Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Mwezi March mwaka 2014 serikali ilitumia Bilioni 375.9 kulipa mishahara kwa watumishi (Salaries and wages). Kumbuka kipindi hicho kulikua na watumishi hewa, kulikua na watu wanalipwa mishahara miwili miwili, kulikua na nyongeza ya mishahara, na watumishi wapya waliajiriwa kila mwaka.
Kipindi kama hicho (mwezi March) Mwaka 2018 serikali ilitumia Bilioni 527.4 kulipa mishahara. Kipindi kama hicho mwaka huu, serikali imetumia Bilioni 557.6 kulipa mishahara. Hizi ni takwimu rasmi kama zilivyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango. Yani gharama ya kulipa mishahara imekua ikiongezeka mwaka hadi mwaka licha ya kuondolewa wafanyakazi hewa na dili nyingine feki.
Kwa wale wachumi daraja la kwanza, hii inawezekanaje? Yani unaondoa wafanyakazi hewa, unazuia nyongeza ya mishahara, unazuia ajira mpya lakini gharama ya kulipa mishahara inazidi kuongezek. JK aliwezaje kuwa na wafanyakazi hewa na wote wakalipwa, akaweka nyongeza ya mishahara kila mwaka kwa watumishi wote hadi wale hewa, na akaweza kuajiri maelfu kila mwaka kwa gharama ndogo? Who can explain this Economic paradox?
By G malisa