Maajabu ya jimbo la Kawe: Halina propoganda za kuletewa Maji, Barabara wala Umeme; akili tu ya mtu wa kujenga Taifa

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,512
2,000
Wana JF,

Jimbo la Kawe ni jimbo lililosheheni viongozi wengi vichwa, mpaka sasa kuna Mawaziri wakuu wastaafu watatu, makatibu wakuu karibu wote. Jimbo hili linataka mtu kichwa tu, si kwa kuwa na hela nyingi eti utafanya kampaini, la hasha. Lenye vituo vya mafuta, lina migogoro ya ardhi tu ambapo nayo inaisha hivi karibuni kufuatana na mifumo waliyoweka wataalum kutoka ardhi chini ya mfumo mpya wa umiliki wa kiwanja kuwa wa kidigitali. Barabara zote za miradi zimetengenezwa.

Pengine anaweza akatokea mtu akajinadi kuwa ataleta maendeleo kama kwamba anatoa pesa zake mfukoni; huyo ni muongo wa kutupwa, Kawe inahitaji mtu anayeweza kuwa na mawazo ya plan ya miji mipya hasa ya Boko, Bunju, Mabwepande, Mbweni na Ununio. Miji hii inakua kwa kasi na wanaojenga huko wana uwezo sana ondoa wale wenyeji ambao walijenga bila mpangilio.

Shida iliyopo ni kuwa na masoko ya kimataifa watu wakitumia Tegeta Nyuki kama soko kuu, kuwe na stand ya maana ya magari yaendayo kasikazini. Lakini hayo yote sio kazi ya mbunge bali ni ya serikali iyafanye ili nayo iweze kufanikiwa kimapato.

Mfano> akiwepo Stand kubwa ya Magari ya kaskazini, watu watajenga magest ya kulalala wageni, masoko makubwa, kukijengwa soko kubwa kama la Kariakoo kutapunguza wigo wa wafanyabiashara ndogo ndogo kutapakaa mjini wajiunge huko Kariakoo.

Kawe kama mji uliobeba vichwa tunahitaji mtu wa mikakati ya kujenga soko kubwa, stand kubwa ya kaskazini, viwanja vikubwa vya michezo ili serikali ivitumie kimapata kwa kuwa aliyepewa majuku ya kufanya hivi kakimbilia ubunge.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom