwa Tsh 4,000 kwa kilo, korosho saa hizi angalao imefika 3,500 sh kwa kilo na mchele angalao 2,500 sh kwa kilo. Hii ndiyo kuwajaza wallet wakulima ambao idadi yao ni asilimia zaidi ya 80% ya watanzania. Ndiyo kukua kwa uchumi ambao hupimwa kwa per capital income. Huko nyuma wallet zilizokuwa zinajaa zilikuwa ni za wajanja wajanja tu. Sasa zinajaa wallet za wavuja jasho kama wakulima. Bei ya vyakula iendelee kupanda. Kama vipi na wewe nenda ukalime kama unataka wallet yako ijae.

Mlizoea kuwanyonya wakulima na wafugaji kwa kuchukua mazao yao kwa bei ya sawa na bure. Utakuta jitu linakunywa bia kwa mwezi za gharama ya laki mbili shs kwa mwezi lakini sembe na nyama linazokula na kufula gharama zake hazizidi shs 30,000/ kwa mwezi, umeme linaotumia kwa mwezi shs 250,000/. Sasa kipi ni cha muhimu kati ya hivyo vitatu? Kwa nini mzalishaji wa kitu cha mhimu kwa maisha yako unataka akuuzie mazao yake kwa bei ya sawa na bure wakati yule anayezalisha vitu ambavyo si vya muhimu kwako kuishi kama vilevi na umeme uko tayari kumlipa pesa ya kutakata?

Mkulima kupata gunia 100 za mahindi kwa mwaka si kazi rahisi. Lakini unakuta alikuwa anauza gunia moja la mahindi kwa shs 40,000 au chini ya hapo (yaani debe sh 7,000/ au chini). Maana yake capital income yake kwa mwaka ni 100×40,000 shs = sh million 4 tu hivyo kwa siku kipato chake kwa siku haifiki US dollar moja na kwa hiyo kwa viwango vya kimataifa ni masikini wa kutupwa. Tupandishe bei ya gunia la mahindi lifikie angalao shs 150,000/ ili kumwondoa mkulima huyu katika kundi la masikini wa kutupwa. Hii ndiyo njia pekee ya kuondokana na umasikini. Wakulima na wafugaji wetu waneemeke. Sasa hivi eti tumekazania kuwaneemesha waigizaji na wasanii wa bongo movie na bongo flava badala ya wakulima, wafugaji na wavuvi. Hii si sawa.
Ebwanaeee wewe ni professor. Umewajibu hawa watu vizuri
 
Mi kura yangu nampigia aisee. Huko nje sijaona viongozi baaaado saaana. Mniambie opp nani anafaa kuwa rais. Alikuwa slaa mlimfukuza wengine wote walafi
Uchumi Tz unakua 7% na Wa Kenya unakua 6.8 , tofauti IPO ndogo siyo kubwa saana kivile. Asiimia 7%ya budget ya trilioni 23 za Tz na %6.8 ya trilioni 53 walizopáta Kenya .Wenye kujua hesabu hivi itachukua miaka mingapi kuwafikia Kenya ?ukilingansha mareka na China ni tofauti sana maana marekani ana trilioni 15 na anakua kwa 2% wakati China ana GDP trilioni 11.5 na anakua kwa asilimia 8%. Ndani ya miaka 10 atapitwa marekani. Bila Tanzania kuipta Kenya IPO lakini si kabla ya mwaka 2050 .tuache ushabiki tuanalyse figure ziatuelezaje? Pia GDP inadanganya sana kwa sababu haionyeshi purchasing power ya individuals Picha unaipat ukiangalia ni sekta zinachangia hiyo GDP.zinaingiza pesa mikononi mwa walala hoi au ni madini na au ni zile za infrastructure ambazo haiwafikii direct walalahoi.hapa mtabishana sana bila tunahitaji wachumi kutafsiri data . ushabiki Wa kichama mnaishi matusi tu. Tafuteni nguvu ya hoja , si hoja ya nguvu. Mnatumia nguvu nyingi lakini hamueiimishi jamii ambayo nadhani ndiyo lengo LA mada?
 
Huo uchumi unaokuwa ni huu huu unaoshindwa kutekeleza Budget kwa 64%? Ni huu unaoshindwa ku strengthen Shilingi dhidi ya Currency nyingine?
Wachumi hebu tusaidieni katika hili!
 
Wana JF,

Habari za kuaminika kutoka wataalamu wa kiuchumi duniani ambao hufuatilia uchumi duniani ikiwemo AFRIKA MASHARIKI Imetoa ripoti yake kuwa UCHUMI wa Tanzania UNAKUA haraka sana na tayari UME OVERTAKE nchi nyingine za kanda hii ya Afrika Mashariki ZOTE!

Sababu zilizotolewa ni kuwa Rais Magufuli amejaribu sana KUZIBA upotevu wa fedha na kuwa HANDS ON katika kufuatilia kwa karibu uchumi wa nchi yake na kuhakikisha uchumi unakua.

ripoti hii inasema kuwa kuna MATUMAINI makubwa kwa Tanzania kuwa KIONGOZI kiuchumi wa nchi za Afrika Mashariki.

Nafikiri kama Watanzania bila kujali vyama vyetu tuna HAJA ya KUJIVUNIA mafanikio ya awamu ya 5 badala ya kuangalia mapungufu.
Maana siku njema huanza asubuhi.

Chanzo: IOL
ECONOMISTS
NTV-Kenya.
IMF. etc.
How? It doesn't make sense. Au ni makusanyo ya kodi?
 
HA HA HA WAONGO WAKUBWA HAO,BARGET YA KENYA NI KUBWA NA HUBAGERT WALICHONACHO MKONONI,NA HUITEKELEZA KWA KUKAMILISHA BURGET YAO KWA 100%,SISI HUITEKELEZA KWA 40%....!/
HATA KAMA SIO MSOMI,ZAKUAMBIWA ONGEZA NA ZAKO.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya Economic growth & Economic Development. Economic growth ni process ambayo imeanza kipindi kirefu na si katika awamu Hii ya tano. Hata hivyo ukuaji wetu hauendani kabisa na maendeleo ya watu kama Mwl Nyerere alivyosema. Ukuaji wetu was Uchumi upo sambamba na kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha Umaskini. Mfano uchumi wetu unakuwa kwa kiwango 7%. Wakati sekta myhimu Kilimo, Uvuvi ukuaji wake ni 2.033 Kilimo ni 0.033 hili sio LA kujivunia kwa RAIA wa Nchi. Kabla ya kusifu ni vyema ujue Takwimu halisi
 
Mitoto ya Lumumba Ina laana ikishapewa buku 3 inashinda humu kuongea utumbo usiku wanalala kwa shemeji zao sebuleni
 
Habari kama hizi zinawaumiza kichwa sana CHADUMAA na wale wafuata upepo wao.. Hii habari ingekua inasema Uchumi unashuka, uzi ungekua unakimbia [HASHTAG]#WatuwanawazaKura[/HASHTAG]
 
Wana JF,

Habari za kuaminika kutoka wataalamu wa kiuchumi duniani ambao hufuatilia uchumi duniani ikiwemo AFRIKA MASHARIKI Imetoa ripoti yake kuwa UCHUMI wa Tanzania UNAKUA haraka sana na tayari UME OVERTAKE nchi nyingine za kanda hii ya Afrika Mashariki ZOTE!

Sababu zilizotolewa ni kuwa Rais Magufuli amejaribu sana KUZIBA upotevu wa fedha na kuwa HANDS ON katika kufuatilia kwa karibu uchumi wa nchi yake na kuhakikisha uchumi unakua.

ripoti hii inasema kuwa kuna MATUMAINI makubwa kwa Tanzania kuwa KIONGOZI kiuchumi wa nchi za Afrika Mashariki.

Nafikiri kama Watanzania bila kujali vyama vyetu tuna HAJA ya KUJIVUNIA mafanikio ya awamu ya 5 badala ya kuangalia mapungufu.
Maana siku njema huanza asubuhi.

Chanzo: IOL
ECONOMISTS
NTV-Kenya.
IMF. etc.

Tunaomba weka links tujihakikishie wenyewe.
 
Uchumi naona unakua kwa kasi ya ajabu ndo maana hata bei ya unga imeshuka ghafla kutoka 1200 hadi 2600.
Hongera raisi

Tafsiri yake ni kuwa mkulima wetu ataingiza dola moja na ushee kwa kila kilo ya unga anazalisha....tukalime mahindi wakuu wachaneni na ngwasuma za mjini wakuu...
 
Back
Top Bottom