Maajabu ya Bunge letu; Spika sasa hataki Mwongozo wala Taarifa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maajabu ya Bunge letu; Spika sasa hataki Mwongozo wala Taarifa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ibrah, Aug 4, 2011.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Jana jioni, nilipata bahati ya kushuhudia Bunge kabla TANESCO hawajanihujumu kwa kunikatia umeme.

  Kwa bahati nilimkuta Mh Halima Mdee akichangia hoja ya Wizara ya Miundo Mbinu, kwa kweli alikuwa anapiga virungu vya hatari. Baadaye akafuata Mh Deo Filikunjombe, naya akaja na kauli ya kutaka Waziri anyongwe!

  Wakati Mh Mdee anachangia hoja na kushusha virungu, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Mwakyembe aliomba mwongozo wa Mwenyekiti wa Kikao; aliwasha kipaza sauti na kusimama kuomba mowngozo, Mwenyekiti alikataa akisema atashhughuilikia habari za Mwongozo baadaya!

  Mh Filikunjkombe naye alipoanza kuchangia akaja na lugha ngumu ngumu na kutaka Waziri anyongwe, wakati huo Mbunge mwingine (sikumbuki nani) akawasha kipaza sauti akiomba kutoa Taarifa, Mwenyekiti wa Kikao agaoma!

  Linalonishangaza na kunichosha ni jinsi sasa Spika na Wenyeviti wamekuja na syle mpya za kukataa miongozo na taarifa! Huu ni woga au ukandamizaji? Maana ni haki Wabunge kuomba mwongozo wa Spika au kutoa taarifa!

  Sasa Spika na Wenyevitai wanapozuia, wanakuwa wanaamnisha nini? Ni kushindwa, ubabe au ni kitu gani?

  Kwa hili nadhani sasa viongozi wa Bunge wame-prove failure, na wanafanya ukandamizaji na kukiuka kanuni zinazowapa Wabunge haki ya kuomba mwongozo wa Spika na kutoa taarifa wakati mchangiaji anapoendelea na hoja.
   
Loading...