Maajabu! Wezi wakata mauno usiku kucha wakiwa uchi baada ya kuiba gari

Akhy D

JF-Expert Member
Jun 10, 2013
365
500
Juzi kati nilisikia kuna mmoja aliiba begi lakini baadae akaenda mwenyewe polisi na begi aliloiba.

*You get what you work for not What you wish for*
 
mwandende JR

JF-Expert Member
Aug 6, 2017
1,094
2,000
Aisee huko si ndy MAREHEMU ISSA MATONA alikimbiya SHOW LIVE baada ya JUMA BHALO kuimba nyimbo ya PETE?mpaka RAIS MOI akasimamisha SHOW hadi BHALO apewe PETE YAKE..... MATONA akakimbia....aisee hapafai hapo....mtoto wa kiume anachungwa kuliko BINTI...itakuwa hao wezi waliipata fresh USIKU huo baada ya kuiba vya watu.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MwendaOmo

JF-Expert Member
Dec 16, 2013
756
1,000
Kwangu ni rahisi kukubali kwamba mtu kategesha kitu kwenye gari kinachompa mwizi ugonjwa wa akili kuliko kuamini "uchawi".

Ukiniambia kuna madawa yametegeshwa katika gari kiasi kwamba mtu akija kuiba atasababisha ku trigger madawa hayo kuenea kwenye gari na kumharibu akili apaki gari na kuvua nguo na kuanza kucheza ngoma uchi, hilo linaweza kuwa explained biologically na chemically.

Ukiniambia gari lina uchawi itabidi unieleze huo uchawi unafanya kazi vipi.

Sent from my Kimulimuli

Madawa hayo pia yatamwezesha Nyoka kuwafwata ili wacheze naye?
 
wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
19,889
2,000
View attachment 582522
Habari zinazochipuka hii leo toka Mombasa Nchini Kenya, wezi wawili yapata jana jioni waliliiba gari la bwana mmoja alilokuwa ameliegesha sehemu apate kinywaji kishe aende zake home, baada ya mabwana hao kufanya tendo hilo leo asubuhi wananchi wametamaushwa kwa kuwakuta wanaume hao wakicheza muziki kulizunguka gari hilo huku wakiwa uchi.

Gari hilo wanalodaiwa kuwa waliiba walikuwa wameliegesha pembeni huku nyoka wako shingoni!

Aisee iwe funzo kwa wengine, Mombasa hata shilingi haiokotwi, utashtukia umeliwa jicho usiku kucha ohhoo!
Natamani huyo mganga angeletwa na huku bongo
 
Hoshea

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
5,069
2,000
Umesguhudia nini na unajuaje kwa hakika kwamba ulichoahuhudia ndicho?

Unaweza kushuhudia chemchemi ya maji jangwani, kumbe mirage.

Unaweza kushuhudia mtu kauawa, kumbe maigizo ya sinema.

Sent from my Kimulimuli
Jamaa unapendaga league sana, it seems una stress mob.
You can't see stress, but you can feel it, wind likewise. Witchcraft likewise, yaani kuna ulimwengu wa roho, ambao macho yetu ya nyama hayawezi kuuona.

Save your energy, utahitaji kutetea nyumbu wenzako kwenye threads zingine za siasa.
 
young MathematiciAn

Senior Member
Oct 31, 2016
160
500
Umesguhudia nini na unajuaje kwa hakika kwamba ulichoahuhudia ndicho?

Unaweza kushuhudia chemchemi ya maji jangwani, kumbe mirage.

Unaweza kushuhudia mtu kauawa, kumbe maigizo ya sinema.

Sent from my Kimulimuli
Hakuna cha sinema mkuu ,kwanza kuna dogo ghafla ilimtokea anapiga makelele na akaanza kukimbia watu wote walijua tayari uchizi umemuanza akakimbizwa wee akadakwa lkn alikuwa haeleweki akapelekwa muhimbili kwa dokta wa akili lkn mwisho tukagundua ni jini kaingiwa na kwa mahojiano wa yule jini ni kwamba yeye katumwa na usianze kubisha na kuleta mambo ya saikolojia ,kwa niliyoshuhudia kwa dogo mpaka matibabu yake amini uchawi upo na hili tukio usibishe sana kuna waganga watabe wapo kufanya maujinga haya wanaweza na hapo hao jamaa wapo unconscious ni majini wanafanya hivyo
 
Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,920
2,000
Jamaa unapendaga league sana, it seems una stress mob.
You can't see stress, but you can feel it, wind likewise. Witchcraft likewise, yaani kuna ulimwengu wa roho, ambao macho yetu ya nyama hayawezi kuuona.

Save your energy, utahitaji kutetea nyumbu wenzako kwenye threads zingine za siasa.

Wewe unayenijibu hupendi league?

Kwa nini unajibizana na mtu mwenye stress?

Wewe unayeamini vitu ambavyo havionekani wala kuthibitishika ni guluguja usiye na ubongo wala uti wa ubongo.

Unaenda kwa kujibiringita biringita tu.

Roho ni nini? Iko wapi? Unaweza kuthibitisha ipo na si stories tu?

Wacha kutetea ujinga hapa. Unatetea ujinga halafu unaniita mimi nyumbu wewe hayawani usiyejua la muadhini wala mchota maji msikitini?

