DAVID PALMER
JF-Expert Member
- Jan 19, 2020
- 285
- 1,447
Nipo kijijini kwetu one time.. hapa home kwa wazazi wanafuga bata miaka mingi saana. Sasa ile siku nafika toka town waliniambia nichinje bata kwa ajili yangu mgeni. Then nikichinja niwaite washughulikie.
Basi nkamchagua bata, nkamshika. Nkashika kisu nkawa natoka nae nkamchinje. Pale nje nikawa nakinoa kile kisu huku nmemshika bata. Then nkaenda nyuma ya nyumba nkamchinja yule bata.
Ebwana ile nyama baada ya kupikwa haikua nzuri kabisa.. yaan sio nzuri kama tulivozoea. Mama akanambia, wewe inaonekana huyu bata kabla hujamchinja, ulimuonesha kisu kwa muda mrefu. Na ni kweli nmenoa kisu, nmezunguka nae kumchinja huku nna kisu mkononi.
Maza akasema ungeandaa kisu kwanza ndo ukamshike. Bata akiona kisu na huku umemshika anaficha damu, so nyama yote huharibika. Nilishangaa sana.
Ajabu ya pili ya bata ambayo hadi leo huwa sielewi ni hii. Bata akiwa anataga mayai..huyahesabu.. ukiwa na tabia ya kuchukua mayai yake, kila akija akute yanapungua, hususa kutaga. Na hatagi kweli.. sasa me huwa najiuliza, mayai ya tumbon huyapeleka wapi?? Sababu nnachohisi mimi kutaga mayai sio tendo la hiyari. Ni lazima..ni mwili wenyewe.. yeye anaamuaje kuacha kutaga???
Kubwa kuliko, bata ukimuua ukianza kumnyonyoa manyoya, yanaota mengine.. mfano ukianza mgongoni kabla hujafika tumboni basi mgongoni utaona vimeanza kutoa.. yaani unaweza ukakesha kunyonyoa. Hii ya juzi maza alichofanya ananyonyoaa then anabanika, ili kuvikausha na hivi vidogo vinavoota upya