Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,589
- 1,679
Mkufu wa dhahabu wa urefu wa mita nne, tani kadhaa za dhabu halisi, masanamu yaliyotengenezwa kwa dhahabu na almasi, magunia kadhaa yaliyojaa vito vya zamani vyenye thamani kubwa vilivyotengenezwa kwa dhahabu na kunakshiwa kwa almasi, zumurudi, na vito vingine, ni baadhi tu ya hazina iliyokutwa katika makasha matano kati ya manane ndani ya hekalu la MABANIANI (Hindu) liitwalo Sree Padmanabhaswamy, huko Kerala, Kusini mwa India, wiki iliyopita.
Hazina hiyo iliyokuwa imefichwa ndani ya makasha hayo makubwa inasemekana ina umri wa zaidi ya miaka 130. Thamani ya mali hiyo iliyokwishafunguliwa hadi sasa inakadiriwa kuwa dola BILIONI 22, lakini wafanyibiashara wa Kimataifa wanasema hazina hiyo ina thamani ya dola BILIONI 100. Hii inalifanya hekalu hilo kuwa tajiri zaidi kuliko VATICAN ambayo utajiri wake unakadiriwa kuwa (vijisenti vya ) dola bilioni 15.
Na stori haishii hapo: bado kuna makasha matatu hayajafunguliwa. Kasha la sita litafunguliwa kesho Ijumaa!
Tayari Wahindi kadhaa wameingiwa na kiherehere cha kutaka kujaza viganja vyao (fistful) fungu la mali hiyo. Usithubutu! Kwani serikali ya Kerala, ishatuma vikosi vya polisi kulizunguka hekalu hilo. Malumbano makali yanaendelea sehemu nyingi za India kujadili ugavi wa mali hiyo nchini kote. Wakuu wa Kerala wanasema mali hiyo ibakie kwenye jimbo hilo, lakini wakuu wa Kitaifa wansema hazina hiyo inayotosha kuendesha Wizara ya Elimu ya India nzima kwa muda wa miaka miwili na nusu, iwanufaishe Wahindi wote!
Huu ni uvumbuzi wa hazina kubwa zaidi mahali pamoja katika historia ya mwanadamu!