Sent from my Kimulimuli
 
Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,920
2,000
Hakuna cha sinema mkuu ,kwanza kuna dogo ghafla ilimtokea anapiga makelele na akaanza kukimbia watu wote walijua tayari uchizi umemuanza akakimbizwa wee akadakwa lkn alikuwa haeleweki akapelekwa muhimbili kwa dokta wa akili lkn mwisho tukagundua ni jini kaingiwa na kwa mahojiano wa yule jini ni kwamba yeye katumwa na usianze kubisha na kuleta mambo ya saikolojia ,kwa niliyoshuhudia kwa dogo mpaka matibabu yake amini uchawi upo na hili tukio usibishe sana kuna waganga watabe wapo kufanya maujinga haya wanaweza na hapo hao jamaa wapo unconscious ni majini wanafanya hivyo
Unajuaje kwamba ni jini na si hallucination au any other mental condition?

Kuna mtaalamu wa magonjwa ya akili katoa ripoti kwamba magonjwa ya akili yameongezeka.

Wewe una utaalamu gani wa magonjwa ya akili kujua hili jini na si ugonjwa wa akili?

Sent from my Kimulimuli
 
Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,920
2,000
Imani kubwa sana za uchawi na dini (supernatural beliefs) ni moja kati ya sababu kubwa kabisa Waafrika ni masikini.

Wakiendelea kuendekeza imani hizo hawatatoka kwenye umasikini kwa miaka hata 200 ijayo.

Sent from my Kimulimuli
 
Hoshea

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
5,069
2,000
Wewe unayenijibu hupendi league?

Kwa nini unajibizana na mtu mwenye stress?

Wewe unayeamini vitu ambavyo havionekani wala kuthibitishika ni guluguja usiye na ubongo wala uti wa ubongo.

Unaenda kwa kujibiringita biringita tu.

Roho ni nini? Iko wapi? Unaweza kuthibitisha ipo na si stories tu?

Wacha kutetea ujinga hapa. Unatetea ujinga halafu unaniita mimi nyumbu wewe hayawani usiyejua la muadhini wala mchota maji msikitini?

Sent from my Kimulimuli

Wewe una uthibitisho wa kuwa hai kesho, una uthibitisho dunia, moon zina float aje kwenye maeneo yao. Una uthibitisho gani asteroids hazijaweza gongana na dunia.
There are superior unseen energies ewe nyumbu. Wewe usiyejua(not believing) haya mambo ndie mbumbumbu usie na ubongo wala uti wa mgongo.
 
Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,920
2,000
Wewe una uthibitisho wa kuwa hai kesho, una uthibitisho dunia, moon zina float aje kwenye maeneo yao. Una uthibitisho gani asteroids hazijaweza gongana na dunia.
There are superior unseen energies ewe nyumbu. Wewe usiyejua(not believing) haya mambo ndie mbumbumbu usie na ubongo wala uti wa mgongo.
Wewe hujui kwamba hata nikikosa uthibitisho wa vyote ulivyotaja, hilo halithibitushi Mungu yupo.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo guluguja wewe?

Sent from my Kimulimuli
 
nasssen

JF-Expert Member
Aug 12, 2012
476
500
Imani kubwa sana za uchawi na dini (supernatural beliefs) ni moja kati ya sababu kubwa kabisa Waafrika ni masikini.

Wakiendelea kuendekeza imani hizo hawatatoka kwenye umasikini kwa miaka hata 200 ijayo.

Sent from my Kimulimuli

Mkuu upo tayari kuwa lab rat or guinea pig kwenye hii ishu ya uchawi na ushirikina?? Hivi haujui kuwa kuna baathi ya vitu ni practically possible and they happen every day but theoretically you cannot make a reasonable explanation out of them?

This is Africa and waaaay before these white pigs came here we were practicing rituals and witchcraft as part of our normal social life. So the irony is you are so blinded by the western mode of life that you forget your own history.

Look around, you will be amazed how many things that happen are connected to supernatural powers. Welcome to Africa!!!
 
Niwe tayari mara ngapi? Mbona nishatoa challenge miaka kibao kama kuna mchawi aniloge na hakuna kilichotokea?

Kitu gani ambacho kiko practically possible lakini theorretically huwezi ku explain?

Na unajuaje kwamba hivyo vitu ni uchawi na si vitu vyenye explanation ambayo hujaijua tu?

Miaka 100- 130 iliyopita babu zetu hawakujua vitu kama radio na gramophone. Ungewaambia kwamba hii redio inayotoa sauti za kutoka mbali ni uchawi wa wazungu wangekuamini.

Leo tunajua redio inavyofanya kazi. Kisayansi.

Ukweli kwamba hawakujua redio inavyofanya kazi, ulifanya matangazo ya redio yawe uchawi?

Sasa na leo, unapoona kitu ambacho hukielewi na hakina explanation, unajuaje kwamba huu ni uchawi na si kitu tu ambacho si uchawi, bali hujakielewa tu?

Huoni kwamba kwa kukimbilia kusema huu uchawi kwa kitu ambacho hujakielewa vizuri unakuwa kama yule babu aliyeishi miaka 120 nyuma ambaye aliona matangazo ya redio ni "uchawi wa wazungu" wakati redio inaelezeka vizuri tu bila kuhitaji uchawi?

Sent from my Kimulimuli
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom