Maajabu ya awamu ya 5: Peter Serukamba naye aomba msamaha kwa mchango wake alioutoa Bungeni, alikosoa ujamaa

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Wabunge wameendelea kumiminika katika kuomba msamaha kwa viongozi wa CCM kuhusu kauli wanazotoa lakini Selukamba ametoboa kosa lake hadharani.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Peter Selukamba (CCM) ameomba radhi bungeni kutokana na kauli aliyoitoa Juni mwaka huu katika mchango wake kuhusu kubeza ujamaa kwamba hakuwa na maana hiyo.

Selukamba ametumia kanuni ya 50 ya Bunge leo Septemba 12,2019 na kueleza kuwa alinukuliwa vibaya hata kusababisha usumbufu kwa chama chake na viongozi wake.

Huyu anakuwa mbunge wa kwanza kueleza hadharani kosa lililofanya aombe msamaha wakati wengine wamekuwa hawatajwi makosa yao hadharani.

Spika Job Ndugai alimuita Selukamba kuwa anampa muda mchache kueleza jambo lililombele yake ndipo mbunge huyo akasimama.

"Juni wakati nahitimisha hoja yangu hapa bungeni nlitumia neno ujamaa vibaya kwa kusema kuwa kama kuna jambo siliamini ni ujamaa,"amesema Selukamba.

"Naomba radhi chama changu naomba radhi kwa viongozi wangu kwa usumbufu wowote walioupa kuhusu kauli yangu, sikuwa na maana kama ilivyochukuliwa."


Selukamba amesema yeye ni zao la CCM, chama ambacho kinaamini katika ujamaa na hivyo na yeye ni mjamaa kama ilivyo kwa chama chake.

Mbunge huyo ameomba radhi ikiwa ni muda mfupi baada ya Spika Ndugai kutangaza bungeni kwa kuwashukuru wabunge Nape Nnauye, William Ngeleja na January Makamba kwamba walifanya jambo lenye maana kubwa kwa kumuomba radhi.
 
Sawa tu kuomba radhi, Ujamaa ndio itikadi ya CCM, usipoamini Ujamaa maana yake huwamini katika CCM.

Baada ya statement alipaswa moja kwa moja karudisha kadi CCM
 
Sijawahi kuona tija ya uwepo wa wingi wa wabunge wa CCM bungeni, kwa kuwa wingi huo huwafanya kuwa wanafiki mno. Licha ya kuwa ni watu wenye uzoefu ktk kila nyanja ya uongozi, weledi; combination nzuri ya wataalamu, jinsia, umri na mambo mengi muhimu. Wakiwa pamoja na kwa umoja wao hawana tija yoyote ile ktk hatma ya taifa letu. Lakini mbaya zaidi na wa kuonewa huruma zaidi ni Watanzania wenyewe, kwa kuzidi kuliamini kundi hili ijapokuwa sitaki kulifananisha na "Interahamwe".
 
Huyo mpuuzi na mnafiki tu,Mbona hajaomba msamaha Kwa wananchi wa kigoma kaskazin,hasa wakaz wa
mwambao waziwa Tanganyika kwa kauli yake aliyoitoa wakat wa kampen 2015 ambayo imekuwa gumzo hadi sasa kwakutofanikisha hata chembe ya barabara aliyoahidi.wananchi bado wanakumbuka kwamba wakufanyie nini kama ukishindwa.
 
Tuna kundi kubwa la wajinga bungeni ambao hata kutetea hoja zao hawawezi zaidi ya kutetea matumbo yao.
Ni kundi LA watu wasio jiamini na RAIA wapiga kura wamesha wagundua wanafiki hao
Naunga mkono hoja, tuna Bunge la ajabu na wabunge wa ajabu.

P
 
GENGE la JMT ni kikundi cha wahuni tu kama walivyo wahuni wengine maana hamnaga hata hoja jenzi zinazojadiliwa kama mabunge ya wenzetu
 
Mwakani ni uchaguzi,yaani full shobo,mbunge wangu hata ukija kuomba msamaha kuwa hakubahatika kutekeleza ahadi zako,sikusamehi ng'o na kura sikupi!
Nalog off
 
Aisee nimekutana na hii habari ikanishangaza kidogo, Mbunge Peter Serukamba wa CCM imembidi kuomba radhi kwa viongozi wake wa chama kutokana na mchango wake alioutoa Bungeni mwezi juni mwaka huu akikosoa sera za kijamaa na kusema haamini katika sera hizo

Hivi hili wimbi la wabunge kuomba radhi linajitokeza awamu hii pekee au pia lilikuwepo awamu nyingine za akina Mkapa kurudi Nyuma?

 
Kila mbunge sasa hivi anawaza jinsi ya kutetea jimbo lake kupitia ccm, na wabunge wote wa CCM Magufuli ndio ameshika mpini.

Hakuna namna inabidi wajipendekeze kwa nguvu zote ili panga la Magufuli lisiwakute.
 
Hapa ndipo wakati wa kuwagundua wabunge walio kwa ajili ya maslahi ya wananchi na wale walio kwa ajili ya maslahi yao binafsi
 
Hata mimi naomba msamaha kwa Serikali ya awamu ya tano kwa kujiita Monopoly wakati nchi ipo katika ujamaa
 
Chama ni itikadi, ni imani, ukiwa CCM unatakiwa ukubaliane na imani ya CCM kama vile vile ukiwa CDM au chama chochote cha siasa. Sasa ukipinga imani maana yake hupo nao. Na una njia mbili, moja kuondoka katika chama au kuboresha katika vikao vyenu au hata cha kijamii. Huyu alichofanya kama kabanwa huko ni sahihi.
Unaweza pinga vingine ila siyo imani. Ni sawa na padre kulaani mwenendo wa wakatoliki juu ya imani yao ambayo madhehebu mengine wanapinga, lazima ushughulikiwe ndani hata kutengwa...
Huyu alipinga kile kinachofanya CCM iwepo... Imani yao...
 
Back
Top Bottom